Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu
za Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL
Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na
kisheria.
Katika ripoti hiyo
iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu
mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya
udanganyifu na ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na
kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na
uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya viongozi.Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.






0 comments:
Post a Comment