Menu - Pages

Monday, 26 January 2015

ANGALIA BIBI WA MIAKA 90 ANASOMA DARASA LA NNE.


Gogo akiwa darasani na wanafunzi wenziwe.

Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi duniani.
Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla alijiunga na shule hii ya Leaders Vision Preparatory School miaka mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na mitano iliyopita.
Darasani Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua kujiunga na shule katika umri wake.
Sababu kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao wana watoto.
Gogo apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende shuleni.

Kwa nini waafrika wanajibadilisha rangi?.



Katika mfululizo wa Barua kutoka kwa Waandishi wa habari wa Afrika, Mwandishi na Mtunzi wa Riwaya,Tricia Nwaubani anaangazia mada ya kung'arisha Ngozi.
Kwa kipindi cha miaka michache iliyopita, nilijenga tabia ya kuwauliza waafrika wenzangu kutoka nchi tofauti tofauti wanafikiria bara letu lingekuwaje kama wafanya biashara ya utumwa na Wakoloni wasingeingia Afrika.
Baadhi wanaona kuwa jamii za kiafrika zingekuwa na maendeleo, ikienda sambamba na maendeleo ya dunia.
Wengine wanaona kuwa Afrika ilikuwa na maendeleo sawa na maendeleo ya dunia nzima, lakini utumwa na ukoloni viliingilia kati na kukwamisha maendeleo.
Wengine wanaamini kuwa sisi waafrika tungeuana kwa mapigano ya kikabila na migogoro, bara lingekuwa na makundi machache ya kikabila yaliyo mbali mbali.
Ninapenda kufikiria kuwa sisi waafrika tungeweza kujisimamia kwa mambo mengi.Tungegundua umeme ,tungetengeneza viyoyozi na majokofu, tungejiuliza ni vitu gani vinaonekana kwenye bahari, kisha tukkatuma wanaume kwa wanawake kufanya uchunguzi.

Ingeweza kuchukua miongo mingi, hata karne, lakini jamii za kiafrika zingeweza kupata hadhi ya kuwa moja ya bara la ulimwengu wa kwanza.
Pia nafikiri kuwa, kwa kiasi fulani ,mwafrika alipaswa kufikiria''Nywele zangu zimejinyonga nyonga na zimependeza.lakini swali ni je zingekuwaje kama zingenyooshwa.
''ingekuwaje kama nywele zangu zingekuwa za bluua au nyeusi kama za gold?''
Mwafrika wa namna hii angetengeneza dawa za nywele na rangi ya nywele, ingawa haonekani na nywele ndefu.
Kusingekuwa na kasumba ya kutaka kufanana na Watu weupe.

Waafrika wangeweza kuangalia uwezekano wa kubadili rangi za ngozi.
''baadhi yetu rangi zetu za ngozi ni nyeusi na nzuri,wengine ngozi ni angavu nao pia ni wazuri.je itakuwaje mwenye rangi nyeusi akataka awe mweupe na mweupe kuwa mweusi?''
'weusi ung'aao'
Wanawake wengi wa Nigeria ninaowafahamu wanaotumia vipodozi vya kung'arisha ngozi si kwamba ngozi zao za asili ni weusi.
Na kuna wanawake wenye ngozi nyeupe lakini wanataka kuongezea zaidi ya rangi waliyonayo.
Kumekuwa na kasumba kuwa kuwa na ngozi nyeupe kumeonekana kuwa kwa kipekee zaidi kwenye jamii ya watu wengi walio na ngozi nyeusi.

Alikaidi wazazi lakini sasa anajuta.


