Friday 28 November 2014

Bunge lasambaratika Tanzania........


Mzozo mkubwa umesababisha Bunge la Tanzania kuvunjika usiku huu wakati likiendelea na mjadala wa kashfa ya Escrow, baada ya wabunge kushindwa kukubaliana njia sahihi ya kuwawajibisha baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la wizi wa Zaidi ya fedha za Tanzania shilingi bilioni 300 kutoka Benki Kuu ya nchi hiyo.
Taarifa ya mwandishi wa BBC Baruan Muhuza imesema kuwa Bunge hilo, leo limeweka rekodi ya kuwa na mjadala wa muda mrefu Zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Hadi kufikia kuvunjika kwa kikao hicho ilikuwa ni saa 4.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Spika wa Bunge hilo Anne Makinda karibu muda wote wa kikao hicho alijikuta akitoa tahadhari kwa wabunge wake kujilinda na hatua za kuingilia mihimili mingine ya utawala ya Tanzania ambayo ni Mahakama na Serikali. Hatua hiyo kwa namna Fulani iliamsha hisia tofauti kutoka upande wa kambi ya upinzani pamoja na wajumbe wa kamati ya hesabu za Serikali ambao walitishia kutoka nje hadi viongozi wanaodaiwa kulindwa na bunge hilo wawajibike wenyewe. Bunge hilo linategemewa kuendelea na kikao chake hapo kesho.


Share:

Ikulu ya Tanzania yahusishwa na Escrow..........BBC


Bunge la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.
Bwana Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo kama ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu.
Kushirikishwa kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa iliopita.
Kiongozi wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa bunge upande wa upinzani bwana Tandu Lissu alifichua jukumu lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa mabilioni hayo ya fedha.

Ripoti hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa miongoni mwa watu maarufu.
Share:

Mtoto mchanga anusurika kuuawa Kenya.....


Mtoto X amelala kwa utulivu, akiwa amefunikwa na Blanketi lenye kumpa joto na kukumbatiwa na Mama yake katika Nyumba moja ya kulelea Watoto yatima nchini Kenya.
Mtoto huyu ni wa miezi miwili hivi sasa, alizaliwa kufuatia tendo la ngono kati ya msichana na Mjomba wake, mtoto huyu anaelezwa kupatikana katika mazingira ya miiko.
Katika nyumba ya watoto wa Kanduyi, mjini Bungoma magharibi mwa Mji wa Nairobi, kama ilivyo kwa Watoto wengine , Mtoto huyu aliokolewa kutoka kwenye Familia yake kulipokua na mipango ya kuuawa.
Katika tukio hilo,siku mbili tu baada ya kuzaliwa Mtoto X, baada ya kupewa Taarifa vikosi vya usalama vilivamia makazi ya mtoto huyo na kumchukua wakiyaokoa maisha yake kutokana na kifo kilichokuwa kinamkabili mbele yake, kifo kilichaoamriwa na wazee wa kimila wa jamii iitwayo Bukusu.
Kuna watoto kama yeye katika nyumba hii ya Kunduyi wenye umri kati ya siku moja mpaka miaka 18.
Watoto waitwao 'mwiko'
Kujamiiana kwa maharimu ni mwiko nchini Kenya kama ilivyo katika maeneo mbalimbali, kwa mujibu wa Sheria ya Kenya, hilo ni kosa lenye kuadhibu kwa kifungo cha miaka mitano,au kifungo cha maisha kwa kujamiiana na binti wa umri mdogo

Lakini kwa Karne nyingi, adhabu ya kimila katika Jamii nyingi za Kenya ni kifo,na katika jamii ya Bukusu si lazima Mwanaume na Mwanamke waliohusika, lakini pia mtoto atakayezaliwa kutokana na uhusiano ulio mwiko.









Waziri wa utamaduni katika Kaunti ya Bungoma,Stephen Kokonya amesema kumekuwa na mahusiano ya namna hii yameenea katika jamii na kuongeza kuwa si sheria kwa jamii kutoa adhabu ya kifo, ni Jaji pekee anayeweza kuhukumu.Kokonya amesema katika maeneo ya kijijini hii ni sehemu ya Sheria za kijamii watoto kuonekana kuwa wamelaaniwa.
Watu wa jamii ya Bukusu huwaita Watoto hawa ''be luswa'' wakimaanisha ''Watoto haram'' wakihofu kuwa watasababisha kupata laana kama utasa na magonjwa ya akili.
''Kila mara tunaposikia mtoto anayedaiwa kuwa haramu amezaliwa katika eneo lolote huwa tunakimbia upesi kumuokoa vinginevyo unaweza kufika na kuambiwa tayari Mtoto alishakufa''Afisa anayetunza Watoto katika nyumba ya Watoto wa Kanduyi,Alice Komotho ameiambia BBC.
Kokonya amesema Serikali inatoa elimu ya uelewa kuhusu vitendo vya adhabu zitolewazo kinyume cha sheria ya nchi na Wazee wa jamii ya Bukusu.
Kisa cha Msichana.
Mama wa miaka 15 ambaye mtoto wake aliokolewa amerudi shuleni,binti huyu wa miaka 15 alibakwa na Mjomba wake. Msichana huyu amesema Mjomba wake alimtishia kuwa atampiga ikiwa atatoa taarifa kuhusu tukio la kubakwa, binti huyu alibakwa na mjomba wake mwenye umri wa miaka 17.
Msichana huyu hivi sasa amerudi shuleni kurudia mwaka wake alioupoteza alipokua mjamzito.
Binti huyu anaeleza kuwa hana mapenzi na Mjomba wake wala mtoto wao.
Mama huyu mdogo ameiambia BBC kuwa anapenda kuwa Daktari atakapomaliza masomo.
Maafisa wanasema kuwafundisha wazee wa kimila itakua ni njia nzuri ya kumaliza mila na desturi mbaya katika maeneo ya vijijini.
Mjomba wa Msichana huyo alikataa kuzungumza na BBC baada ya kuwasiliana nae.
Haki ya Kuishi
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wazee wa Bukusu anaeleza namna mtoto anavyouwawa,anakataa kuzungumzia kisa cha Mtoto X lakini anaeleza namna mtoto wanayedai kuwa haramu anavyouawa, anaeleza..
''Wakati binti anapokaribia kujifungua,huwakusanya baadhi ya Wanawake ambao hujifanya kama wanakwenda kumsaidia mzazi badala yake humziba pumzi mtoto kwa kuzibana nyonga za mama na kumuua Mtoto.
Wakinamama hawa hufanya haya kwa makini wakiamini kuwa ni budi mtoto kufa ili mzazi aishi katika jamii kwa amani.
Mzee mwingine anasema pia Wanakijiji wakati mwingine huua uzao wa pili ambao huwa pacha kwa madai kuwa huleta hali ya bahati mbaya, ambao wanapenda kubaki na watoto wao hulazimishwa kuondoka kijijini hapo.
Lakini Waziri wa utamaduni anasema kuwa angependa kuwakumbusha Wazee wote ambao hukaa na kuamua maamuzi ya mauaji kuwa wanaingilia haki ya msingi ya kuishi.
Share:

Msikiti washambuliwa nchini Nigeria..........BBC






















Taarifa kutoka mjini Kano, Kaskazini ya Nigeria, zinasema kuwa watu wengi wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu.
Ni baada ya milipuko mitatu inayoaminika kuwa ya mabomu kutokea katika msikiti mkubwa zaidi mjini humoulio katikati mwa jiji karibu na eneo anakoishi Emir au kiongozi wa waisilamu nchini humo Muhammad Sanusi.
Emir huyo kwa sasa yuko nchini Saudi Arabia.
Mabomu hayo yalilipuka wakati maombi ya Ijumaa yalipokuwa yanaendelea.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, alihesabu karibu miili 50 ya waliofariki katika shambulizi hilo.
Taarifa zingine zinasema watu waliokuwa wamjihami waliaingia msikitini humo na kuanza kufyatua risasi baada ya mabomu kulipuka.
Wapiganaji wa Boko Haram, wamekuwa wakifanya mashambulizi katika mji huo ambao ni mkubwa zaidi Kaskazini ya Nigeria.
Mapema mwezi huu , Emir alitoa wito kwa watu kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram.
Aliwashauri wakazi kujihami na kufanya kila wawezalo kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo.

Msemaji wa Polisi alisema matamshi ya Emir, yalikuwa ya uchochezi na kwamba watu wanapaswa kumpuuza.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.