Bunge
la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais
bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa
kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.
Bwana
Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika
barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo
kama ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu.
Kushirikishwa
kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu
kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa
iliopita.
Kiongozi
wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa
bunge upande wa upinzani bwana Tandu Lissu alifichua jukumu
lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba
baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa
mabilioni hayo ya fedha.
Ripoti
hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa
Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa
miongoni mwa watu maarufu.
No comments:
Post a Comment