Menu - Pages

Monday, 17 November 2014

Ebola yamuua daktari Marekani........BBC

 Daktari Salia alikuwa anafanya kazi nchini Sierra Leone na haijulikani ikiwa aliwatibu wagonjwa wa Ebola

 Daktari mmoja kutoka nchini Sierra Leone aliyekuwa anapokea matibabu ya Ebola nchini Marekani amefariki. Taarifa hii ni kwa mujibu wa hospitali ya Nebraska nchini humo. Daktari, Martin Salia mwenye umri wa miaka 44 na ambae ana uraia wa Marekani kutokana na ndoa yake kwa mwanamke mmarekani, aliwasili nchini humo kwa matibabu mnamo siku ya Jumamosi. Lakini Jumatatu asubuhi, hospitali ya Nebraska ilitangaza kuwa daktari huyo alifariki akipokea matibabu. Yeye ni mtu wa pili kufariki kutokana na Ebola nchini Marekani. Zaidi ya watu 5,000 wamefariki kutokana nba Ebola, tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuripotiwa, wengi wao wakiwa katika mataifa ya Afrika Magharibi.

Eric Duncan raia wa Liberia alifariki kutokana na Eboka wakati akipokea matibabu nchini Marekani mwezi jana. Alikuwa amekwenda Marekani kuwatembelea jamaa wake. "tunasikitika sana kutangaza kuwa mgonjwa wa pili ambaye alikuwa anapokea matibabu ya Ebola, Dr Martin Salia, amefariki kutokana na ugonjwa huo kuwa katika hali iliyokuwa sugu kwa matiibabu,'' ilisema taarifa ya hopistali hiyo.

Wahudumu wa afya, walimsafirisha Dr Salia katika kituo cha afya cha Nebraska akiwa katika hali mbaya sana. Mkewe Salia alisema anashukuru kwa juhudi zilizofanywa kumtibu mumewe.
Alikuwa amefanya kazi kama daktari wa upasuaji katika hospitali ya Kissy United Methodist Hospital nchini Sierra Leone. Haijulikani ikiwa alihusika na kuwatibu wagonjwa wa Ebola.

No comments:

Post a Comment