Menu - Pages

Thursday, 20 November 2014

Obama kutangaza mabadiliko ya uhamiaji......source BBC



Ikulu ya Marekani imesema Rais Obama atatumia muda ambao watazamaji wa televisheni nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi kutangaza mabadiliko makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo.
Inatarajiwa kuwa Rais Obama atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba kuzuia wahamiaji wapatao milioni tano kurejeshwa makwao na badala yake wapatiwe vibali vya kufanya kazi nchini humo.

Rais Obama amesema hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa facebook kabla ya hotuba yake.Tangu kuingia madaraka Obama amekuwa akipigania baadhi ya mabadiliko ikiwemo huduma ya utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa bima ya afya.

Bill Cosby ashutumiwa kuwa mdhalilishaji......source BBC


Televisheni ya NBC imesitisha mradi wa kurusha kipindi cha mchekeshaji maarufu duniani, Bill Cosby baada ya kukabiliwa na shutuma zaunyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake .
Katika taarifa hiyo, kampuni imethibitisha kusimamishwa kwa kipindi hicho.
Siku ya jumanne kamouni inayotoa huduma ya vipindi vya video kwa njia ya internet, Netflix iliahirisha kipindi kilichomuhusu Cosby baada ya mwanamitindo mmoja kudai kuwa alidhalilishwa kijinsia mwaka 1982.
Mtandao wa Netflix ulikataa kutoa sababu ya kusitisha uzalishaji wa kipindi, lakini umesema kuwa maandalizi ya uzalishaji ulikua haujaanza. Cosby amekana kuhusika na vitendo hivyo.
Hatua hii imekuja baada ya mwanamitindo na mtangazaji kipindi cha Televisheni Janice Dickinson kusema kuwa alidhalilishwa na Cosby walipokutana kwa ajili ya chakula cha usiku huko California mwaka 1982.
Janice amesema aliandika katika kitabu kinachohusu maisha yake kuhusu tukio hilo lakini alipata shinikizo kutoka kwa Mwanasheria wa Cosby na mchapaji wa kitabu chake kuondoa sehemu hiyo.
Mwanasheria wa Cosby Martin Singer amesema madai ya Dickinson ni ya uongo na hayana msingi.
Dickinson ni miongoni mwa wanawake kadhaa waliomshutumu kuwadhalilisha kijinsia miaka takriban 30 iliyopita.
Nae muigizaji wa zamani Barbara Bowman amesema alidhalilishwa na Cosby katika nyakati tofauti mwaka 1985 alipokuwa na umri wa miaka 17.
Mwanzoni mwa mwezi huu Barbara alisema alishindwa kupeleka mashitaka polisi kwa kuwa alihofu hataaminika.

Cosby hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la kihalifu.

Mkuu wa kampuni ya ferry Korea jela....


 Mahakama moja nchini Korea kusini imemhukumu miaka kumi gerezani mkurugenzi mkuu wa kampuni iliyoitengeza feri ya Sewol iliyozama mwezi Aprili na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300, wengi wao wakiwa ni watoto.
Mahakama ya wilaya ya Gwangju imeelezwa kwamba feri hiyo ilikarabatiwa kuweza kubeba mizigo zaidi na mabadiliko hayo yaliongeza uwezekano wa chombo hicho kupindukia.
Mapema mwezi hu kapteni wa feri hiyo, alihukumiwa miaka 36 kwa kukwepa majukumu yake. Mmiliki wa kampuni hiyo alifariki akitoroka.
Wapiga mbizi waliiokoa miili 295 kabla ya serikali kusitisha shughuli hiyo ya kutafuta miili zaidi wiki iliyopita. Bado waathirwa tisa hawajulikani waliko.