Menu - Pages

Saturday, 17 January 2015

Huduma ya kuokoa watumishi wa Umma Kenya..

Serikali ya Kenya imeanzisha mpango kabambe wa kutoa huduma za kuokoa kwa kutumia ndege na magari kwa watumishi wa umma nchini humo. Huduma hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano na shirika la bima ya afya,shirika la msalaba mwekundu na kundi lamadaktari wanaosafiri kwa ndege la AMREF. Kenya inakuwa nchi ya pili baada ya Afrika Kusini kutoa huduma ya aina hii. Victor Kenani alkuwepo kwenye uzinduzi wa mpango huo ambapo Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria.




Bondia Muhammad Ali anaendelea vizuri..


Hali ya afya ya gwiji wa zamani wa ndondi Duniani Muhammad Ali inaendelea vizuri
Bondia huyo alirudishwa hospital kwa tatizo la maradhi ya maambukizi ya njia ya mkojo.
Msemaji wa familia Bob Gunnell alisema "Ali yuko imara na anatarajiwa kutolewa leo,kulikua na uchunguzi zaidi juu ya maambukizi yake.
Ali mwenye miaka 72 kabla alitolewa hospitali mapema mwezi huu baada ya kupatiwa mabaibatu kwa wiki mbili kwa maradhi yanayomsumbua.
Bondia huyo aliwahi kuwa bigwa wa dunia kwa uzito wa juu alistaafu mchezo huo mwaka 1981.

Marekani yalaani ICC kuhusu Israel.


Marekani imelaani hatua ya mahakama ya kimaitaifa ya uhalifu wa kivita ICC kuanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa uhalifu wa kivita kwenye utawala wa Palestina.
Msemaji wa wizara ya ndani nchini Marekani anasema kuwa ni jambo lisiloaminika kuwa Israeli ambayo imekuwa ikishambuliwa kwa makombora yanayofyatuliwa katika ardhi yake kuwa sasa ndiyo inayochunguzwa na ICC.
Mapema Isreal iliitaja hatua hiyo kama yenye lengo la kuizuia isijilinde kutokana na vitendo vya kigaidi.
Uchunguzi huo ambao ICC inasema utakuwa huru utatumiwa kuamua iwapo kutafanyika uchunguzi ulio kamili.

Dubai inaongoza kwa uaminifu..


Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.
Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake.
Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa ameificha kamera yake na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan, mwenye miaka 25, walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko Dubai,siku za karibuni na kuweka swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka kuichunguza jamii na kurushwa vipande vyake katika YouTube ambapo mpaka kufikia jana usiku watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000 .
Jarvis aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa kilichowasangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni euro za kutosha na fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa.
Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika barabra ya Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye tukafikiri sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni matajiri.
Basi utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali ambapo palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa.
Jarvis anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza kukimbia nayo wa nako hakuna aliyethubutu kuichukua pochi hiyo.
Jarvis, alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi anaonekana kwenye video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha kuwa ni raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti wetu umegundua tofauti na wayasemayo.
Trollstation ina wanachama wapatao 230,000 na utafiti wao kutoka Falme za Kiarab unaelekezwa Ulaya, Marekani na hatimaye Afrika .
Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya Dubai tusubiri wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis .

Mavazi ya mhubiri yawaacha vinywa wazi..


Mhubiri mmoja nchini Iran amewaacha watu vinywa wazi kwa kuvalia vazi la rangi ya manjano.
Hoseyn Khademian alionekana kwenye televisheni akivalia shati la manjano , viatu na hata saa ya rangi hiohio. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr.
Wahubiri nchini Iran, kwa kawaida huvalia mavazi meupe na joho la rangi isiyong'aa sana huku viatu vyao vikiwa vyeusi au vya hudhurungi.
Lakini mavazi ya Khademian yalikejeliwa na kufanyiwa gumzo sana kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati baadhi ya watu kwenye Facebook walimzomea wakisema anajitakia tu sifa, wengine walimfananisha na ndizi lilioivaa kupitiliza. ''
Msomaji mwengine alisema, '' angependeza zaidi ikiwa angevalia kilemba cha waridi,basi angependeza sana''.
Wakati mwonekano wake umegonga vichwa vya habari nchini Iran, bwana Khademian anasema yeye haoni kwa nini watu wanamsema sana kwani sio mara yake ya kwanza kuvalia mavazi ya manjano.
Mara ya mwisho alionekana kwenye TV akiwa amevalia mavazi ya waridi, anahoji ''kwa nini watu hawakunisema sana wakati huo,''ikilinganishwa na sasa rangi ya mavazi yangi sio kitu kipya,'' alisema Bwana Khademian. Rangi ya manjano ni rangi ya kawaida kama rangi nyinginezo''.

