Menu - Pages
▼
Wednesday, 17 December 2014
Kijana mzungu abadilika kuwa m'masai..
Aliposafiri nchini Kenya mwaka 2011 kama mtu aliyejitolea katika shirika moja lisilo la kiserikali ,uamuzi wa kuwa kijana wa kimasai wa Ilchamus lilikuwa wazo la mwisho katika akili ya Max Roing,ambaye ni raia wa Sweden.
Lakini miaka mitatu baadaye ,Max mwenye umri wa miaka 25 amependa sana utamaduni wa watu hao walio wachache katika fukwe za ziwa Baringo.
Max pia alikuwa miongoni mwa vijana 5,000 wa Ilchamus katika kaunti ya Baringo waliotawazwa kuwa wanaume kamili baada ya kupashwa tohara.
''Nilikuja nchini Kenya kama mtalii na pia kusaidia kuhifadhi mazingira kupitia upandaji wa miti katika kaunti ya kajiado''bwana Roing aliliambia gazeti la Nation nchini Kenya baada ya kuhitimu.
Kwa sasa anafuata mila yake mpya inayoshirikisha mavazi yanayovaliwa pamoja na shuka nyeusi,simi iliofungwa katika ukanda wake wa rangi ya hudhurungi,viatu vyeusi na nguo iliorembeshwa kwa shanga.
Hafla hiyo ya kuhitimu imemfanya kuingia katika umri wa Ilmeng'ati.
''Mimi ni Max Lemeyan Le Kachuma kutoka kabila la Ilchamus na ukoo unaojiita Iltoimai''alisema jina lake huku akinywa maziwa yalio chungu katika kikombe.
Ebola:Msako wa wagonjwa kufanywa S.Leone
Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ametaka kufanyika kwa msako wa nyumba hadi nyumba kwa waathiriwa wa ugonjwa wa ebola nchini humo
Aidha, Rais huyo amepiga marufuku biashara siku ya Jumapili..... >>>>INGIA HAPA<<<<
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania ajiuzulu.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia jana, Jumanne, kufuatia sakata....... >>>>INGIA HAPA<<<<
Pakistan yaomboleza mauaji ya watoto
Raia nchini Pakistan wanaadhimisha siku tatu za maombolezo kuwakumbuka zaidi ya watu 140 waliouwawa,karibia wote wakiwa...>>>>INGIA HAPA<<<<