Friday, 2 January 2015

BAADA YA KUKAA KIMYA HATIMAYE YULE ASKOFU ALIYEKULA PESA ZA ESCROW AELEZA ALIVYOPEWA MGAO HUO.


Askofu Nzigilwa.












Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, amevunja ukimya kuhusu mgao wa Sh. milioni 40 alioupata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIP Engineering & Marketing Limited, James Rugemalira.

Ukimya wa Askofu Nzigilwa unatokana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akaunti hiyo ilifunguliwa baada ya waliokuwa wanahisa wa Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwamo VIP kuingia katika mgogoro na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).

Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilisema fedha alizopewa Askofu Nzigilwa na Rugemalira, zilikuwa za matoleo kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa.

Alisema kiutaratibu siyo vibaya kwa waumini kutoa michango na matoleo kwa Kanisa na watumishi wake.

Katika taarifa hiyo ambayo Askofu Nzingilwa alipotafutwa alithibitisha kwamba ni yake, alifafanua kuwa alifahamiana na familia ya Rugemalira tangu akiwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Makongo Juu, Dar es Salaam na hata baada ya kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wameendelea kushirikiana na kuwasiliana katika masuala mbalimbali ya kikanisa na kijamii.

“Samahani nipo kwenye kazi fulani hatuwezi kuongea kwa sasa.

 Ni kweli kuna taarifa nimeitoa leo kwa Tumaini Media na nimewaambia waitume pia kwa vyombo vingine vya habari,” alisema Askofu Nzingilwa alipowasiliana na NIPASHE kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms).

Askofu Nzingilwa katika taarifa hiyo aliyoisaini juzi, alisema mwanzoni mwa Februari 2014, Rugemalira alimuomba namba ya akaunti yake ya benki ya Mkombozi ili aweke matoleo yake.

Alisema aliombwa akaunti yake na Rugemalira mapema Februari, mwaka jana na kwamba hakuwahi kufahamu kiasi cha fedha kilichowekwa kwenye akaunti yake hadi alipoangalia taarifa ya benki Februari 27, mwaka jana iliyoonyesha aliingiziwa Sh. milioni 40.4.

“Niliwasiliana na Rugemalira na kumwambia nimeona kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yangu, naye akaniambia hayo ni matoleo yake ambayo anaamini yatasaidia katika shughuli zetu za kitume na kichungaji. Nikamshukuru kwa ukarimu huo mkubwa,” alibainisha Askofu huyo.

Alisema matoleo hayo yalipokelewa kwa moyo mnyofu kutoka kwa mtu anayefahamika kwa ukarimu wake katika kusaidia Kanisa na watumishi wake.

“Kampuni anazomiliki na biashara anazofanya Rugemalira kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, haviwezi kumpa shaka mtu anayemfahamu kuhusu uwezo wake au kampuni yake kutoa mchango mkubwa kama huo,” alisema.

Alisema ni desturi ya kawaida katika Kanisa kwa waamini kutoa michango na matoleo mbalimbali kila mmoja kwa kadri ya uwezo na ukarimu wa moyo wake na kwamba matoleo ya waamini hutumika katika shughuli za uinjilishaji na uendeshaji wa Jimbo, Parokia na taaisi zake.

Askofu huyo aliongeza kuwa hutumika katika miradi maalum iliyokusudiwa na matoleo hayo na kwa kadri ya matakwa na lengo la mtoaji.

“Nilipokea matoleo hayo kwa roho safi na moyo mweupe na wa shukrani kama tunavyofanya siku zote tunapopokea ukarimu wa michango na matoleo ya waamini wetu. Na tangu matoleo hayo yalipotolewa Februari, mwaka jana, hakuna mamlaka yoyote iliyowahi kuniuliza ,” alifafanua na kuongeza:

“Nawaomba waamini tuendelee kujitoa kwa hali na mali katika kulijenga Kanisa la Mungu; kila aliyepewa talanta na Mungu aitumie kwa kuzalisha matunda mema ili kulijenga kanisa letu na hatimaye kuurithi ufalme wa mbinguni.”

Hata hivyo, alisema Kanisa hilo litaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki, ukweli na uadilifu, na halitarudi nyuma wala kukaa kimya katika kukemea maovu katika jamii.

