Thursday 23 April 2015

Hasira zamfanya aipige kompyuta risasi


Mwamamme mmoja kwenye mji wa Colorado nchini Marekani huenda akachukuliwa hatua za kisheria kufuatia kisa ambapo alikasirishwa na kompyuta yake kisha akaitoa nje na kuifyatulia risasi mara nane.
Polisi wanasema kuwa Lucas Hinch alikuwa na matatizoya kiteknolojia ndipo akaipeleka kompyuta hiyo upande wa nyuma ya nyumba yake na kuiharibu ambapo alikamatwa muda mfupi baadaye.
Vyombo vya habari vilisema kuwa alichoka na kusumbuliwa na kompyuta yake lakini hakufahamu kuwa alikuwa akivunja sheria alipoiadhibu kwa risasi.
Gazeti moja lilisema kuwa wakati herufi za ctrl+alt+delete zilifeli , bwana Hinch alishikwa na hasira nna kuamua kulipiza kisasi kwa kuiharibu Kompyuta hiyo hadi kiwango ambacho haiwezi kutumika tena
Share:

Mashambulizi ya Yemen yawapa tuzo marubani


Mwana wa mfalme nchini Saudi Arabia ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini humo, ameshambuliwa katika mitandao ya kijamii baada ya kuwapa magari ya kifahari marubani wa ndege za kivita wa nchi yake ambao walishiriki katika kampeni ya kurusha mabomu na kuishambulia Yemen.
Mwanzoni mwa wiki hii Saudi Arabia iliweka bayana mwisho wa awamu ya kwanza ya kampeni yake ya kijeshi nchini Yemen.Katika sherehe za kufurahia matokeo ya kampeni hiyo ya kwanza mwana wa mfalme Al-Waleed bin Talal, ,aliweka maoni yake kwenye ukurasa wake wa twitter wenye wafuasi milioni tatu akisema kwamba; kwa kutambua na kuonesha nimethamini kile walichofanya askari wetu kwenye awamu hii ya kwanza ,ninajisikia fahari kuwazawadia askari ambao ni marubani pia wapatao mia moja magari aina ya Bentley kwa matokeo mazuri ya oparesheni yetu .
Pendekezo la zawadi hiyo kutoka kwa mawana wa mfalme lilikumbwa na upinzani mkali mara tu baada ya kuwekwa katika mtandao huo wa kijamii na kuwagawa wafuasi wake katika makundi mawili, zaidi ya wafuasi wake elfu ishirini na nane walitumiana ujumbe huo na zaidi ya wafuasi wake elfu tano waliupenda ujumbe huo.

Mwana wa mfalme huyo alisifiwa kwa moyo wake wa ukarimu na wasaudia wengi, ambao walitoa maoni yao juu ya uamuzi wake huo,na kusema kwamba marubani hao wanastahili magari hayo ya kifahari na zaidi ya hayo kwa kazi yao nzuri ya kutukuka waliyoifanya nchini Yemen.
Hata hivyo ujumbe huo wenye kutoa zawadi nono kwa marubani hao umefutwa katika akaunti yake ya twitter,ingawa hapo awali ujumbe huo ulishasambazwa na unaendelea kusambaa mitandaoni.
Na baadhi ya vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vimeripotiwa kudai kuwa akaunti ya mwana wa mfalme ilikuwa imedukuliwa ,ingawa hakukuwa na taarifa yoyote hapo awali iliyolalamikia udukuzi huo ,na mwana wa mfalme huyo mpaka sasa ameamua kupiga kimya, wala hajasema neno.
Mwaka uliopita, mwana mfalme huyo,anayetambuliwa kwa mahaba yake ya kupenda maisha ya kifahari na mwenye mkono mwepesi wa kutoa zawadi kubwa kubwa ,mwaka huo inaarifiwa kuwa aliipatia timu ya mpira wa miguu ya nchi hiyo magari ishirini na matano baada ya kushinda michuano ya kandanda ya nchi hiyo,suala ambalo lilizua mjadala yakwamba nani anapaswa kutoa zawadi nchini humo na nani hastahili kutoa zawadi.
Share:

Raisi wa Everton afariki dunia

Rais wa heshima wa klabu ya Everton Sir Philip Carter amefariki akiwa na miaka 87.
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Everton imethibitisha kifo hicho na Kueleza Carter alifariki akiwa nyumbani kwake Alhamisi asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Carter, alikua mshabiki wa timu hii tangu utotoni ambapo mwaka 1973 alijiunga na timu kama mkurugenzi na mwaka 1978 akawa mwenyekiti wa timu.
utoto Everton shabiki, alijiunga na klabu kama mkurugenzi mwaka 1973. Yeye alipata nafasi ya mwenyekiti mwaka 1978 na aliendelea ataongoza kipindi cha mafanikio ndani na Ulaya
Wakati wa uongozi wake kama mwenyekiti akiwa na meneja Howard Kendall ,Carter , alishinda mataji mwaka ya FA cup 1985 na 1987, 1984 na Kombe la Ulaya 1985.
Alichaguliwa kuwa Raisi wa heshima wa maishan wa timu ya Everton mwaka 2004
Share:

Akiri kudanganya kuhusu tiba ya Saratani


Mwanablogu aliyelimbikiziwa sifa baada ya kudai kwamba alimiliki dawa za kuponya ugonjwa wa saratani ya ubongo kupitia tiba ya kiasili amekiri kwamba alidanganya kuhusu ugonjwa wake.
Belle Gibson alianza kazi iliojawa na mafanikio mbali na uzinduzi wa kitabu cha mapishi kufuatia madai ya afueni ya kimiujiza.
Lakini wengine walipoanza kumuuliza kuhusu habari hiyo aliliambia gazeti moja la nchini Australia kwamba hajawahi kuwa mgonjwa.
Alisema kuwa alipambana na maisha kuhusu kusema ukweli.
Shirika moja la wahisani wa saratani limewataka wagonjwa kuwa na hofu punde wanapoelezwa kuhusu tiba zisizoaminika.
Share:

Wanawake wanaokuwa watawa waongezeka UK


Idadi ya wanawake wanaokuwa watawa imeongezeka pakubwa katika kipindi cha miaka 25,kanisa katoliki nchini Uingereza na Wales limesema.
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake wanaokula viapo vitakatifu imeongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka mitano kutoka wanawake 15 mwaka 2009 hadi 45 mwaka uliopita,ikiwa ni idadi kubwa tangu mwaka 1990.
Wanawake 14 walioingia katika utawa mwaka 2014 walikuwa na miaka 30 ama chini yake ,takwimu mpya zinaonyesha.
Kanisa hilo linasema kuwa wanawake wanajiingiza katika maisha ya kidini kutokana na pengo la utamaduni kutotiwa maanani.
Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 1980 takriban wanawake 80 walijiunga na utawa lakini idadi hiyo ilipungua hadi mwaka 2004 ambapo wanawake saba pekee walijiunga na utakatifu huo.
Idadi hiyo imeongezeka katika kipindi cha miaka 10 ambapo ilifika 45 mwaka 2014.
Share:

Alshabaab washukiwa kumteka nyara Chifu


Wanamgambo wanaoaminika kuwa Al Shabaab wamemteka nyara chifu na gari la miraa katika eneo la Arabia, kaunti ya Mandera.
Shambulizi hilo limetokea mapema siku ya Alhamisi , na maafisa wa usalama wako katika harakati ya kuwaokoa manusura waliotekwa nyara.
Viongozi wamesema washambuliaji walionekana kufahamu eneo hilo na pia Chifu waliyemteka nyara. Inasemekana kuwa Chifu huyo alikuwa akielekea Mandera wakati wa shambulizi hilo.
Awali katika idhaa yaa BBC Somali tuliweza kuzungumuza na mwakilishi wa kaunti katika wadi ya Arabia na kaweza kutuhakikishisa shambulizi hilo na vile vile alisema kuwa wanashuku wanamgambo wa Alshabab ndio waliofanya kitendo hicho.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka serikali kuhusiana na utekaji nyara na muda mfupi uliopita kulikuwa na taarifa isiyo thibitishwa kuwa chifu huyo ameuwawa na Alshabaab.
Kutokana na swala hili la Usalama wanasiasa jimbo la Mandera waliweza kuongea na wanahabari huku wakilaani kitendo hicho huku wakihimiza serikali kuimarisha usalama katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa Kenya.
Share:

Boko Haram labadilisha jina Nigeria


Picha mpya zimetolewa kuhusu wapiganaji wa Boko Haram ambao wanajielezea kuwa Islamic State Jimbo la Magharibi mwa Afrika.
Kundi hilo limekuwa watiifu kwa wapiganaji wa Islamic State mwezi uliopita.
Baadhi ya wanajeshi wa Nigeria ambao wameshirikishwa katika oparesheni ya kulishinda kundi hilo katika msitu wa Sambisa uliopo Kazkazini mashariki wamelazimika kurudi nyuma kwa kuwa wanadhani kwamba huenda msitu huo umewekwa mitego.
Mwanachama wa kundi moja la kuweka usalama mtaani JTF ameiambia BBC kwamba mwanajeshi mmoja na walinzi watatu wa mitaani waliuawa wakati gari lao lilipopita juu ya mtego.
Share:

Obama:Mateka waliuawa kwa bahati mbaya


Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa watu wawili waliokuwa wamezuiliwa na wapiganaji katika nyumba moja nchini Afghanistan, waliuwawa kimakosa na majeshi ya Marekani yanayopambana na ugaidi katika maeneo ya Afghanistan na Pakistan.
Akisoma taarifa kuhusiana na vifo hivyo, Rais Barrack Obama, amesema kuwa amesikitishwa mno na kisa hicho kilichofanyika Januari mwaka huu.
Anasema watu hao walikuwa wamezuiliwa na wapiganaji wa al Qaeda, kwa miaka kadha.
Wametajwa kama Mmarekani Warren Weinstein, na Giovanni Lo Porto raia wa Italia.
White House inasema pia kuwa, raia wengine wawili waliouliwa walikuwa waamerika, na wanachama wa kundi la al Qaeda.
Share:

Waandamana kupinga ubaguzi Afrika Kusini


Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wanaandamana kupinga wimbi la visa vya hivi majuzi vya mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni.
Mikutano mikubwa imeandaliwa katika mji mkuu Johannesburg na katika mji wa Port Elizabeth ulioko kusini mwa nchi hiyo ambao ulishuhudia mashambulio kadhaa dhidi ya wahamiaji wa mataifa ya kigeni mnamo mwaka 2008.
Makundi ya kiusalama yanafanya misako katika majumba ya makaazi katika mji wa Alexandra mjini Johannesburg, mahala ambapo mashambulio kadhaa dhidi ya raia wa kigeni hasa Afrika yalifanyika katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita.
Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, kuonekana kwa walinda usalama barabarani kumeleta udhibiti na amani.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.