Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda.
Mwili wa Rais wa Zambia, Michael Sata umewasili Zambia tayari kwa mazishi ambayo yamepangwa kufanyika November 11,2014
Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda kesho tarehe 10 Novemba, 2014 ataongoza ujumbe wa Bunge la SADC kushiriki Misa Maalum ya kuombea mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Chilufya Sata katika misa maalum itakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mjini Lusaka, Zambia.
Katika
ujumbe huo wa Bunge la SADC, Makinda ataongozana na viongozi wengine
wa Bunge hilo ambao ni Spika wa Zimbabwe Mhe. Jaji Jacob Mudenda,
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete, Spika wa Bunge la
Malawi Mhe. Richard Msowoya Spika wa Bunge la Angola Mhe. Fernando da
Piedade Dias dos Santos na Mwenyeji wao Spika wa Zambia Dkt. Patrick
Matibini.
Kutoka
secretariat ya makao makuu wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa Bunge Bunge
la SADC Dkt. Essau Chiviya ataambatana na ujumbe huo kuwakilisha
sekretariati ya Bunge hilo katika Misa hiyo Maalum Mjini Lusaka,
Zambia.
Kwa
mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Serikali ya Zambia, Misa
hiyo Maalum ya kuombea mwili wa Rais Rata itanyika kesho tarehe 10
Novemba, 2014 na inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka kila kona
ya dunia pamoja na viongozi mbalimbali wa Kimataifa
watakaoziwakilisha nchi zao kabla ya kufanyika kwa mazishi yake
ambayo yamepangwa kufanyika siku ya jumatatu tarehe 11 Novemba, 2014
mjini Lusaka.
Sata
aliyekuwa na umri wa miaka 77 alifariki tarehe 29 Oktoba, 2014 jijini
Londo Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo kifo chake
kilitokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru
wa nchi hiyo, sherehe ambazo hakuweza kushiriki kutokana na maradhi
yaliyokuwa yakimsumbua.
Mwanasiasa
huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya
kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda,
ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for
Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.
Sata
ambaye alibatizwa jina la "King Cobra" na wafuasi wake
wakati alipochaguliwa mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za
Zambia na mtu ambaye alikuwa wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu
kubwa na upinzania.
Makinda
na ujumbe wake wanatarajia kurudi nchi siku ya jumatano baada
kushiriki pia mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Novemba, 2014.
No comments:
Post a Comment