Menu - Pages

Saturday, 29 August 2015

Waandishi wa Al Jazeera miaka 3 Jela


Mahakama nchini Misri imewahukumu waandishi watatu wa kituo cha runinga cha Al jazeera miaka mitatu jela.
Wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, Mohamed Fahmy, Peter Greste na Baher Mohamed walipatikana na hatia ya kutangaza habari za uongo na kulisaidia kundi la Muslim Brotherhood ambalo kwa sasa linatambuliwa kuwa kundi la kigaidi.
Baher Mohamed pia alihukumiwa kifungo kingine cha miezi sita.
Hata hivyo Peter Greste, yuko nje ya nchi baada ya kutimuliwa kutoka nchini humo mwezi Ferbruari.

Mkutano wa usalama kufanyika Ufaransa


Mawaziri wa masuala ya ndani wa nchi za ulaya wakutana mmji Paris hii leo kujadili njia za kuboresha usalama kwenye usafiri wa reli baada ya shambulizi lililotibuka wiki iliyopita kwenye treni iliyokuwa safarini kutoka Amsterdam kwenda Paris.
Ufaransa inataka kutangaza hatua kali za usalama ikiwemo vifaa vya kutambua chuma kwenye treni za kimataifa, kuweka wahudumu waliojihami na mifumo ya mawasiliano iliyoboreka kufuatilia mienendo ya wanamgambo walioshukiwa.

Raia wa Morocco ambaye alikuwa amejihami vikali (Ayub al-Khazani) ambaye alishindwa nguvu na abiria baada kupanda treni mjini Brussels alikuwa akifanya safari kote barani Ulaya hata baada uhispania kutoa onyo kuwa huenda mtu huyo alikuwa ni gaidi.

Ban aitaka ulaya kuwasaidia wahamiaji


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa serikali zote zinazolishughulikia suala la wakimbizi barani ulaya kutenga maeneo salama kwa wahamiaji na kuonyesha utu.
Ban amesema kuwa idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji ni ishara ya matatizo makubwa kama ya vita vilivyo nchini Syria ambapo ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuonyesha moyo wa kutatua mizozo kama hiyo.

Ban amesema kuwa masuala hayo yatapewa kipaumbele wakati viongozi wa dunia watapokusanyika kwenye mkutano wa umoja wa mataifa mwezi ujao.
Mapema umoja wa mataifa uliwataka viongozi wa nchi za ulaya kuzuia vifo vya wahamiaji baada ya mamia kuaga dunia siku tatu zilizopita.

Mafuriko yaua 20 Dominica


Waziri mkuu nchini Dominica anasema kuwa watu 20 wanariporitiwa kuaga dunia kwenye mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Erika.
Kwa njia ya televisheni Roosevelt Skerrit alisema kuwa mamia ya nyumba, madaraja na barabara vimeharibiwa na kisiwa hicho kumerudishwa nyuma miaka ishirini.
Kimbunga kwa sasa kinazikumba Haiti na Jamhuri ya Dominica kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya karibu kilomita 85 kwa saa.
Watabiti wa hali hewa wanaseme kuwa hata hivyo kinaonyesha dalili za kupoteza nguvu zake.

Yaliomo kwenye makubaliano ya S.kusini


Hivi ndio vipengee vikuu kwenye makubaliano ya amani ambayo rais wa Sudan kusini Salva Kiir anatarajiwa kusiani Juba:
Mapigano yasite mara moja. Wanajeshi wasalie kweny kambi zao kwa siku 30, vikosi vya nje viondoke katika siku 45 na watoto wanaotumiwa jeshini na wafungwa wa vita waachiliwe huru.
Vikosi vyote vya usalama vitoke umbali wa kilomita 25 kutoka Juba, nabadala yake vikosi maalum na polisi ya pomoja vichukuwe nafasi hiyo.
Waasi wapewe cheo cha "makamu wa kwanza wa rais"
Serikali ya mpito ya muungano wa kitaifa iidhinishwe katika muda wa siku 90 na iongoze nchi kwa miezi 30.
Uchaguzi ufanyike siku 60 kablaya ya kumalizika kipindi cha mpito.
Serikali ipate uwingiwa nyadhifa serikalini katika kiwango cha kitaifa na katika majimbo 7 kati ya 10 yaliopo.
Katika majimbo yanayokumbwa na vita - Jonglei, Unity, na Upper Nile - waasi wanapata uwakilishi ulio sawana serikali.
Tume ya ukweli na mapatano ichunguze ukiukaji wa haki za binaadamu.

