Menu - Pages

Tuesday, 4 November 2014

Kambi ya jeshi yavamiwa Mombasa,Kenya


Wanajeshi katika kambi ya jeshi ya Nyali iliopo mjini Mombasa pwani ya Kenya wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 6 baada ya genge la wahalifu kuvamia kituo hicho cha jeshi mapema leo.
Inadaiwa kuwa kundi la watu 15 lilijaribu kuvamia kambi hiyo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ya jumapili.
Wanajeshi waliokuwa katika zamu waliweza kulidhibiti kundi hilo ambapo watu watano waliuawa huku askari mmoja akiweza kujeruhiwa kwa kukatwa na mapanga na wavamizi hao.
Kufikia sasa maafisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha shambulizi jilo.
Hatahivyo wengi wanashuku watu hao huenda ni wanachama wa kundi la Mombasa Republican Council MRC.

Lakini msemaji wa kundi hilo Randu Nzai amekanusha habari hizo akisema kuwa kundi hilo halikuhusika kamwe.

Nick Wallenda alivuka mto Chokago kuanzia kwenye orofa ya Maria City Tower hadi upande wa pili kwenye jengo la leo Burnett

Wallenda aliwastaajabisha watu waalipotembea akiwa amefunga macho kati ya majengo ya Marina City huku akikumbana na upepo mkali uliokuwa ukivuma kwa zaidi ya kilomita 40 kwa saa. 


Vigezo vya kijenetiki vinaweza kuwa sababu muhimu kumwezesha mtu kunusurika na maambukizi ya virusi vya Ebola, wanasema wanasayansi wa Marekani.

Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika kwa panya waliotungwa virusi walionyesha dalili tofauti kwa panya hao ambapo asilimia 19 walibaki bila kupata madhara ya virusi hivyo.
Hii inaweza kueleza kwa nini baadhi ya watu wanapona ugonjwa huu wakati wengine wakifa kwa maumivu, wamesema wanasayansi hao.
Mfanyakazi wa afya akimhudumia mgonjwa wa Ebola
Uchunguzi wao umechapishwa katika jarida la Sayansi.
Wanasayansi kutoka vyuo vikuu vya Washington na North Carolina, na Taasisi ya Afya ya Taifa huko Montana, waliwapima panya ambao walitungwa virusi vya aina moja vya Ebola vinavyosababisha milipuko huko Afrika Magharibi.
Ingawaje panya wote walipoteza uzito katika siku chache za kwanza baada ya kupandikizwa virusi, karibu mmoja kati ya watano alipata nguvu na hakuonyesha kuwa na dalili za ugonjwa.
Lakini asilimia 70%ya panya walikuwa wagonjwa taabani, baadhi yao wakionyesha dalili za ini kushindwa kufanyakazi na kundi kubwa wakitokwa na damu ambayo ilichukua muda mrefu kuganda.
Kirusi cha Ebola
Pia panya hawa walikuwa na tatizo la damu kuvujia ndani, kuvimba bandama na kubadilika kwa rangi ya ini.
Pia walikuwa na uwezekano mkubwa wa zaidi ya asilimia 50% kufa kutokana na ugonjwa huo.
Angela Rasmussen, kutoka Maabara ya Katze katika chuo kikuu cha Washington, amesema namna tofauti za madhara ya maambukizi kwa panya hao inaonyesha aina ya dalili zilizooneka kwa binadamu wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwaka 2014.
Watu walionusurika na ugonjwa wa Ebola hivi karibuni huenda wamekuwa na kinga dhidi ya virusi hivi au vinavyofanana, kinga ambayo imewaokoa.