Wakili
wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na
kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini
Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.
Mapema
wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu
miongoni mwa waamerika weusi.
Afisa
huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo
yalisababisha majuma kadha ya maandamano.
Gazeti
la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28 aliamua
kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho kwamba
ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.
Gazeti
hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo
ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa
idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na
raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali
hata kidogo.
No comments:
Post a Comment