UHUSIANO NA FAMILIA YA RUGEMALIRA
Alisema familia ya Rugemalira ni waumini wakatoliki wanaosali katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu, Makongo juu katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kwamba ni washiriki wazuri katika shughuli za ibada na wamekuwa na moyo mkubwa wa ukarimu katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kanisa ndani na nje ya jimbo.

“Binafsi, nimeifahamu familia hii muda mrefu kutokana na majitoleo yao katika shughuli za Kanisa na uhusiano baina yangu na familia hiyo ulizidi kuimarika pale alipopangwa kufanya huduma za kichungaji katika Parokia ya Makongo Juu nikiwa Paroko Msaidizi, mwaka 2008,” alibainisha na kuongeza:

“Kipindi hicho ilikuwa katika harakati za ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba ya mapadre na mikakati ya ujenzi wa Kanisa jipya la Parokia na walikuwa wachangiaji wazuri katika kufanikisha.”
Hata hivyo, aliwaomba waumini wa kanisa hilo kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika kulijenga Kanisa la Mungu.

Aidha, Askofu huyo alisema utume wa kanisa siku zote umekuwa ukiwezeshwa na kutegemezwa kwa nguvu ya Mungu Roho Mtakatifu anayeliongoza kanisa katika ukweli wote, na kwa sadaka, matoleo na michango mbalimbali ya hali na mali kutoka kwa waamini na watu wengine wenye mapenzi mema waliopo ndani na nje ya nchi.

“Kwa waumini kutoa michango na matoleo kwa kanisa na watumishi wake ni jambo la kawaida katika desturi za imani yetu tangu nyakati za mitume,” alisema Askofu Nzigilwa.

KASHFA YA ESCROW
Mei, mwaka jana, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, aliibua kashfa ya kuchotwa kwa zaidi ya Sh bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali na Mbunge huyo kutakiwa kufuta kauli kwa kulidanganya Bunge.

Mbunge huyo aliendelea na msimamo wake na kutaka Bunge kuunda kamati ya kuchunguza sakata hilo.Juni mwaka jana, Bunge liliagiza Ofisi ya CAG kufanya ukaguzi wa fedha hizo na ripoti yake kuwasilishwa Bungeni.

Baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukamilisha kazi yake, ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya uenyekiti wa Zitto Kabwe.
 
Kamati hiyo ilifanya uchunguzi na kuweka wazi ripoti na mapendekezo yake ya awali ambayo yalizua mjadala mkali bungeni kiasi cha kutishia Bunge kushindwa kufikia maamuzi ya pamoja na baadaye Spika Anne Makinda, aliunda kamati ya maridhiano ambayo ilikubaliana katika maazimio yaliyowasilishwa Bungeni na Zitto.

Novemba 26, mwaka jana, Zitto, aliwasilisha ripoti iliyowataja viongozi wa dini, serikali na watu wengine waliopokea fedha za Tegeta Escow.

Viongozi wa dini waliotajwa na Zitto kiasi cha fedha walichopokea kwenye mabano ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini (Sh. milioni 80)  Askofu Eusebius Nzigirwa na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh. milioni 40.4), ambao walipewa fedha hizo kupitia Benki ya Mkombozi.

VIONGOZI WA SERIKALI WALIOWAJIBIKA
Desemba 16, mwaka jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, alijiuzulu nafasi kutokana na ushauri alioutoa.

Desemba 22, mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete, alimfukuza kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye katika kashfa hiyo alipokea kiasi cha Sh. bilioni 1.6, huku akimuweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Desemba 23, mwaka jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alimsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

VIONGOZI WENGINE WALIOPATA MGAWO
Viongozi waliopata mgawo wa Rugemalira Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (bilion 1.6); Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (milioni 40.4); Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona (milioni 40.4); Mbunge mstaafu Paul Kimiti (milioni 40.4); Msajili wa zamani wa Hazina na Mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk. Enos Bukuku (milioni 161.7).

Wamo pia Jaji Profesa Eudes John Ruhangisa (milioni 404.25) na Jaji Aloysius Mujulizi (milioni 40.4).

Watumishi wa umma ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa wa Rita, Philip Saliboko (milioni 40.4); aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Emmanuel Ole Naiko (milioni 40.4) na Mtumishi wa TRA, Lucy Appolo (milioni 80.8).
Share:

PANYA ROAD WAZUA TAFRANI DAR..



































Picha hii ni moja ya vingozi wa kundi hilo ambao kamishna kova aliwahi kuudhibitishia mtandao huu kuwa wamefanikiwa kuukamata mtandao wa wahuni hao lakini sasa wameibuka tena jijini Dar es salaam
Hali ya sintofahamu imetanda katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam usiku huu baada ya vijana wanaofanya fujo maarufu kama PANYA ROAD kuingia barabarani usiku huu kufanya fujo na kuvuruga hali ya amani katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es salaam.vijana hao wameanzia fujo hizo katika maeneo ya magomeni kagera na kusambaa maeneo yote ya magomeni,mabibo na kuelekea maeneo ya sinza na kufanya shughuli zote za kiuchumi kufungwa ikiwa ni pamoja na maduka na shughuli za ushafiri kusimama kwa muda kupisha vijana hao ambao haieleweki wanadai nini ila wao wanapiga kila wanayekutana naye mtaani.
maeneo ya sinza muda huu kukiwa hakuna shughuli zinazoendelea na badala yake wananchi wanalazimika kukaa majumbani mwao kuokoa maisha yao juu ya vijana hao ambao wanatembea kimakundi wakiwa na silaha a jadi kama mapanga,mawe na siaha nyingine.
Baadhi ya wanachi waliozungumza, wamelitupia lawama jesho la polisi kwa kushindwa kuwadhibiti vijana hao kwani wameanza harakati hizi zamani lakini jeshi la polisi limekuawa likishindwa kuwachukulia hatua madhubuti kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa hawakai kwa amanai kuogopa fujo hizo.

Wananchi wanaoishi maeneo ya sinza,kwa mtogole,magomeni,mabibo na viunga vyake wanashauriwa kutokuzurura ovyo mitaani muda huu kwani vijana hao wapo maeneo hayo na bado hawajaondoka.

Share:

Ajali ya pikipiki Magomeni Usalama.




kumetokea ajali mbaya maeneo ya magomeni usalama ikihusisha pikipiki (bodaboda) na coaster ambapo dereva wa pikipiki na abiria wake wameumia vibaya.

Dereva pikipiki amevunjika mguu katika ajali hiyo na abiria wake amevunjika mkono na kuumia vibaya kichwani.

Polisi waliokuwa eneo hili wamewachukua majeruhi hao na kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kupata huduma ya kitabibu.

Usafiri wa pikipiki kwa upande mwingine unasaidia sana
hasa katika dharura au foleni ya magari. Ajali za pikipiki zinakuwa nyingi kwa sababu madereva walio wengi hawana ujuzi na uzoefu wa kuendesha pikipiki.
Share:

Utafiti waelezea sababu za saratani.














Utafiti mpya unasema aina nyingi za ugonjwa wa saratani ni matokeo ya bahati mbaya, kuliko malezo ya vinasaba, mazingira na mtindo wa maisha.
Watafiti nchini Marekani walichunguza aina 31 za saratani na kugundua kwamba theluthi mbili zilisababishwa na mgawanyiko holela wa seli. Kwa mgawanyiko wa kila seli kuna hatari ya mabadiliko yanayoweza kusababisha saratani.
Wanasayansi hao wanasema kuimarisha mtindo wa maisha na mazingira kunasaidia kudhibiti magonjwa kama ya saratani ya ngozi na saratani ya mapafu.
Share:

Idara ya polisi yaongoza kwa ufisadi TZ. source BBC


Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Ripoti hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya hongo zote zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka uliopita.
Ya pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia mfukoni asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.
kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi nchini Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.
Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.
Utafiti huo ulifanywa mwezi Julai na Agosti mwaka uliopita na shirika la lenye na maslahi ya kimaendeleo barani afrika ForDIA likishirikiana na Jukwaa la uwazi nchini tanzania Trafo.
Share:

UN:Itachukua mda mrefu kuangamiza EbolaUN:Itachukua mda mrefu kuangamiza Ebola.