Kidimbwi kinachounganisha majumba 2 UK


Kidimbwi cha kuogelea chenye urefu wa mita 25 kinachounganisha kilele cha majumba mawili marefu yenye ghorofa 10 kitajengwa mjini London.
Kidimbwi hicho kinachoitwa ''Sky Pool'' ni cha kwanza duniani na kitakuwa na eneo la chini lililo wazi.Uwazi huo utawasaidia waogoleaji kuwaona raia wanaotembea chini ya majumba hayo kwa urefu wa mita 35.
Kampuni ya Eckersley O'Callaghan ambayo imeshirikiana na ile ya Apple kuhusu mtindo wa kidimbwi hicho cha kuogelea itatengeza mradi huo.
Kidimbwi hicho ni miongoni mwa miradi ya ujenzi ya maeneo ya kujivinjari kwa jina Embassy Gardens at Nine Elms,karibu na kituo cha umeme cha Battersea

Inatarajiwa kuwa mradi huo utakamilika ifikiapo mwaka 2019,lakini mtindo huo una changamoto zake hususan kutokana na hatua kwamba kidimbwi hicho kitazuiliwa na misukumo itakayotoka kutoka kuta za majumba hayo mawili ambayo yamejengwa na misingi tofauti.
''Upepo unapovuma majumba hayo huyumba tofauti na hivyobasi kuwa changamoto kwa watengezaji wa kidimbwi hicho'' kulingana na Brian Eckersley

Treni iliyosheheni dhahabu yapatikana


Afisa mmoja wa serikali ya Poland, amesema kuwa ana imani kuwa treni moja ya kijeshi ambayo imefichwa tangu vita vya pili vya dunia, zaidi ya miaka sababini iliyopita, na kusemekana kubeba vitu vya dhamani, imepatikana, chini ya ardhi Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.
Naibu waziri wa utamaduni amesema shehena iliyoko kwenye treni hiyo bado haijulikani.
Kwa mujibu wa ripoti treni hiyo ilipotea ikiwa imejaa shehena ya dhahabu kutoka mji wa Breslau nchini Ujerumani, mji ambao kwa sasa unajulikana kama Wroclaw and sehemu zingine za Poland, wakati wanajeshi wa Ujerumani walipokaribi mji huo.
Afisa mkuu wa makavazi ya kitaifa, Piotr Zuchowski, amesema anaimani kuwa treni hiyo itapatikana chini ya ardi karibu na mji wa Walbrzych.
Amesema ameona picha zilizopigwa na kifaa maalum chini ya ardhi ikionyesga treni hiyo yenye urefu wa karibu mita mia moja ikiwa na bunduki juu yake.
Amesema hamna anayefahamu kile treni hiyo ilikuwa imebeba wakati huo na asema anatarajia iwe na vitu vya Sanaa vilivyoibiwa nchini Ujerumani wakati wa utawala wa Kinazi.
Raia wawili ambao hawajatambuliwa kutoka Ujerumani na Poland waliifahamisha utawala wa eneo hilo kuwa wanafahamu eneo lililofichwa treni hiyo, na wamedai wapewe asilimia kumi ya vitu vitakavyopatikana ndani yake.
Watu hao wanasema kuwa walipewa habari hizo na mtu mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa walioficha treni hiyo, muda mfupi tu kabla ya mtu huyo kufariki.