Daktari Salia alikuwa anafanya kazi nchini Sierra Leone na haijulikani ikiwa aliwatibu wagonjwa wa Ebola
Daktari mmoja kutoka nchini Sierra Leone aliyekuwa anapokea
matibabu ya Ebola nchini Marekani amefariki. Taarifa hii ni kwa
mujibu wa hospitali ya Nebraska nchini humo. Daktari, Martin Salia mwenye umri wa miaka 44 na ambae ana uraia
wa Marekani kutokana na ndoa yake kwa mwanamke mmarekani, aliwasili
nchini humo kwa matibabu mnamo siku ya Jumamosi. Lakini Jumatatu asubuhi, hospitali ya Nebraska ilitangaza kuwa
daktari huyo alifariki akipokea matibabu. Yeye ni mtu wa pili
kufariki kutokana na Ebola nchini Marekani. Zaidi ya watu 5,000 wamefariki kutokana nba Ebola, tangu mlipuko
wa ugonjwa huo kuripotiwa, wengi wao wakiwa katika mataifa ya Afrika
Magharibi.
Eric Duncan raia wa Liberia alifariki kutokana na Eboka wakati
akipokea matibabu nchini Marekani mwezi jana. Alikuwa amekwenda
Marekani kuwatembelea jamaa wake. "tunasikitika sana kutangaza kuwa mgonjwa wa pili ambaye
alikuwa anapokea matibabu ya Ebola, Dr Martin Salia, amefariki
kutokana na ugonjwa huo kuwa katika hali iliyokuwa sugu kwa
matiibabu,'' ilisema taarifa ya hopistali hiyo.
Wahudumu wa afya, walimsafirisha Dr Salia katika kituo cha afya
cha Nebraska akiwa katika hali mbaya sana. Mkewe Salia alisema
anashukuru kwa juhudi zilizofanywa kumtibu mumewe.
Alikuwa amefanya kazi kama daktari wa upasuaji katika hospitali ya
Kissy United Methodist Hospital nchini Sierra Leone. Haijulikani
ikiwa alihusika na kuwatibu wagonjwa wa Ebola.







0 comments:
Post a Comment