Je unakumbuka kisa cha wapenzi wawili waliozua gumzo nchini Kenya?
Msichana mhindi Sarika Patel kutoka familia tajiri na Timothy Khamala mbukusu kutoka familia maskini kutoka Magharibi mwa Kenya kuoana? wakati yao mapenzi yao yalijulikana kama Bukusu Darling, sifa kwa wanakoishi wawili hao.
Taarifa sasa ni kwamba mapenzi yao yamefika kikomo. Familia ya msichana Sarika ililaani sana mapenzi hayo kwani Timothy alikuwa anafanya kazi kwao kama mfanyakazi wa nyumbani.
Na Sarika alipoamua kwenda kuishi na Timothy kama mume na mke familia yake ilimfukuza na kisha kumfuta kazi Timothy.
Wawili hao walioana kinyume na matakwa ya familia ya Sarika ambayo kwao ilikuwa ni kama aibu kubwa sana kwa mtoto wao kutoka familia tajiri kuolea na kijana asiyekuwa na mbele wala nyuma.
Wakati taarifa ya wawili hao ilipogonga vichwa vya habari nchini Kenya, Sarika na mume wake walipata kazi katika kiwanda cha kutengeza Sukari kutoka kwa wahisani.
Lakini sasa kuna madai kwamba ndoa yao imevunjika baada ya Sarika kulalamika kwamba Timothy amekuwa akimdhulumu na kumtusi kila mara hali iliyosababisha wawili hao kutalakiana.
Mtandao wa Standard Digital umemnukuu Sarika akisema: "nilipokuwa mgonjwa , hakuwa hata na muda wa kunipeleka hospitalini badala yake wazazi wake ndio walionipeleka kutafuta matibabu. Mbali na hayo amekuwa akinichapa, '' alisema Sarika huku akibubujikwa na machozi.
Kwa sasa inaarifiwa anajuta sana kwa nini alikaidi amri ya wazazi wake.
''Ninajuta sana kwa nini sikuwasikiliza wazazi wangu na kuolewa kinyume na mapenzi yao. Ninaomba radhi, natumai watanikubali kurejea nyumbani. ''
Sarika ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano, ameamua kurejea nyumbani na kusema kamwe hatawahi kuwa na uhusiano wa kimepenzi tena. Lakini wazazi wake wamempa masharti, mwanzo aishi na rafiki yake huku akifanya uamuzi wa mwisho kuhusu anakotaka kuishi.
Anasema anahofia kwamba jamii ya wahindi haitamkubali tena kwani hakuwasikiliza wakati walipomshauri kutoolewa na mwanamume mwafrika.

Unywele wa Lincoln wauzwa dola 25,000.


Vitu vya kumbukumbu vya aliyekuwa rais wa 16 wa Marekani Abraham Lincoln vimeuzwa katika mnada mjini Dallas nchini Marekani na kupata dola 800,000.
Msokoto mmoja wa nywele za rais huyo aliyeuawa umeuzwa kwa dola 25,000 lakini barua iliokiri kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe havikuwa vizuri haikuuzwa.
Barua iliotiwa sahihi na naibu wake John Wlkes Booth iliuzwa kwa dola 30,000 huku agizo lake la kijeshi likitia kibindoni dola 21,250.





















Vitu vya Lincoln vilipigwa mnada mjini Dallas marekani.

ukusanyaji wa vitu hivyo 300 ulianzishwa mwaka 1963 na mmiliki wa jumba la sanaa Donald Dow aliyefariki miaka mitano iliopita.
Mwanawe Greg amesema kuwa ni wakati wakusanyaji wengine wapate fursa ya kuifurahia.
Amesema kuwa babaake alikuwa ameanza ukusanyaji huo kutokana na maslahi yake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na historia ya kijeshi,lakini baadaye alikuwa na hamu na Lincoln na mauaji yake.

Asilimia moja ya watu m.atajiri duniani

Aliko Dangote tajiri mkubwa barani Afrika.

