Sunday 19 April 2015

Jacob Zuma aapa kukabiliana na ghasia

Rais Jacob Zuma amewatembelea watu walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo.

Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita.Amesema kuwa ghasia hizo ni kinyume na maadili ya taifa la Afrika kusini.

Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika maeneo yenye mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.

Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini.

Nchini Harare Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alilaani ghasia hizo.

Ghasia hizo zilianza baada ya mfalme mmoja wa Kizulu, Goodwill Zwelethini, kusema kuwa raia wa kigeni sharti waondoke Afrika Kusini.

Akiongea katika kambi hiyo iliyoko mjini Durban kiongozi mkuu wa jimbo la Gauteng, David Makhura, anasema kuwa uhasama na ghasia hizo zinazoshuhudiwa, haundamani na uhuru wa miaka mingi ambayo Afrika Kusini ilipigania.





Share:

Vita vya kikabila:Watu 45 wauawa Nigeria


Takriban watu 45 wameuawa kwenye mapambano ya kikabila katika jimbo la Benue, katikati mwa Nigeria.

Polisi wanasema ghasia hizo baina ya jamii za Ologba na Egba, zilizuka kutokana na umiliki wa bwawa la samaki.

Watu zaidi waliuawa pale kundi moja liliposhambulia mazishi ya mtu aliyekufa katika ghasia za awali.

Watu wengi wamelitoroka eneo hilo.

Kumetokea mapambano mengi katika jimbo la Benue katika miaka ya karibuni, lakini mara nyingi ni mizozo baina ya wafugaji na wakulima.
Share:

Dawa ya magugu yauwa watu Nigeria


Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inavoelekea dawa ya kuuwa magugu ndio chanzo cha vifo vya watu 18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.

Katika siku chache zilizopita wakaazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache baada ya kuhisi macho hayaoni sawasawa na kuumwa na vichwa, Baadae wakazimia.

Msemaji wa WHO alieleza kuwa ukaguzi uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu
Alisema kwa sasa mawazo yao ni kuwa vifo hivyo vilisa-babishwa na dawa ya kuuwa magugu.
Share:

IS watoa tena video ya mauaji


Kundi la wapiganaji wadola ya Kiislam IS limetoa video inayo onyesha mauaji ya zaidi ya watu 30 raia Ethiopia ambao ni Wakristo wakiuawa wengine kwa kuchinjwa katika ufukwe wa bahari na wengine kwa kupigwa risasi kichwani jangwani. Hata hivyo video hiyo inabainisha wazi kwamba kundi hilo la IS linawaua watu hao kwa sababu ni wakristo. Serikali ya Ethipia imesema kuwa inajaribu kufuatilia utambulisho wa utaifa wa watu hao kupitia ubalozi wa Cairo nchini Misri. Hali ya usalama nchini Libya imetetereka tangu kuangushwa kwa utawala wa Kanal Muamar Gadaf, ambapo pia ustawi wa kundi la kigaidi wa wapiganaji wa dola ya Kiislam umekuwa mkubwa.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.