Ndege ya jeshi la KDF nchini Kenya imeanguka katika eneo la Kismayu nchini Somali.
Ndege
hiyo ilianguka siku ya Alhamisi mwendo wa saa tisa na robo ilipokuwa
ikirudi Kenya baada ya kutekeleza mashambulizi katika eneo la Jamaame
kusini mwa Somalia.
Kulingana na msemaji wa Jeshi kanali david
Obonyo: ''Ndege ya KDF iliokuwa ikirudi nchini Kenya baada ya kufanya
mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somali,ilikumbwa na
matatizo ya kiufundi na kuanguka katika eneo la Kismayu .
Kanali Obonyo hata hivyo hakusema iwapo kulikuwa na majeruhi yoyote.
Jeshi
la Kenya limesema kuwa ndege hiyo ilianguka kutokana na hitilafu za
kimitambo baada ya kufanya oparesheni katika eneo la Jamaane Kusini mwa
Somalia.
Hata hivyo baadhi ya mitandaoa iliyohusishwa na kundi la
AL shabaab imechapisha habari kuwa AL shabaab wamedai kuwa ndio
waliodungua ndege hiyo mwendo wa saa tisa Alasiri, Afrika Mashariki.
Msemaji
wa kiksoi cha kivita cha Al shabaab Sheikh Abdi Azizi Abu Musab
amenukuliwa akisema kuwa walishambulia ndege hiyo kwa kombora baada ya
kulipua kijiji cha Bulaguduud.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa
idhaa ya kisomali, ni vigumu kwa Al Shabaab kufanya shambulio kama hilo
katika mji wa Kismayu kwa kuwa eneo hilo zima limefurika vikosi vya
usalama vya AMISOM.
Mnamo mwaka wa 2012, majeshi ya Kenya
yaliuteka mji wa bandari wa Kismayu, unaotazamiwa kuwa mji muhimu sana
wa kiuchumi katika eneo zima la Somalia kutoka kwa wanamgombo hao wa Al
shabaab.