Huku wafanyibiashara na wanasiasa wa ngazi za juu wakikutana katika mkutano wa kiuchumi duniani mjini Davos wiki hii ,hisia tofauti zimetolewa kuhusiana na kuwepo kwa ukosefu wa usawa duniani bila kuisahau asilimia moja ya watu Matajiri duniani.
Matajiri hao wanaishi katika visiwa vya kibinafsi,lakini je, hao ndio matajiri wanaojulikana Pekee?.
Ripoti moja ya shirika la wahisani la Oxfam iliotolewa sanjari na mkutano huo wa Davos,ilizua hisia kali baada ya kubashiri kwamba asilimia moja ya matajiri duniani huenda ikamiliki idadi yote ya watu duniani.
Ilitoa utafiti wake kutoka kwa benki ya Credit nchini Uswizi ambayo inakadiria jumla ya utajiri katika kila nyumba kuwa dola trillioni 263.
Huo ni itajiri na wala si mapato.
Watu matajiri kama vile Bill gates ,Warren Buffet na Mark Zuckerberg ni miongoni mwa asilimia 1.
Bill Gates na Warren Buffet.
Lakini je, ni nani mwengine aliyeorodheshwa katika asilimia hiyo?.
Kulingana na ripoti hiyo ya benki ya Credit watu wengine millioni 47 wana utajiri wa dola 798,000 kila mmoja.
Hiyo inashirikisha watu wengi katika mataifa tajiri ambao pengine wasingejitambulisha kama matajiri,lakini ambao wanamiliki nyumba ama wamelipa kiwango kikubwa cha mkopo.
Miongoni mwao ni:
Watu millioini 18 wanatoka Marekani
Millioni 4 inatoka Japan
Watu millioni 3.5 wanatoka Ufaransa
Watu millioni 2.9 wanatoka Uingereza
Millioni 2.8 wanatoka Ujerumani
Millioni 4 inatoka Japan
Na millioni 1.6 inatoka China

Tumesambaratisha IS,.Wakurdi

Serikali ya Kurdi imesema tayari imekwisha sambaratisha kikundi cha wapiganaji wa Islamic State katika mapigano yaliyodumu kwa takriban miezi minne.
Wapiganaji wa kundi la Islamic State walikuwa wakishikilia eneo la Kaskazini mwa Syria Kobane.
Wakrud katika eneo la jubilant wameanza kusherehekea kutokana na ushindi huo wa kuwaondoa wapiganaji wa IS.
Hata hivyo kumekuwa na maoni wapiganaji wa Kikurdi bado hawana udhibiti wa eneo la Mashariki. Wachambuzi wanasema kuwa kama mji wa Kobane umechukuliwa na majeshi ya Kurdi basi hiyo ni hatua mhimu katika kudhoofisha nguvu ya Islamic state.

Kasisi wa kwanza mwanamke aapishwa UK.

Kanisa moja nchini Uingereza hii leo limemuapisha mwanamke wa kwanza kuwa kasisi.
Mchungaji Libby Lane kama anavyojulikana sasa atakuwa kasisi wa Stockport katika sherehe iliofanyika katika eneo la York Minster,ikiwa ni miezi sita tu baada ya kanisa hilo kumpigia kura ili kumaliza utamaduni wake wa wanaume kuwa makasisi.
Kasisi huyo amesema kuwa iwapo uchaguzi wake utawafanya wanawake kubaini uwezo wao basi anafurahia.
Hatua hiyo imeendelea kuzua hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wa kanisa hilo la kianglikana duniani.

Ongwen afikishwa katika mahakama ya ICC.

Kiongozi mmoja wa kundi la waasi nchini Uganda, Dominic Ongwen, amekuwa mwanachama wa kwanza wa kundi la Lord's Resistance Army LRA, kufika mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake huko The Hague, Bwana Ongwen alithibitisha kuwa ndiye, huku akijieleza kuwa ni mwanajeshi wa zamani wa LRA.


Anakabiliwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na makosa mengine ya kivita, ikiwemo mauwaji na utumwa.
Awali mwezi huu alikuwa amezuiliwa nchini Afrika ya kati, miaka kumi tangu ICC ilipotoa ilani ya kumkamata.