Menu - Pages
▼
Sunday, 9 November 2014
SHULE za msingi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa zimeongoza matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2014 kwa kushika namba moja hadi saba kati ya shule 10 bora kitaifa.
Jiji la Mwanza
Aidha,
watahiniwa wamefaulu zaidi somo la Kiswahili na kufeli zaidi somo la
Hisabati.
Katika
matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa
(NACTE), wavulana wameongoza somo la Hisabati kwa kupata alama 50/50,
ambapo 26 wamefaulu kwa kiwango hicho na wasichana wakiwa wanane.
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alizitaja
shule 10 bora kuwa ni Twibhoki ya Mara ambayo imeshika nafasi ya
kwanza, Mugini iliyoshika nafasi ya pili, Peace land na Alliance zote
za Mwanza, Kwema (Shinyanga), St. Severine (Kagera), Rocken Hill
(Shinyanga), Tusiime (Dar es Salaam), Imani (Kilimanjaro) na Palikas
(Shinyanga).
“Kwa
upande wa mikoa iliyofanya vizuri kitaifa na asilimia zake za ufaulu
kwenye mabano ni Dar es Salaam (46,434), Kilimanjaro (26,192), Mwanza
(37,017), Iringa (14,650), Arusha (23,250), Tanga (26,261), Njombe
(11,389), Kagera (24,501), Geita (17,560) na Mtwara (15,608).
“Wilaya
zilizoongoza kitaifa ni Mpanda Mji (Katavi), Biharamulo (Kagera),
Moshi (Kilimanjaro), Kibaha (Pwani), Arusha (Arusha), Kinondoni (Dar
es Salaam), Korogwe Vijijini (Tanga), Ilala (Dar es Salaam), Iringa
(Iringa) na Mji Makambako (Njombe),” alisema Dk. Msonde.
Akizungumzia
ufaulu wa kimasomo, alisema katika masomo yote umepanda kwa asilimia
kati ya 0.64 na 8.94 ikilinganishwa na mwaka jana.
“Watahiniwa
wamefaulu zaidi somo la Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 69.70
tofauti na asilimia 69.06 ya mwaka jana, na somo walilofaulu kwa
kiwango cha chini zaidi ni Hisabati lenye ufaulu wa asilimia 37.56
ambapo mwaka jana ilikuwa ni asilimia 28.62.
“Katika
somo la Kiingereza watahiniwa waliofaulu kwa mwaka huu ni asilimia
38.84 ikilinganishwa na mwaka jana asilimia 35.52 na Sayansi kwa
mwaka huu waliofaulu ni asilimia 54.89 na mwaka jana asilimia 47.49,”
alisema.
Dk.
Msonde alisema jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 waliofanya
mtihani huo wamepata alama 100 au zaidi katika alama 250 ambapo idadi
hiyo ni sawa na asilimia 56.99.
Alisema
kati ya watahiniwa hao, wasichana ni 226,483 ambao ni sawa na
asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909 sawa na asilimia 60.87.
Miongoni
mwa watahiniwa hao waliofaulu, Dk. Msonde alisema wamo wenye ulemavu
795 wakiwamo wasichana 355 ambao ni sawa na asilimia 44.65 na
wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35.
“Katika
mtihani huo uliofanyika Septemba 10 na 11, mwaka huu jumla ya
watahiniwa 808,085 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani
huo wakiwamo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana
378,461 sawa na asilimia 46.83.
“Kati
ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 691 walikuwa na uoni
hafifu, 87 walikuwa na ulemavu wa macho (wasioona), wenye matatizo ya
kusikia 374, wenye mtindio wa ubongo 252 na watahiniwa 27 walikuwa na
ulemavu zaidi ya mmoja,” alisema Dk. Msonde.
Pamoja
na mambo mengine, NECTA imemfutia matokeo mtahiniwa mmoja
aliyebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo. Mwaka jana
watahiniwa 13 walifutiwa matokeo yao kwa kufanya udanganyifu.
Hata
hivyo, Baraza hilo limesita kutoa matokeo ya shule zilizofanya vibaya
kwa madai ya kuendelea na uchambuzi wa kuzitambua zaidi.
MAKINDA KUONGOZA UJUMBE WA BUNGE LA SADC KUMZIKA RAIS SATA LUSAKA, ZAMBIA
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda.
Mwili wa Rais wa Zambia, Michael Sata umewasili Zambia tayari kwa mazishi ambayo yamepangwa kufanyika November 11,2014
Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda kesho tarehe 10 Novemba, 2014 ataongoza ujumbe wa Bunge la SADC kushiriki Misa Maalum ya kuombea mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Chilufya Sata katika misa maalum itakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mjini Lusaka, Zambia.
Katika
ujumbe huo wa Bunge la SADC, Makinda ataongozana na viongozi wengine
wa Bunge hilo ambao ni Spika wa Zimbabwe Mhe. Jaji Jacob Mudenda,
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete, Spika wa Bunge la
Malawi Mhe. Richard Msowoya Spika wa Bunge la Angola Mhe. Fernando da
Piedade Dias dos Santos na Mwenyeji wao Spika wa Zambia Dkt. Patrick
Matibini.
Kutoka
secretariat ya makao makuu wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa Bunge Bunge
la SADC Dkt. Essau Chiviya ataambatana na ujumbe huo kuwakilisha
sekretariati ya Bunge hilo katika Misa hiyo Maalum Mjini Lusaka,
Zambia.
Kwa
mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Serikali ya Zambia, Misa
hiyo Maalum ya kuombea mwili wa Rais Rata itanyika kesho tarehe 10
Novemba, 2014 na inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka kila kona
ya dunia pamoja na viongozi mbalimbali wa Kimataifa
watakaoziwakilisha nchi zao kabla ya kufanyika kwa mazishi yake
ambayo yamepangwa kufanyika siku ya jumatatu tarehe 11 Novemba, 2014
mjini Lusaka.
Sata
aliyekuwa na umri wa miaka 77 alifariki tarehe 29 Oktoba, 2014 jijini
Londo Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo kifo chake
kilitokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru
wa nchi hiyo, sherehe ambazo hakuweza kushiriki kutokana na maradhi
yaliyokuwa yakimsumbua.
Mwanasiasa
huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya
kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda,
ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for
Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.
Sata
ambaye alibatizwa jina la "King Cobra" na wafuasi wake
wakati alipochaguliwa mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za
Zambia na mtu ambaye alikuwa wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu
kubwa na upinzania.
Makinda
na ujumbe wake wanatarajia kurudi nchi siku ya jumatano baada
kushiriki pia mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Novemba, 2014.
HOTUBA YA SHIGONGO YAWAKUNA WAHITIMU MLIMANI SCHOOL OF PROFESSIONAL STUDIES
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Eric Shigongo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo akiongoza maandamo maalumu yaliyoandaliwa na chuo hicho, kushoto ni Mkuu wa Chuo, Hassan Ngoma.
Shigongo akihojiwa na mwandishi wa chuo hicho cha Professional FM, Shikunzi Haonga ambaye ni mkuu wa kitengo idara ya habari mawasiliano kwa umma (hayupo pichani) ndani ya studio iliyopo chuoni hapo.
Shigongo akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa studio hiyo ya chuoni hapo.
Msisimko huo ulikua pale Shigongo alipotoa simulizi ya
riwaya ya ombaomba mmoja aliyekuwa akiomba kila siku kwa
kutumia kopo, kumbe kopo lile ni dhahabu yenye thamani ya
mabilioni ya fedha kwenya mahafali ya pili katika chuo hicho.
Mmoja wa wahitumu ngazi ya diploma katika fani ya Habari
na Mawasiliani ya Umma, Neema Kisimbo alimpongeza Shigongo kuwa ni
kati ya Watanzania wachache waliopewa thawabu na Mungu hata
kama akifa leo atakuwa na la kusema kuhusu alivyoweza kuisaidi jamii.
“Baba
huyu ana kipaji lakini mbali na kipaji chake pia kujituma kwake
kumefanya awe na mafanikio makubwa maana maisha ni malengo, si
kweli kwamba ameenda kwa waganga,” alisema mhitimu huyo.
Katika mahafali hayo, Shigongo aliwatunuku vyetu
wahitimu 119 katika Chuo cha Mlimani School of Profession Studies
katika mahali yaliyofanyika katika chuo hicho hapo jana Mbezi Kwa
Msugur jijini Dar es Salaam.
Wahitumu hao walifunzu katika kozi tofauti ndani ya chuo
hicho ambapo kuna baadhi ya walipata ngazi ya cheti na wengine
katika ngazi ya diploma ambapo wote hao walitunukiwa vyeti
hivyo na mkurugenzi wa Global Publishars ambaye alikuwa
mgeni rasimi katika mahafali hayo.
