Ebola:Msako wa wagonjwa kufanywa S.Leone
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa msako wa nyumba kwa nyumba unaanza kote nchini humo kuwatambua watu walio na ugonjwa hatari wa ebola.
Aidha, Rais huyo amepiga marufuku biashara siku ya Jumapili.
Katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, Koroma amesema kwamba usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine ni marufuku.
Juma moja lililopita, wakuu walifutilia mbali mikutano yote na sherehe za siku kuu ya krismasi na mwaka mpya kama njia ya kukabiliana na kusambaa zaidi kwa ebola.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde kutoka shirika la afya Duniani WHO, Sierra Leone ni taifa ambalo limeathirika pakubwa na ebola ambapo zaidi ya visa elfu nane vimeripotiwa.
''Musiwafiche wagonjwa'',alisema rais.
Mbali na kufutilia mbali biashara za siku ya jumapili,mikakati hiyo mipya itashirikisha mda wa kununua bidhaa siku ya jumamosi na katikati ya wiki.
Mji wa Freetown umerekodi zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi ya ugonjwa wa ebola nchini Sierra leone katika kipindi cha majuma mawili yaliopita.
Mwandishi wa BBC nchini Sierra Leone Umaru Fafana amesema kuwa mikakati hiyo inalenga kudhibiti makundi ya watu.
Amesema kuwa wakaazi wa mji wa Freetown wanaendelea kujumuika katika barabara mbali na kufanya mazoezi kwa pamoja licha ya tishio hilo la Ebola.
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania ajiuzulu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia jana, Jumanne, kufuatia sakata la uchotaji wa fedha kutoka akaunti ya ESCROW ambapo zaidi ya dola milioni 120 zilihamishwa.
Mwanasheria mkuu, pamoja na baadhi ya wanasiasa na maafisa waandamizi wa serikali walituhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha kufanyika kwa miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta.
Leonard Mubali ameandaa taarifa ifuatayo:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, imesema Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali.
Katika barua yake kwa Rais Kikwete, Jaji Werema amesema ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali ilipeleka pendekezo kumtaka Jaji Werema kuwajibika
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Baada ya uchunguzi kuwasilishwa katika mkutano wa bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Novemba, kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hii na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika na wengine kuondolewa katika nyadhifa zao za kuteuliwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe
Kamati hiyo ya Bunge pia ilipendekeza kuwa waziri wa Nishati na Madini, waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mwanasheria mkuu, katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.
Pia maazimio ya Kamati ya kudumu ya bunge ilipendekeza kuwa, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya Tanesco na makampuni binafsi imeisababishia Tanesco hasara ya mabilioni ya fedha na kutishia uhai wake wa kifedha, serikali iwasilishe mikataba husika bungeni au kwenye kamati zake kwa lengo la kutekeleza vema wajibu wake wa kuimamia na kuishauri serikali.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilikuwa za juu mno. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hayo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao wawili lingepatikana.
Pakistan yaomboleza mauaji ya watoto
Raia nchini Pakistan wanaadhimisha siku tatu za maombolezo kuwakumbuka zaidi ya watu 140 waliouwawa,karibia wote wakiwa watoto katika shambulio lililotekelezwa na kundi la Taliban.
Waziri mkuu Nawaz Shariff ameitisha mkutano wa vyama vyote vya kisiasa nchini humo kujadili vile watakavyoweza kujibu shambulizi hilo la Peshawar.
Ameelezea shambulizi hilo kuwa janga la kitaifa lililotekelezwa na wakatili.
Mkuu wa jeshi Jenarali Raheel Shariff ameahidi kulipiza kisasi kwa kila tone la damu linalomwagika.
Nchini India ,shule zimenyamaza kwa dakika mbili ili kutoa heshima kwa wale waliouawa.
Tahadhari:'Hatari za urembo bandia'
Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.
Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii
Kwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.
Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.
Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya kidevu chake iliyohitaji kubadilishwa.
Matokeo,kidevu chenye umbo bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya hayo,anadhamiria kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.
'Uasi mkubwa'
Katika nchi hii,wazazi wananielezea kuwa wanawapa mabinti zao zawadi ya 'upasuaji maradufu wa vibugiko vya macho'' inayowezesha macho yao kuonekana zaidi-''kwa kweli huku ni kupunguza maumbile ya Kiaasia.Sijui mbona kwani macho ya Kikorea yanavutia sana vile yalivyo.
''Msisitizo unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!
Isipokuwa kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema ''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.
Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''
'Gharama si mchezo'
Kim Bok-soon alitumia Won milioni 30 (£17,320) kwa jumla ya upasuaji mara 15 kwenye uso wake katika kipindi cha siku moja na baadaye akagundua kuwa daktari wake hakuwa mpasuaji wa kuongeza urembo bandia mwilini ambaye alimhadaa Kim BoK-Soon kutumia won (17,320) kufanya upasuaji mara 15 kwenye uso wake.
