Wednesday 31 December 2014

Aua watu 8 naye ajiua Canada.



Polisi Nchini Canada wanasema kuwa watu 8 wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mmoja ambaye naye alijiuua katika kile kilichotajwa kama mfululizo wa unyanyasaji wa majumbani.
Siku ya jumatatu polisi walikuta mwili wa mwanamke mmoja katika mji wa Edmonton eneo magharibi mwa jimbo la Alberta.
Polisi pia waliikuta miili mingine ambayo ni ya wanawake watatu,wanaume wawili na watoto wawili wakati ilipokuwa ikishughulikia taarifa ya mtu huyo aliyejiua katika eneo jingine kwenye mji huo.
Muuaji huyo alijiua mwenyewe kwenye mgahawa mmoja katika eneo la kaskazini mwa Edmonton.
Polisi bado haijatoa majina wala uhusiano wa waathirika.
Share:

Miili 40 yaopolewa baharini.


Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.
Share:

Boko haram wavamia kijiji na kuua 15.


Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.
Shambulizi hilo lilitokea katika kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga askari wa ulinzi wa jadi wa mji huo.
Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, liliwateka nyara wasichana wa shule zaidi ya mia mbili mwezi Aprili mwaka huu.
Zaidi ya watu elfu kumi wameuwawa Nchini Nigeria na Boko Haram mwaka huu pekee.
Share:

Rais Jammeh:'Bado niko mamlakani.


Rais wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.
Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.
Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.
Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa.
Share:

MTUHUMIWA ALIYEJARIBU KUTOROKA MAHAKAMA YA KISUTU APIGWA RISASI.


























Maofisa wa Polisi na Magereza wakiangalia mwili wa mtu aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya dawa za kulevya na kupigwa risasi wakati akijaribu kutoroka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam saa 2:00 asubuhi ya leo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinapasha kuwa mwili wa marehemu huyo ambaye bado jina lake halijatambulika umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Muhimbili. Picha kwa hisani ya Father Kidevu.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.