Mkurugenzi huyo alitoa vyeti kwa wahitimu 19
katika ngazi ya cheti kwa fani ya Manunuzi na Ugavi, Fani ya Habari
na Mawasiliano ya Uma wahitimu ngazi ya cheti walikuwa 20,
Rasilimali Watu wahitimu 18, ngazi ya cheti wahitimu Uhasibu walikuwa
17 , Uongozi na Biashara ngazi ya cheti sita, Mauzo na Masoko ngazi
ya cheti 3, Rasilimali Watu ngazi ya diploma sita , Uongozi wa
Biashara diploma 10, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma
ngazi ya diploma10.
Wengine ni wa Mauzo na Masoko ngazi ya diploma mmoja,
Uhasibu ngazi ya diploma sita, Manunuzi na Ugavi ngazi ya diploma
wanne.
Mkuu wa chuo hicho, Hassan Ngoma alimtunuku Shigongo
cheti cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ngazi ya Diploma
kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari.
JK AFANYIWA UPASUAJI WA TEZI DUME
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. JakayaMrisho Kikwete akizungumza na Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya Johns Hopkins na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi(kulia) baada ya kuwasili katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyopo Baltimore, Maryland, Marekani kwa upasuaji Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
iliyopo Baltimore, Maryland, Marekani kwa upasuaji Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
MWAKIFWAMBA ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI MORO
RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba jana usiku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupata ajali na kupinduka eneo la Mkindu jirani na mizani mkoani Morogoro.
Mwakifwamba alipata ajali hiyo wakati akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki 'bodaboda' baada ya gari lake aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 176 CYM kupata pancha na kuanza kupoteza muelekeo. Katika gari hilo, Simon alikuwemo peke yake na alitoka salama salimini. Akiongea na tovoti hii kwa njia ya simu akiwa njiani kurudi Dar, Mwakifwamba alisema, "Ilikuwa majira ya saa 3 usiku wakati nikitokea mkoani…
Lowassa azindua helkopta ya kanisa la ufufuo na uzima, Askofu Gwajima ataka apewe eneo la Tanganyika Parkers
Joseph Zablon, Kawe Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameahidi kumsaidiana kwa maombi na njia zingine, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili aweze kulipata eneo la Tanganyika Pakers analolitumia kwa mahubiri ili ajenge kanisa kwa ajili ya waumini wake. Kauli ya Lowassa imefuatia ombi la askofu huyo wakati wa uzinduzi wa helkopta ya kanisa hilo ambayo ameahidi kuitumia kwa ajili ya kusaidia majanga yanapotokea na pia kusambaza neno la Mungu ambako alidai kuwa amesikia kuwa eneo hilo lipo katika mchakato wa kupatiwa mwekezaji. “Nasikia hapa kuna mtu anataka kulinunua hili eneo hivyo naomba sana ikiwezekana liuziwe kanisa langu ili liweze kujenga kanisa kwa ajili ya waumini” alisema Gwajima wakati anamkaribisha waziri mkuu mstaafu kuzungumza katika hafla hiyo. Alisema Lowassa kuwa ombi na kilio hicho amekisia na anahidi kushirikiana nao kuhakikisha wanapata ardhi kwa ajili ya kanisa hilo “Nitashirikiana nayi kwa maombi na njia zingine kuhakikisha mnapata ardhi kwa ajili ya kanisa hili” alisema. Alibainisha kuwa Gwajima ni mmoja kati ya viongozi wenye maono ambao kimsingi ndio wanaohitajika kwa ajili ya ustawi wa jamii.Awali Askofu Gwajima alisema kuwa helkopta hiyo ni moja kati ya zingine mbili zinazotarajiwa mwakani kwa ajili ya huduma za kanisa na uokozi. Alisema kuwa ameshawishika kuinunua baada ya kuona abiria waliokuwa katika meli yam v Spice walivyopoteza maisha kutokana na kukosa msaada hali ambayo inawapata pia majeruhi wa ajali zingine ambao wengi hufariki dunia wakiwa njiani kukimbizwa hospitalini. waziri mkuu mstaafu, Mhe Edward lowassa akiwasili viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es salaam kwa ajili ya uzinduzi wa helkopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima jijini Dar es Salaam.
Mhe Edward lowassa akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
Mhe Edward lowassa akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
waumini wakishuhudia uzinduzi wa helkopta hiyo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa
akiikagua helkopta hiyo mara baada ya uzinduzi.