Sehemu ya shida ni kuwa upasuaji wa kuongeza urembo bandia una faida kubwa na kwa hivyo unawaalika madaktari wengi ambao hawajahitimu- ama madaktari wale waliohitimu katika nyanya zingine za utabibu.
Inadaiwa kuwa taratibu zimefanywa na wanaoitwa ''madaktari mapepo''.Katika kesi moja kotini,inadaiwa kuwa daktari alihepa chumba cha upasuaji wakati mgonjwa wake akiwa kwenye dawa za kuondoa fahamu na kupunguza uchungu na kuwacha kazi hiyo kufanywa na mpasuaji mwingine badala yake.
Juu ya hiyo, iliibuka kuwa madakatari hao wamejifanyia upasuaji wa kujiongeza urembo bandia kuilingana na picha zao kabla - na - baada ya upasuaji.
Kwa uhakika ni kwamba Chama cha madaktari wa upasuaji wa kuongeza urembo bandia Korea kimetoa wito kwa kuwepo na sheria kali ya madaktari na wanaotoa ujumbe. Wanahofia kwamba utangazaji mbaya unaharibu sifa ya sekta ambayo kwa kiasi kikubwa imesimamiwa vizuri.
'Biashara kubwa'
Lakini wao wanapigana na mseto huu, Upasuaji una faida sana, hata una bei ambazo zinadhoofisha upasuaji huo Marekani na Ulaya. Ni biashara kubwa sana huko Gangnam, hapa katika Seoul, bei ya "kurekebisha jicho" ni dola 1500 na ni shughuli inayochukua dakka 30 tu. hiyo huongezeka hadi dola 11,000 kwa upasuaji wa kurekebisha sura.
Lakini labda watu wa China ambao wanataka kuwa kwenye filamu au, wazazi wa Korea Kusini ambao wanadhani wanaweza kuwarembesha mabinti wao kupitia kisu cha upasuaji lazima watafakari njia ya kushtua ya kupitia kwenye mahakama.
Malkia aliyekuwa mshindi wa taji la urembo, alifanyiwa upasuaji wa kukuza kifua ambayo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani upasuaji huo ulifanya titi lake moja kuwa kubwa kuliko lingine.
Analaumu madaktari kwa kushindwa na matibabu na pia kwa kutomweleza kwa uwazi ". Angalia, huna haja ya upasuaji huu" "Upasuaji wa plastiki ni kama madawa ya kulevya," alisema. "Kukishafanya macho, utataka pua."
Na madaktari pia hawakwambii kuwa "uko mrembo sana ulivyo bila upasuaji" Masaibu yanayokupata baadaye kutokana na madhara ya upasuaji huo huwa ni juu yako mwenyewe.
Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi
amewasili nchini Uturuki baada ya safari iliyojaa hatari nchini Syria
kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua mjini Raqqa, mji unaokaliwa
na waasi wa Islamic State.
Raia wengi kutoka Ulaya wamejiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.
Monique alikwenda Uturuki mara ya
kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha kusafiri kwenda Syria kuoana na
mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye asili ya Uholanzi na Uturuki.
Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS.
Aicha
,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia
wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi
Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa.
Aicha aliondoka Uholanzi
mwezi Februari, akaolewa na Omar Yilmaz, mwanamgambo mwenye asili ya
Uturuki na Uholanzi ambaye alishawahi kuwa mwanajeshi nchini
Uholanzi,alitumia mbinu alizopatiwa akiwa mwanajeshi na kuwafunza
wapiganaji wenzake.
Monique amesema mwanae alibadilika ghafla kutoka binti aliyefahamika vyema na kuwa Msichana mwenye msimamo mkali.
Wapiganaji wa Islamic State wakifanya mashambulizi.
Baada ya Polisi kumuonya Aicha
kutosafiri kwenda Syria walikamata Pasi yake ya kusafiria, Aicha
hakuvunjika moyo alitumia kitambulisho chake.
Aicha alikuwa akiwasiliana na Yilmaz kwa njia ya mtandao wa kijamii kisha wakapendana.
Monique alisafiri mpaka Uturuki mwezi Oktoba ili kumchukua mtoto wake lakini alishindwa kuvuka mpaka.
Lakini
wiki iliyopita, baada ya Aicha kuomba msaada alirudi tena nchini Syria
ingawa Polisi walimkataza kufanya hivyo.Monique alifika Raqqa nchini
humo na kumchukua bintiye kisha kurejea Uturuki
Yilmaz, Mume wa Aicha anamtaja mkewe kuwa mtalaka wake kwenye anuani yake ya Tweeter.
Hivi sasa Mama na mwana wanashikiliwa mpakani mwa Uturuki, wakisubiri ruhusa ya kurudi Uholanzi.
Serikali
ya Uholanzi imeiambia BBC kuwa inawasiliana na Monique lakini haijatoa
ufafanuzi zaidi, tatizo ni kuwa Aicha hana Pasi ya kusafiria ingawa
mwanasheria wake anasema huenda wakarejea Uholanzi ndani ya wiki moja.
