Menu - Pages
▼
Saturday, 14 February 2015
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE.....
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini Dk.Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini dar leo.
Shule za sekondari za binafsi zinaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Akizungumza na waandish wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es salaam, katibu mtendaji wa Baraza la mitihani nchini (NECTA)
, Dk. Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka kwa 12.67% ikilinganishwa na mwaka 2013.
katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab, Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufuatia wavulana.
Shule za sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi
wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.
Msonde anasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mpya wa GPA kwa kuangalia masomo saba hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.
Amkodishia mkewe mume wa 'kumhudumia'...
Mtu mmoja katika mahakama ya Kwale nchini Kenya ameshtakiwa kwa kumkata pua na mkono mkewe ambaye anamshuku kwa kufanya uasherati.
Kulingana na gazeti la the Nairobian nchini Kenya,Chirope Mwaruwa anadaiwa kumkodisha mwanamume ili kulala na mkewe mjamzito akidai kwamba ana matatizo.
Alishtakiwa kwa kumshambulia mkewe Sada Dzea katika kijiji cha Mukundi taarafa ya Mangawani ,kaunti ya Kwale.
Kulingana na upande wa mashtaka Dzea mara ya kwanza alimkataa mtu aliyekodishwa na mumewe wafanye naye tendo la ngono akiwa mjamzito.
Baada ya Dzea kukataa mumuwe alianza kumshtumu kwa kufanya uzinzi huku akitaka kumvua nguo kwa lengo la kutafuta ushahidi.
Na alipokasirishwa na shtuma hizo Dzea alidaiwa kumtembelea mtu huyo aliyekodishwa na mumewe ili afanye naye tendo la ngono kwa lengo la kumfurahisha mumewe.
lakini kabla ya yeye kufika kwa mawanmume huyo mumewe mwenye wivu mwingi alidaiwa kumvamia na kuanza kumshambulia.
Zuma: hakuna ruhusa mgeni kumiliki ardhi...
Wageni hawatoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini, kufuatana na sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma.
Siku zijazo wageni wataruhusiwa tu kukodi kwa muda mrefu ardhi ya mashamba ya Afrika Kusini.
Mbali ya hayo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000 atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kugawiwa.
Ardhi bado ni swala linalozusha hamasa nchini humo - ambako karne tatu za ukoloni na ubaguzi wa rangi - zimeacha ardhi nyingi mikononi mwa wachache, hasa wazungu.
Tangu kumalizika ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa thuluthi ya ardhi ya kilimo kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014.
Boko Haram waondoka Gombe....
Wapiganaji Waislamu wa Boko Haram wametoka katika mji wa Gombe kaskazini-mashariki mwa Nigeria baada ya mapambano makali na jeshi.
Wakuu wanasema wapiganaji wamerejeshwa nyuma, lakini ripoti nyengine zinasema kuwa wapiganaji hao waliondoka kwa hiari yao.
Boko Haram waliingia Jumamosi asubuhi katika vitongoje vya Gombe baada ya kushambulia mji jirani wa Dadin Kowa.
Wapiganaji hao wamewahi kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga katika mji wa Gombe, lakini hawakupata kujaribu kuuteka mji wenyewe.
Nigeria ikitarajiwa kufanya uchaguzi tarehe 14 Februari, lakini umeakhirishwa kwa majuma sita kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama.