Polisi
wamebadilisha mashtaka ya mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa
kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu,
kutoka kwa kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la
mauaji.
Video
hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila babake
mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi
wenegine.
Mfanyakazi
huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la
Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha
41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.
Mwanamke
huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.
Hata
hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka
dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha
mkuu wa mashitaka.
Tumuhirwe
alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tuki olililonaswa
kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili
na kubaini kuwa ana akili timamu.
Afisaa
mkuu wa polisi Fred Enaga, amewaonya waajiri kuchunguza mbinu
zinazotumika kuwachagua wasichana wa kazi, kwa sababu matendo kama
haya yanaweza kutokana na matatizo ya kisaikologia.
Waziri
wa Jinsia, Kazi na maendeleo ya jamii Bi Mary Karooro Okurut
alipongeza juhudi za wazazi wa mtoto huyo Arnella "kutokana na
kitendo hicho kwa mtoto. Ingekuwa mtu mwingine angemuua mischana huyo
wa kazi lakini alifuata sheria. Pia tunapeleka marekebisho katika
katiba kuhusu maslai ya watoto bungeni kuimarisha sheria zinazowajali
watoto," alisema waziri huyo.
Polisi
wamesema kuwa nia ya shambulio hilo haijatambulika na pia msichana
huyo amefanyia kazi familia hiyo kwa siku 26 pekee. Wazazi wamesema
kuwa mtoto huyo ametolewa hosipitalini na hali yake ya afya
inaimarika.
Kulingana
na msemaji wa polisi Fred Enaga, kesi hiyo iliripotiwa na Baba ya
mtoto Erick Kamanzi mnamo tarehe 13 Novemba katika kituo cha polisi
cha Kiwatule baada ya kuona video hio.
Kesi
hiyo ilipelekwa kwa kitengo cha polisi cha Kiira. Baada ya uchunguzi,
msichana huyo wa kazi alihukumiwa na shataka la mateso katika
mahakama ya Nakawa na kuzuuliwa katika gereza la Luzira.
Bwana
Enaga alisema Bi Tumuhirwe alishtakiwa chini ya kifungo cha tatu
kwenye katika kinacholinda maslahi ya watoto. Kifungo hicho
kinajumuisha mashataka kama ya kutesa inayopeana uwezekano wa
kumfunga mtu hadi miaka 15 gerezani.
Hata
hivyo, Bwana Enaga anashauriana na mkurugegenzi wa pande za mashtaka
kurebisha hukumu hilo kuwa kifungu cha maisha.