Tanzania kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia 1,000
Tanzania imekubali kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia kama sehemu ya jitihada zake kusaidia amani na usalama nchini Somalia, lakini baadhi ya maofisa wa Tanzania wameelezea wasiwasi kwamba kujihusisha zaidi katika masuala ya Somalia kunaweza kukaribisha mashambulio ya kigaidi kutoka kwa al-Shabaab.Mapatano ya kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia 1,000 kwanza yalitolewa mwaka 2012, wakati Tanzania ilipokubali ombi la aliyekuwa rais wa Somalia Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambalo tena limerudiwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud mwaka huu. "Tumeandaa makambi ya mafunzo na wakati huu ninapozungumza kila kitu kiko tayari. Tunasubiri kutoka kwao kuteua askari 1,000 kuja hapa kwa ajili ya mafunzo, Tunasubiri kuwapa mafunzo kuwa askari wa kitaalamu ili kwamba wadumishe usalama wa nchi yao kutoa fursa ya kujihusisha katika masuala ya maendeleo." alisema Salva Rweyemamu, mkurugenzi wa mawasiliano wa rais wa Tanzania.