Menu - Pages

Saturday, 27 December 2014

Tibaijuka:Nitatetea kiti changu.


Siku kadhaa tu baada ya rais Kikwete kumfuta kazi Anne Tibaijuka kama waziri wa ardhi,nyumba na makao ,kiongozi huyo amewaambia wakaazi wa bunge lake kwamba hawakumchagua kama waziri bali kama mwakilishi wao wa bunge, kulingana na gazeti la The citizen nchini Tanzania.
Tibaijuka alipigwa kalamu kutokana na maadili yake kufuatia kashfa ya akaunti ya tageta escrow ambapo alipokea sh.billioni 1.6.'' Mungu anayetoa ndiye aliyechukua jina la mungu libarikiwe alisema tibaijuka akimaanisha kuwa yule aliyempa kiti hicho cha uwaziri ndiye aliyekichukua.
Katika kile alichoelezea kama harakati za kukitetea kiti chake katika uchaguzi wa 2015,Tibaijuka aliwaonya wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ndiyo chagua bora la wapiga kura.
Kulingana na The Citizen kiongozi huyo aliwashukuru wapiga kura wa eneo bunge lake kwa kumchagua kuwa mbunge,wadhfa aliodai kumfungulia milango ya kupewa uwaziri.
''Lazima muelewe kwamba ninyi mulinipigia kura mimi ili niwahudumie bungeni na sio kama waziri,kwa hivyo yaliotokea si ndwele tugange yajayo kwa kuwa tayari kashfa ya escrow imezikwa'',aliwaambia wakaazi wa Muleba.
Hatahivyo bi Tibaijuka amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na viongozi wa upinzani waliochaguliwa katika uchaguzi wa madiwani wa hivi karibuni.

Korea Kazkazini yamtusi Obama.


Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananisha rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa kwa filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.

Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.
Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.

Wanaume waliooana wapunguziwa hukumu.


Mahakama moja ya Misri imepunguza hukumu ya watu wanane waliodaiwa kushiriki katika ndoa ya watu wa jinsia moja kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja.
Mwezi Uliopita ,wanane hao walipatikana na hatia ya kuchochea uasherati.
Walishtakiwa baada ya kanda moja ya video kusambaa katika mitandao ikiwaonyesha wakisherehekea katika boti moja lililokuwa mto Nile huku wanaume wawili wakionekana wakivalishana pete na kukumbatiana.

Watu hao baadaye walikataa kwamba ilikuwa harusi ya watu wa jinsia moja.
Ushoga ni kinyume na utamaduni wa Misri ,ijapokuwa si kinyume na sheria.
Wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu wanasema kuwa kampeni dhidi ya mashoga imeimarishwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni nchini Misri.

Kiongozi wa Al-Shabaab akamatwa.


Maafisa nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali.
Kamishna wa Wilaya ya El Wak mjini Gedo ameiambia BBC Somalia kwamba vikosi vya usalama vilimkamata Zakariya Ismail Ahmed Hersi katika maficho yake ndani ya nyumba moja baada ya kupashwa habari.
Mwaka 2012 Marekani ilitoa zawadi ya dola millioni 3 kwa yeyote yule ambaye angeweza kutoa habari za Hersi.
Kundi la Al Shabaab limejiondoa kutoka miji kadhaa nchini Somalia tangu uzinduzi wa mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo yanayotekelezwa na vikosi vya AMISOM vikishirikiana na wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Bwana Hersi alikuwa kiongozi wa kundi la Alshabaab upande wa Amniyat.
Mapema mwaka huu alikosana na kiongozi wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane ambaye aliuawa katika mashambulizi ya Marekani mnamo mwezi Septemba.