Kutoweza
kufanya kazi kwa pamoja baina ya rais na Congress kumezorotesha
kupitishwa kwa miswada na viongozi wa Republican.
Seneta
wa Republican na kiongozi wa walio wengi Mitch Mc Connell amepata
tena kiti chake katika jimbo la Kentucky.
Chama
cha Republican kimezoa viti vingi katika uchaguzi huo na kukifanya
kuchukua udhibiti wa taasisi hizo muhimu dhidi ya kile cha Democrat.
Kiongozi
wa zamani wa seneti kutoka chama cha Democratic , Harry Reid,
amemuita Mitch McConnell kumpongeza na akasema ilikuwa ni wazi kwamba
wapiga kura walitaka vyama vyote kushirikiana.
Mwenyekiti
wa Kamati ya kitaifa ya Republican Reince Priebus amesema kuwa umma
wa wamarekani umekiamini chama chake.
Sheikh
Salim Bakari Mwarangi ambaye ni mwanaharakati wa kampeni dhidi ya
itikadi kali alipigwa risasi wakati alipokuwa akirudi nyumbani kutoka
msikitini jumanne usiku.
Viongozi
sita wa dini ya kiislamu badhi yao wenye itikadi kali na wale walio
na misimamo ya wastani wameuawa mjini Mombasa tangu mwaka 2012.
Eneo
la pwani ya kenya lenye waislamu wengi limekumbwa na misururu ya
mashambuli ya mabomu yanoyoaminika kutekelezwa na watu walio na
uhusiano na kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia.
Rais
wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia
amesema baadhi ya wanachama wa baraza hilo wanaunga mkono hatua ya
kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara ya silaha. Haijajulikana
ni lini hatua hiyo itatekelezwa.
Mapigano
yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za
kimataifa kuhakikisha makubaliano ya amani yanatekelezeka. Mzozo
wa kuwania madaraka uliokuwepo kwa miezi kumi kati ya Rais Salva Kiir
na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar umegharimu maisha ya maelfu ya
Watu na takriban watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao.
Makubaliano
ya amani yaliyotiwa saini yalishindwa, kwa kuwa pande zinazokinzana
zilishindwa kuunda Serikali ya umoja
Hoteli
hiyo inatoa huduma kama vile vidimbwi vya kuoga vya wanyama
hao,vyumba vyenye hewa safi na vyakula vya kuvutia, na hivyobasi
kuimarisha viwango vya kuwabembeleza wanyama hao katika taifa hilo
lenye utajiri mkubwa.
Hoteli
hiyo yenye urefu wa futi 4,317 kwa jina Wagington Hotel imejengwa
katika nyumba za zamani za wakolini wa Uingereza zilizobadilishwa
katika makaazi ya wanadiplomasia.
Vyumba
vya kulalia katika hoteli hiyo vinagharimu dola 271 kwa mbwa watatu
wanaotumia kwa pamoja chumba cha kifalme,kilicho na maeneo ya
kifahari ya kuweka balbu,runinga,na vitanda vilivyotengezwa na ngozi.
Hoteli
hiyo iliojengwa hususan kwa mbwa pia huwakaribisha paka.
''iwapo
tunajitakia mema katika maisha yetu, kwa nini marafiki zetu walio
waaminifu nao tusiwafanyie mambo mazuri'' aliuliza mmiliki wa hoteli
hiyo Estelle Taylor.
''Kama
watu tunaowapenda wanyama,tuna hisi kwamba ni vyema kuwa na eneo
ambalo wanyama wanaweza kuwekwa ili nao wajisikie nyumbani''
aliongezea.
Wanaomiliki
wanyama hao pia wanaweza kupata eneo la kufanya mafunzo,kunyoa,
kukata kucha,kubadilisha rangi za wanyama hao pamoja na masaji.
Hoteli
hiyo pia hutoa huduma ya gari la kifahari aina ya Limousine kwa
wanyama hao kutoka makaazi yao hadi hoteli hiyo na kutoka hoteli hiyo
hadi makaazi yao.
Nchini
Singapore kuna zaidi ya maduka 250 ya wanyama, mengi yakiwa katika
maduka makubwa ya jumla.
Mfanyibiashara
mmoja hutoa huduma za kitalii kila wikendi ambapo wamiliki wa wanyama
hao na wanyama wenyewe hutembezwa katika maboti.
Shambulio
hilo lilitokea wakati wa mchana Nafada na kuharibu kituo cha polisi,
benki na ofisi ya chama
tawala cha (PDP).Mashahidi wa tukio hilo wanasema waliona miili ya
wanajeshi watano. Kiongozi wa dini ya kiislamu wa eneo hilo ameuawa
pia.
Mwandishi
wa BBC anasema wanamgambo wa kundi hilo wamevamia maeneo mengi
nakufanya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kuzidi kuanguka kutokana na
mashambulizi hayo.
Mashambulizi
hayo yanakuja siku baada ya kulipuliwa kwa bomu la kujitoa muhanga
katika jimbo la Yobe na kuuwa zaidi ya watu kumi na tano.
Wanajeshi
katika kambi ya jeshi ya Nyali iliopo mjini Mombasa pwani ya Kenya
wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 6 baada ya genge la wahalifu
kuvamia kituo hicho cha jeshi mapema leo.
Inadaiwa
kuwa kundi la watu 15 lilijaribu kuvamia kambi hiyo mwendo wa saa
kumi na moja alfajiri ya jumapili.
Wanajeshi
waliokuwa katika zamu waliweza kulidhibiti kundi hilo ambapo watu
watano waliuawa huku askari mmoja akiweza kujeruhiwa kwa kukatwa na
mapanga na wavamizi hao.
Kufikia
sasa maafisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha
shambulizi jilo.
Hatahivyo
wengi wanashuku watu hao huenda ni wanachama wa kundi la Mombasa
Republican Council MRC.
Lakini
msemaji wa kundi hilo Randu Nzai amekanusha habari hizo akisema kuwa
kundi hilo halikuhusika kamwe.
Wallenda
aliwastaajabisha watu waalipotembea akiwa amefunga macho kati ya
majengo ya Marina City huku akikumbana na upepo mkali uliokuwa
ukivuma kwa zaidi ya kilomita 40 kwa saa.
Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika kwa panya waliotungwa virusi walionyesha dalili tofauti kwa panya hao ambapo asilimia 19 walibaki bila kupata madhara ya virusi hivyo.
Hii inaweza kueleza kwa nini baadhi ya watu wanapona ugonjwa huu wakati wengine wakifa kwa maumivu, wamesema wanasayansi hao.
Mfanyakazi wa afya akimhudumia mgonjwa wa Ebola
Uchunguzi wao umechapishwa katika jarida la Sayansi.
Wanasayansi kutoka vyuo vikuu vya Washington na North Carolina, na Taasisi ya Afya ya Taifa huko Montana, waliwapima panya ambao walitungwa virusi vya aina moja vya Ebola vinavyosababisha milipuko huko Afrika Magharibi.
Ingawaje panya wote walipoteza uzito katika siku chache za kwanza baada ya kupandikizwa virusi, karibu mmoja kati ya watano alipata nguvu na hakuonyesha kuwa na dalili za ugonjwa.
Lakini asilimia 70%ya panya walikuwa wagonjwa taabani, baadhi yao wakionyesha dalili za ini kushindwa kufanyakazi na kundi kubwa wakitokwa na damu ambayo ilichukua muda mrefu kuganda.
Kirusi cha Ebola
Pia panya hawa walikuwa na tatizo la damu kuvujia ndani, kuvimba bandama na kubadilika kwa rangi ya ini.
Pia walikuwa na uwezekano mkubwa wa zaidi ya asilimia 50% kufa kutokana na ugonjwa huo.
Angela Rasmussen, kutoka Maabara ya Katze katika chuo kikuu cha Washington, amesema namna tofauti za madhara ya maambukizi kwa panya hao inaonyesha aina ya dalili zilizooneka kwa binadamu wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwaka 2014.
Watu walionusurika na ugonjwa wa Ebola hivi karibuni huenda wamekuwa na kinga dhidi ya virusi hivi au vinavyofanana, kinga ambayo imewaokoa.
Tanzania kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia 1,000
Tanzania imekubali kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia kama sehemu ya jitihada zake kusaidia amani na usalama nchini Somalia, lakini baadhi ya maofisa wa Tanzania wameelezea wasiwasi kwamba kujihusisha zaidi katika masuala ya Somalia kunaweza kukaribisha mashambulio ya kigaidi kutoka kwa al-Shabaab.Mapatano ya kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia 1,000 kwanza yalitolewa mwaka 2012, wakati Tanzania ilipokubali ombi la aliyekuwa rais wa Somalia Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambalo tena limerudiwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud mwaka huu. "Tumeandaa makambi ya mafunzo na wakati huu ninapozungumza kila kitu kiko tayari. Tunasubiri kutoka kwao kuteua askari 1,000 kuja hapa kwa ajili ya mafunzo, Tunasubiri kuwapa mafunzo kuwa askari wa kitaalamu ili kwamba wadumishe usalama wa nchi yao kutoa fursa ya kujihusisha katika masuala ya maendeleo." alisema Salva Rweyemamu, mkurugenzi wa mawasiliano wa rais wa Tanzania.
wengi huamini panya haliwi, lakini panya ni mboga kwa baadhi ya makabila nchini Tanzania, hususa mkoa kama wa Mtwara. hivyo panya ni nyama kama nyama zingine wanavyoamini wao.