Televisheni ya NBC imesitisha mradi wa kurusha kipindi
cha mchekeshaji maarufu duniani, Bill Cosby baada ya kukabiliwa na
shutuma zaunyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake .
Katika taarifa hiyo, kampuni imethibitisha kusimamishwa
kwa kipindi hicho.
Siku ya jumanne kamouni inayotoa huduma ya vipindi vya
video kwa njia ya internet, Netflix iliahirisha kipindi kilichomuhusu
Cosby baada ya mwanamitindo mmoja kudai kuwa alidhalilishwa kijinsia
mwaka 1982.
Mtandao wa Netflix ulikataa kutoa sababu ya kusitisha
uzalishaji wa kipindi, lakini umesema kuwa maandalizi ya uzalishaji
ulikua haujaanza. Cosby amekana kuhusika na vitendo hivyo.
Hatua hii imekuja baada ya mwanamitindo na mtangazaji
kipindi cha Televisheni Janice Dickinson kusema kuwa alidhalilishwa
na Cosby walipokutana kwa ajili ya chakula cha usiku huko California
mwaka 1982.
Janice amesema aliandika katika kitabu kinachohusu
maisha yake kuhusu tukio hilo lakini alipata shinikizo kutoka kwa
Mwanasheria wa Cosby na mchapaji wa kitabu chake kuondoa sehemu hiyo.
Mwanasheria wa Cosby Martin Singer amesema madai ya
Dickinson ni ya uongo na hayana msingi.
Dickinson ni miongoni mwa wanawake kadhaa waliomshutumu
kuwadhalilisha kijinsia miaka takriban 30 iliyopita.
Nae muigizaji wa zamani Barbara Bowman amesema
alidhalilishwa na Cosby katika nyakati tofauti mwaka 1985 alipokuwa
na umri wa miaka 17.
Mwanzoni mwa mwezi huu Barbara alisema alishindwa
kupeleka mashitaka polisi kwa kuwa alihofu hataaminika.
Cosby hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la kihalifu.
No comments:
Post a Comment