Menu - Pages
▼
Sunday, 12 April 2015
Mufti asema unaweza 'kumla' mkeo Saudia..
'Ni sawa kumla mkeo unapohisi njaa nchini Saudi Arabia lakini tu iwapo unahisi njaa kali'.
Mufti-kiongozi wa dini ya kiislamu aliye na uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu maswala ya kidini-ametoa idhini ya ulaji wa mtu.
Kulingana na gazeti la Metro nchini Uingereza na mtandao wa Alalam nchini Saudia Abdul Azizi bin Abdullah alishtumiwa kufuatia tamko lake kulingana na mitandao mingi ya kiarabu.
Mtandao wa A Tayyar uliripoti:Mufti mmoja wa Saudi Arabia alitoa agizo ambalo linamruhusu mwanamume aliye katika ndoa kumla mkewe iwapo anahisi njaa kali.
Mufti huyo amesema kuwa hatua hiyo inaonyesha vile mwanamke anafaa kumheshimu mumewe.
Lakini mamlaka ya kidini yamekana kwamba kiongozi huyo alitoa matamshi kama hayo.
Wakimbizi wa Somalia:Kenya yaonya UN..
Serikali ya Kenya imeupatia Umoja wa Mataifa makataa ya miezi mitatu kuwahamisha wakimbizi wa Somalia wapatao nusu milioni hadi nchini Somalia.
Naibu rais William Ruto amesema kuwa iwapo Umoja wa mataifa utakataa kuwahamisha wakimbizi hao, Kenya itachukua jukumu la kuwandoa.
Makataa hayo yanajiri siku kadhaa baada ya shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 148 waliuawa na kundi la wapiganaji wa Al-shaabab.
Baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakiishi katika kambi za Dadaab mashariki ya taifa hilo kwa zaidi ya miongo miwili.
Kenya imelishtumu kundi la Alshabaab kwa kujificha katika kambi hizo huku likiwasajili wanachama wapya.
Obama na Castro wafanya mkutano.
Viongozi wa marekani na Cuba wamefanya mkutano wao wa kwanza tangu zaidi ya nusu karne iliyopita.
Rais Obama na mwenzake wa Cuba Raul Castro walikutana ana kwa ana pembezoni mwa mkutano wa nchi za Amerika nchini Panama.
Mkutano huo utatoa mwelekeo wa kuboresha uhusiano baada ya miongo kadha ya uhasama kati ya Marekani na kisiwa hicho cha utawala wa kikoministi
Rais Obama alisema kuwa angependa kuona watu wa Cuba wakiendelea kuishi kwa uhuru na kwa usalama. Naye Castro kwa upande wake alisema kuwa Cuba ilikuwa tarayi kujenga urafiki na marekni lakini akaongeza kuwa nchi hizo mbili zina tofauti nyingi na historia iliyokumbwa na utata.
Hillary Clinton kuwania urais Marekani..
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Hillary Clinton atakuwa rais bora na mwenye maono kwa nchi ya Marekani. Bi Clinton anatarajiwa kutangaza hii leo kuwa atawania uteuzi wa chama cha Democratic.
Obama amesema kuwa Bi Clinton alitekeleza kwa njia nzuri majukumu yake alipohudumu kama waziri wa mashauri ya kigeni. Atatangaza azma yake ya kuwania urais kwa njia ya video ambayo itasambazwa kupitia kwa mitandao ya kijamii.
Kinyume na miaka minane iliyopita Bi Clinton anatarajiwa kuangazia zaidi jinsi wapiga kura wataandikisha historia kwa kumchagua kuwa mwanamke wa kwanza rais wa Marekani.
Islamic State waharibu mji wa Nimrod...
Wanamgambo wa Islamic State wametoa kanda ya video kupitia kwa mtandao ikiwaonyesha wakiharibu maeneo ya thamani kubwa kwenye mji wa Nimrod nchini Iraq.
Picha za wanamgambo hao wakitumia misumeno ya umeme kukata sanamu, zinaonekana kuthibitisha ripoti za mwezi uliopita kutoka kwa maafisa nchini Iraq kuwa wanamgambo hao wameharibu mji wa kitamadanu wa Nimrod.
Wanamgambo hao hutumia tinga tinga na milipuko kuharibu mji huo ambao wakati mmoja ulikuwa ni mji mkuu wa himaya ya Assyrian.