Kiongozi wa ujumbe wa ebola katika shirika la Umoja wa Mataifa amesema kuwa harakati za kukabiliana na ugonjwa huo zinazochukuliwa hazijafikia kiwango cha kuuangamiza katika eneo la Afrika Magharibi.
Katika mkutano na vyombo vya habari nchini Ghana,Tony Banburry amesema kuwa jamii ya kimataifa imekuwa ikikabiliana na ugonjwa huo na huenda ikachakua mda mrefu kabla ya kudhibitiwa.
Hatahivyo amesema kuwa anaamini jamii ya kimataifa itafaulu katika kuuangamiza mlipuko huo mwaka 2015.
Virusi vya ugonjwa huo vimewaua takriban watu 8000 hususan nchini Sierra Leone ,liberia na Guinea.
Share:

Wednesday, 31 December 2014

Aua watu 8 naye ajiua Canada.



Polisi Nchini Canada wanasema kuwa watu 8 wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mmoja ambaye naye alijiuua katika kile kilichotajwa kama mfululizo wa unyanyasaji wa majumbani.
Siku ya jumatatu polisi walikuta mwili wa mwanamke mmoja katika mji wa Edmonton eneo magharibi mwa jimbo la Alberta.
Polisi pia waliikuta miili mingine ambayo ni ya wanawake watatu,wanaume wawili na watoto wawili wakati ilipokuwa ikishughulikia taarifa ya mtu huyo aliyejiua katika eneo jingine kwenye mji huo.
Muuaji huyo alijiua mwenyewe kwenye mgahawa mmoja katika eneo la kaskazini mwa Edmonton.
Polisi bado haijatoa majina wala uhusiano wa waathirika.
Share:

Miili 40 yaopolewa baharini.


Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.
Share:

Boko haram wavamia kijiji na kuua 15.


Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.
Shambulizi hilo lilitokea katika kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga askari wa ulinzi wa jadi wa mji huo.
Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, liliwateka nyara wasichana wa shule zaidi ya mia mbili mwezi Aprili mwaka huu.
Zaidi ya watu elfu kumi wameuwawa Nchini Nigeria na Boko Haram mwaka huu pekee.
Share:

Rais Jammeh:'Bado niko mamlakani.


Rais wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.
Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.
Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.
Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa.
Share:

MTUHUMIWA ALIYEJARIBU KUTOROKA MAHAKAMA YA KISUTU APIGWA RISASI.


























Maofisa wa Polisi na Magereza wakiangalia mwili wa mtu aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya dawa za kulevya na kupigwa risasi wakati akijaribu kutoroka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam saa 2:00 asubuhi ya leo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinapasha kuwa mwili wa marehemu huyo ambaye bado jina lake halijatambulika umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Muhimbili. Picha kwa hisani ya Father Kidevu.
Share:

Monday, 29 December 2014

Watoto wazuiwa kuitembelea Israel.


Kundi la Hamas limewazuia kundi la watoto kutoka ukanda wa Gaza wengi wakiwa ni wale waliowapoteza wazazi kwenye vita vya hivi majuzi kati ya Hamas na Israel waliotaka kuitembelea Israeli katika ziara ambayo waandalizi wake wanasema ililenga kuleta uwiano. Msemaji wa Hamas anasema kuwa ziara hiyo ilizuiwa ili kulinda tamaduni ya watu wa ukanda wa Gaza.
Wapiganaji wa kundi la Hamas wamezuia kundi la watoto kutoka Gaza wengi wao wakiwa ni wale ambao wazazi wao waliuawa katika vita.
Wanaharakati wa masuala ya Amani waliowasaidia watoto hao kufanya safari hiyo wamesema kuwa mamlaka ya Gaza waliruhusu watoto hao kufanya safari yao lakini wakabadili msimamo wao baadae.
Share:

Filamu ya Interview yatikisa mitandaoni.


Kampuni ya Sony Picutues inasema kuwa - the interview - ambayo ni filamu yenye utata ya dhihaka kuhusu njama ya kumuua kiongozi wa korea kasakzini Kim Jong un imekuwa yenye mafanikio zaidi mtandaoni.
Kampuni hiyo inasema kuwa filamu hiyo imenunuliwa na pia kukodishwa zaidi ya mara milioni mbili kwa muda wa siku nne tangu iwekwe kwenye mitandao.
Sony iliahirisha mpango wake wa filamu baada ya komputa za kampuni hiyo kudaiwa kuingiliwa na wadukuzi,huku Korea Kaskazini ikihusishwa katika udukuzi huo.
Share:

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama.


Waokoaji wamekuwa wakipambana na upepo mkali pamoja na mawimbi ya bahari gizani kuwakoa karibu abiria 300 ambao wamekwama ndani ya ferry moja ya Italia iliyokuwa imeshika moto kwenye bahari ya Adriatic.
Maofisa nchini Italia wanasema kuwa oparesheni ya uokoaji itandelea.Hadi sasa watu 190 wamekolewa kutoka kwa ferry hiyo.
Share:

Abiria miamoja wakwama:ATC


Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya ATC wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari zao kuarishwa. Wengi wao wakielekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, kuelekea Mtwara na Kigoma wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.
Abiria hao imebidi wakodiwe hoteli ilivyo ada wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka lini
Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.
Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro….Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.
Share:

Sunday, 28 December 2014

Feri ya abiria 460 yashika moto Ugiriki.


Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki kwenda Italia.
Abiria waliokuwa kwneye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe .
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.
Share:

Mashindano ya Miss Tanzania yafungwa..


Serikali ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.
Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.
Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.
Alisema bwana Mgereza:"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,"
Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.
Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.
Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika
Share:

Indonesia yasitisha utafutaji wa Airasia.


Indonesia imesitisha utafutaji wa ndege ya AirAsia hadi kesho iliopotea na takriban abiria 160 waliokuwa wakielekea Singapore kutoka mji wa Surabaya nchini Indonesia.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.
Takriban abiria 162 walikuwa wakiabiri ndege hiyo aina ya Airbus 320 wengi wao wakiwa raia wa Indonesia.

Rubani wa chombo hicho anadaiwa kutaka kubadilisha njia ili kuepuka kimbunga lakini hakuomba usaidizi wowote.
Baadhi ya meli katika eneo hilo zinaendelea kuitafuta ndege hiyo,licha ya hali mbaya ya hali ya anga
Familia na marafiki wa waathiriwa wamekongamana nchini Singapore na uwanje wa ndege wa surabaya wakingojea habari kuhusu ndege hiyo.
Share:

Saturday, 27 December 2014

Tibaijuka:Nitatetea kiti changu.


Siku kadhaa tu baada ya rais Kikwete kumfuta kazi Anne Tibaijuka kama waziri wa ardhi,nyumba na makao ,kiongozi huyo amewaambia wakaazi wa bunge lake kwamba hawakumchagua kama waziri bali kama mwakilishi wao wa bunge, kulingana na gazeti la The citizen nchini Tanzania.
Tibaijuka alipigwa kalamu kutokana na maadili yake kufuatia kashfa ya akaunti ya tageta escrow ambapo alipokea sh.billioni 1.6.'' Mungu anayetoa ndiye aliyechukua jina la mungu libarikiwe alisema tibaijuka akimaanisha kuwa yule aliyempa kiti hicho cha uwaziri ndiye aliyekichukua.
Katika kile alichoelezea kama harakati za kukitetea kiti chake katika uchaguzi wa 2015,Tibaijuka aliwaonya wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ndiyo chagua bora la wapiga kura.
Kulingana na The Citizen kiongozi huyo aliwashukuru wapiga kura wa eneo bunge lake kwa kumchagua kuwa mbunge,wadhfa aliodai kumfungulia milango ya kupewa uwaziri.
''Lazima muelewe kwamba ninyi mulinipigia kura mimi ili niwahudumie bungeni na sio kama waziri,kwa hivyo yaliotokea si ndwele tugange yajayo kwa kuwa tayari kashfa ya escrow imezikwa'',aliwaambia wakaazi wa Muleba.
Hatahivyo bi Tibaijuka amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na viongozi wa upinzani waliochaguliwa katika uchaguzi wa madiwani wa hivi karibuni.
Share:

Korea Kazkazini yamtusi Obama.


Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananisha rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa kwa filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.

Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.
Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.