Polisi nchini Liberia wametangaza kuwa watafunga fuko
zote za bahari kuanzia tarehe 29 mwezi Novemba hadi pale taifa hilo
litakapo tangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umemalizwa..
Tarehe hiyo itakuwa ni siku ya taifa la Liberia ya
kuadhimisha kuzaliwa kwa raisi aliyeiongoza Liberia kwa miaka mingi
William Tubman.
Polisi wanasema kuwa yeyote atakayetumia fuo hizo za
bahari atakuwa amekiuka amri hiyo na atachukuliwa hatua za kisheria.
Polisi pia wamepiga marufuku mikutano yote ya umma
isipokuwa ya kisiasa.
Karibu watu 3000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment