Wednesday 27 May 2015

Bolt ashinda mita 200


Mwanariadha raia wa Jamaica Usain Bolt ameshinda kwa urahis katika shindano lake la kwanza mwaka huu huko barani Ulaya japokuwa ameshindwa kuvunja rekodi yake ya sekunde 20, kwenye mbio za mita 200 za Golden Spike huko Ostrava Jamhuri ya Czech.
Katika shindano hilo lililofanyika jana Bolt alitumia sekunde 20.13 ikiwa ya rekodi yake ya dunia ya sekunde 19.19 akimbwaga mmarekani Isiah Young "huwezi ridhika kama sivunji sekunde 20" alisema Bolt ambaye anajiandaa kwa mashindano ya dunia yatakayofanyika Beijing mwezi August. Naye Asafa Powell ameshinda katika mbio za mita 100 akitumia sekunde 10.04.
Share:

Wakili nchini Kenya kuwa mkwe wa Obama?


Taarifa kuwa wakili mmoja wa kenya amesema yuko tayari kutoa mahari kwa mtoto wa raisi wa Marekani,Barrack Obama zimeenea duniani kote Felix Kiprono amesema yuko tayari kutoa ng'ombe 50,kondoo 70 na mbuzi 30 kwa ajili ya mahari ya mtoto wa Obama,Malia Obama.Hivyo anajiandaa kuzungumzia swala hilo na baba wa mtoto huyo atakapo tembelea Kenya ,mwezi Julai.
Share:

Rushwa:Maafisa wa Soka wakamatwa Zurich.


Waandishi wa Habari wakishuhudia kukamatwa kwa maafisa wa Soka nje ya hoteli mjini Zurich

Maafisa sita wa shirikisho la soka duniani Fifa wamekamatwa katika hoteli moja mjini Zurich,Switzerland. kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Watuhuhumiwa hao ambao wanasemekana kuwa ni pamoja na makamu wa rais wa Fifa,wanashikiliwa wakisubiri kusafirishwa kwenda Marekani.
Shutma hizo zinahusisha rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20
Wanachama wa Fifa wanakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku ya ijumaa, ambapo rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter anawania muhula wa tano.
Mwana mfalme Ali Bin Al-Hussein wa Jordan,ambaye ndiye mpinzani pekee wa Blatter amesema tukio hilo ni "baya kwa maendeleo ya soka".

Rais wa Fifa ambaye anawania muhula wa tano ndani ya shirikisho hilo, Sepp Baltter

Gazeti la New York Times limesema askari kanzu walichukua funguo za chumba cha hoteli kutoka eneo la mapokezi ya hoteli ya Baur au Lac hotel ambayo maafisa hao walikuwa wakiishi na kuingia vyumbani mwao.Gazeti hilo limesema Operesheni hiyo ilifanyika kwa utulivu.
Jeffrey Webb, Mkuu wa shirikisho la Amerika ya Kaskazini na Kati na Visiwa vya Caribbean ametajwa kuwa mmoja kati ya maafisa waliokamatwa.
Maafisa wengine wa Fifa walishuhudiwa na BBC wakisindikizwa na Polisi kutoka kwenye hoteli hiyo ni:
Mkuu wa Shirikisho la soka la Costa Rica, Erduado Li, ambaye alikuwa akitarajia kuwepo kwenye mkutano wa kamati ya Fifa siku ya ijumaa.Wengine ni rais wa shirikisho la Uruguay Eugenio Figueredo,rais wa shirikisho la soka Amerika kusini Conmebol na wa Brazil,Jose Maria Marin,mwanakamati ndani ya Fifa,Polisi walionekana wamebeba mikoba yake kwenye mifuko ya Plastiki.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa vipi Blatter amekuwa Kiongozi wa Fifa kwa muda mrefu, pamoja na kuwepo kwa ripoti nyingi za vitendo vya rushwa lakini ameendelea kushikilia wadhifa huo.
Wizara ya sheria ya Uswiss imesema katika tamko lake siku ya jumatano kuwa maafisa wa serikali ya Marekani waliwashuku maafisa hao kupokea rushwa ya dola milioni 100, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa ajili ya michuano ya Amerika ya kati.
Serikali ya Uswiss imesema itaidhinisha haraka kusafirishwa kwao.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu baadhi ya wafanyakazi wenzake wa zamani walikuwa wakichunguzwa lakini amekanusha kuwa uchunguzi huo ulimhusu pia.
Share:

AfDB kupata rais mpya kumrithi Kaberuka.