Familia
ya aliyekuwa mwanamuziki wa Jamaica, Bob Marley imezindua kampuni
ambayo wanaitaja kama ya kwanza duniani kuuza bidhaa za Canbbisa au
marujuana au Bangi kama wanavyoijua wengi.
Bidhaa hizo zitajulikama kama 'Marley Natural' na na zitajumuisha mafuta ya urembo pamoja na manukato mengine ya wanawake na bidhaa nyinginezo.
Bidhaa hizo zitatengezwa na kampuni kubwa ijulikanano Privateer Holdings iliyo mjini Washington Marekani, ikisisitiza kutaka kudumisha kumbukumbu ya mwanamuziki huyo aliyesifika kote duniani.
Bidhaa hizo zitauzwa nchini Marekani na kwingineko duniani kunzia mwaka jana.
Mwanawe Bob Marley, Cedella Marley, alisema hayati babake angekuwa hai angefurahishwa sana na wazo hilo.
''Babangu angekuwa na fahari kubwa kuona watu wakitambua uwezo wa kuponya wa Bangi,'' alisema Cedella.
Mkuu wa kampuni hiyo, Brendan Kennedy alisema Marley alikuwa mtu ambaye kwa njia nyingi alisaidia kuanzisha harakati za kupinga juhudi za kuharamisha Bangi miaka 50 iliyopita.
"Marley alipenda sana kutumia Bangi na hakuna aliyemshinda kwa hilo duniani kote. ''
Bob Marley alifariki mwezi Mei mwaka 1981, kutokana na Saratani.Alipenda sana kutumia Bangi kama sehemu ya imani yake ya Rastafarian na kuunga mkono kuhalalishwa kwake.
Matumizi ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa katika majimbo ya Colorado na Washington nchini Marekani.
Majimbo mengine huenda yakaidhinisha matumizi ya Bangi nchini Marekani na mengine tayari yanaruhusu utumiaji wa bidhaa hiyo kwa sababu za matibabu.
India imemuweka karantini mwanaume mmoja ambaye alipatiwa matibabu baada ya kuathirika na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia, kwa hofu kuwa huenda akasambaza virusi vya Ebola kwa njia ya kujamiiana.
Mtu huyo alipimwa na kukutwa hana virusi vya ugonjwa huo alipowasili Uwanja wa ndege wa Delhi.
Hata hivyo Maafisa wamesema amewekwa karantini kwa sababu virusi bado vilikuwepo kwenye mbegu zake za kiume ,ambapo vingeweza kusambaa kwa njia ya kujamiiana.
Vifo vingi vimeripotiwa Liberia,Guinea na Sierra Leone.
Wanaume ambao hufanikiwa baada ya matibabu hushauriwa kutoshiriki kitendo cha kujamiiana vinginevyo wahakikishe wanatumia mipira ya kiume,kwa kuwa mbegu za kiume hubeba virusi hivyo kwa siku 90 baada ya kutibiwa.
Waziri wa afya wa India amesema mwanaume huyo (26) alifika nchini humo tarehe 10 mwezi Novemba.Amekuwa akibeba nyaraka zake zilizoeleza kuwa alitibiwa maradhi ya Ebola nchini Liberia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya afya, pamoja na ushahidi huo sampuli za mbegu zake za kiume zilichukuliwa na kupimwa kisha kubainika kuwa bado virusi vya ugonjwa vipo. Wizara imesema ataendelea kubaki kwenye Karantini mpaka virusi hivyo viishe kabisa mwilini.
kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, takriban Raia 45,000 wa India wanaishi Afrika Magharibi. Hakuna mtu yeyote aliyripotiwa kuathiriwa na Ebola nchini India.
Mfuko
wa Bill na Melinda Gates umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7
kwa ajili ya mradi kusaidia matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini
Guinea na nchi nyingine zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
Mfuko
huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio.
Zaidi
ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka
Afrika Magharibi.
Mpaka
sasa hakuna dawa iliyoidhinishwa wala chanjo ya kupambana na Virusi
vya Ebola,matibabu ya hospitalini hutolewa kwa kuwapa wagonjwa maji
ili kufunga kuharisha na dawa za kupambana na vijidudu.
Hata
hivyo kuna chanjo kadhaa za majaribio na dawa za kutibu maradhi ya
Ebola, lakini hazijajaribiwa kwa ajili ya kuona usalama wake na namna
zinavyofanya kazi.
Shirika
la Madaktari wasio na mipaka, MSF linatarajia kuanzisha majaribio ya
tiba Afrika Magharibi mwezi Desemba.
Mfuko
huo unamilikiwa na mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates na
mkewe Melinda umesema kuwa utafanya kazi na washirika kadhaa kwa
ajili ya kutengeneza tiba.
Tiba
hiyo itatumia damu iliyotolewa na watu waliopona maradhi ya Ebola.
Akiongea
mwanzoni mwa mwezi huu, Bill Gates alisema utafiti zaidi kuhusu Ebola
unahitajika
0 comments:
Post a Comment