Viatu vinavyojifunga kamba vyenyewe...


Ni miaka 26 tangu tuone viatu vikijifunga kamba zenyewe kama ilivyokuwa kwenye matangazo ya biashara ya viatu vya Nike vyake Marty McFly vikijifunga miaka hio. hio
Hilo lilikuwa tu tangazo la bishara zamani sana lakini kuna mtu ambaye aliwaza hivyo miaka hiyo na kusema atakuja kuzindua viatu vyenye uwezo wa kujifunga kamba. Na kwake ndoto hio imetimia.
Wahandisi nchini Ujerumani wamebuni viatu ambavyo vina uwezo wa kujifunga kamba.
Walifanikiwa kufanya hivyo kwa kuweka 'cherger'mfano kama ile ya simu kwenye viatu hivyo ambavyo vinatumia kawi kujionea wenyewe itakavyokuwa kwenye miguu tofauti.
Pindi unapovaa kiatu hicho, sensa ya kiatu inakiambia kwamba mguu uko sawasawa na kuchochea kawi kwenye kiatu kile kuamrisha kamba kujifunga zenyewe.
Wakati unataka kuvua viatu utahitajika kubonyeza au kugonga wayo wa kiatu kile mara mbili na vile vile kuna miale inayoamrisha kamba za viatu vile kujifungua kwa kuzilegeza kamba.
Wanasema kiatu hicho hakihitaji kuwekwa kwenye charger au kubadilisha betri kwa sababu kawi inatokana na hatua za kuukanyaga mguu chini kwa mvaaji au anapotembea zile hatua ndizo zinakipatia kiatu nguvu au kawi.
Mmoja wa wahandisi waliokitengeza kiatu hicho, anasema kwamba kiatu hicho kitawasaidia watu wengi.
Miongoni mwa watakaofaidi ni watu wanaokumbwa na ulemavu wa miguu au wenye matatizo ya kutembea lakini pia vinaweza kuwasaidia watoto au kwa wanaotaka tu kubadili mfumo wao wa maisha.
Saa moja ya kutumia viatu hivyo inatosha kuweza kurejesha kawi ya kufunga kamba.
Bwana Ylli na kikundi cha wahandiisi wengine wanashughulikia kifaa kingine ambacho kitawezesha viatu kumuonyesha mvaaji mwelekeo anakokwenda.

Boko Haram ishughulikiwe kimataifa.


Rais wa Ghana, John Mahama, ameiambia BBC kwamba msaada wa kimataifa unahitajika kuweza kulishinda kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, nchini Nigeria.
Rais Mahama alisema nchi moja pekee haiwezi kuwashinda wapiganaji hao na kwamba ugaidi kila pahala ni tishio la dunia nzima.
Rais wa Ghana alisema viongozi wa nchi za Afrika Magharibi watakutana juma lijalo kuomba idhini ya Umoja wa Afrika kuunda kikosi cha kimataifa ili kupambana na Boko Haram, lakini aliongeza kusema kuwa kutuma kikosi hicho kunaweza kuchukua miezi.
Wanajeshi wa Chad wameanza kujongea Cameroon, kama sehemu ya ushirikiano zaidi wa kanda hiyo dhidi ya Boko Haram.

Charlie Hebdo:Makanisa yachomwa Niger

Ripoti kutoka Niger zinasema kuwa makanisa matatu yamechomwa katika mji mkuu wa Niamey katika siku ya pili ya maandamano dhidi ya uchapishaji wa vibonzo vya mtume Mohammed uliofanywa na gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Baadhi ya biashara zimeripotiwa kushambuliwa kama vile vibanda vya kampuni ya simu ya Orange.
Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake wanaoishi mjini Niamey kusalia majumbani mwao

Polisi wa kukabiliana na ghasia kwa sasa wameweka ulinzi mkali katika kanisa la Cathedral mjini humo ambapo makundi ya vijana wanaowarushia mawe.
Siku ya ijumaa watu wanne walifariki huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya waandamanaji kuyapekua makanisa matatu kabla ya kuyachoma mbali na kukichoma kituo kimoja kilicho na utamaduni wa Ufaransa huko Zinder.