Rais wa Benki ya maendeleo Afrika, Donald Kaberuka

Benki ya Maendeleo ya Afrika inaendesha shughuli zake chini ya uongozi wa rais, ambaye anafanya kazi kama mwakilishi halali wa Benki, mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na mnadhimu wa Benki hiyo. Rais anaendesha shughuli za sasa za Benki, chini ya maelekezo ya Bodi ya Wakurugenzi. Rais huchaguliwa na Bodi ya Magavana na anahudumu kwa miaka mitano. Pia anaweza kurudia kipindi kimoja tu cha miaka mitano mingine.
Rais wa sasa wa AfDB, Dr. Donald Kaberuka, raia wa Rwanda, alichaguliwa mwezi Julai 2005,na alianza awamu yake ya kwanza Septemba Mosi 2005. Kufuatia kuchaguliwa kwake tena mwezi Mei 2010, alianza kipindi chake cha pili cha miaka mitano mingine Septemba Mosi 2010. Kwa mujibu wa taratibu za uongozi katika Benki hiyo, Bodi ya Magavana inalazimika kumchagua mtu mwingine kuchukua nafasi hiyo
Wanaowania kushika nafasi hiyo ni:

Birima Sidibe, Mali Birama Sidibe ni mhandisi ambaye amejikita katika utaalam kilimo umwagiliaji. Kwa zaidi ya miaka thelathini, alikuwa akifanya kazi katika sekta ya maendeleo. Alifanya kazi na Benki ya Maendeleo ya Afrika tangu mwaka 1983-2006. Birama Sidibé pia alifanya kazi katika benki ya Maendeleo ya kiislamu, mjini Nairobi na kwa ajili ya shirika la River Senegal.

Benki ya Maendeleo ya Afrika

Jalloul Ayed, Tunisia Jelloul Ayed ni mfanyakazi wa benki mwenye mafanikio nchini mwake na ana umri wa miaka 64. Yeye pia anajulikana kwa kuendesha harambee ya kuchangisha fedha zilizotolewa katika soko la Ulaya kwa ajili ya kampuni za Tunisia na Morocco. Mwaka 2011, akiwa waziri wa fedha wa mpito wa serikali baada ya kuanguka kwa Serikali ya aliyekuwa rais wa Tunisia Ben Ali, aliwahi kuwasilisha programu ya maendeleo ya kijami na kiuchumi katika mkutano mkuu wa G8. Bedourma Kordje, Chad, Ni waziri wa fedha nchini Chad sasa ivi, huyu mhandisi wa mawasiliano ya simu kwa miaka 29 ameitumikia benki ya maendeleo Afrika kabla ya kurudi nchini kwake na kuwa waziri wa fedha mwaka 2012. Rais Idriss Deby ameahidi kushawishi wanachama wa jumuiya ya afrika ya kati kwa ajili ya uchaguzi wa benki ya maendeleo ya Afrika AfDB.

Cristina Duarte, Sura Verde Ni mgombea mwanamke pekee kwa nafasi hii, lakini si kwa sababu yeye ni mwanamke, bali Anataka aangaliwe kwa uwezo wake wa kazi pia na si jinsia yake. Amelirudia mara kadhaa hilo na pengine ni sahihi. Amekuwa waziri wa fedha wa nchi yake tangu mwaka 2006. Anasifa kubwa ya kufanya mageuzi na kunyanyua uchumi wa nchi yake. Amefanya kazi pia na mashirika tofauti ya kimataifa ya kuleta maendeleo. Adesina Akinwumi, Nigeria Ni waziri wa sasa wa Kilimo na Maendeleo ya vijijini, Nigeria. Ana miaka 55 na amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA). Elimu yake ni shahada ya juu ya uzamivu katika uchumi wa Kilimo.Jarida liitwalo Forbes lilimtunuku jina la mwafrika wa mwaka 2013 kutokana na mageuzi yake katika sekta ya Kilimo.

Wanaowania Urais wa Benki ya maendeleo Afrika

Sufian Ahmed, Ethiopia Waziri huyu wa fedha na maendeleo ya kiuchumi mwenye umri wa miaka 57 anataka kutumia matokeo mazuri ya kiuchumi ya nchi yake kama mtaji kwa ajili ya kazi anayo iomba. Anasifika kwa kiasi kikubwa sana kwa kuwa na mchango mkubwa wa kiuchumi nchini mwake. Kamishna huyu wa zamani wa Mamlaka ya Forodha Ethiopia anajichukulia kama mwanamatumaini wa kiafrika. Pia elimu yake yote ameipatia nchini mwake.

Samura Kamara, Sierra Leone Ni mfanyakazi wa zamani wa shirika la fedha duniani, IMF na sasa ni waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa pia ni mwanamchumi mzoefu. Hiyo ni sababu kuu ya Rais Ernest Bay Koroma ametaka awe mjumbe wa serikali yake. Yeye awali alikuwa waziri wa Fedha. Ushirikiano wa Afrika ni kati ya mada kuu ya kampeni zake.

Thomas Sakala, Zimbabwe SADC imemchagua Raia wa Zimbabwe huyu kuwa mgombea wa kanda ya kusini mwa Afrika. Alistaafu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika mwaka jana tu na hadhi yake hiyo inaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kinyang'anyiro hicho. Alifanya kazi na serikali nyingi za Afrika katika programu mbalimbali. Yeye anapigia upatu maendeleo ya miundombinu miongoni mwa masuala mengine.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.