Mzozo
mkubwa umesababisha Bunge la Tanzania kuvunjika usiku huu wakati
likiendelea na mjadala wa kashfa ya Escrow, baada ya wabunge
kushindwa kukubaliana njia sahihi ya kuwawajibisha baadhi ya viongozi
wa kisiasa wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la wizi wa Zaidi ya fedha
za Tanzania shilingi bilioni 300 kutoka Benki Kuu ya nchi hiyo.
Taarifa
ya mwandishi wa BBC Baruan Muhuza imesema kuwa Bunge hilo, leo
limeweka rekodi ya kuwa na mjadala wa muda mrefu Zaidi kuliko wakati
mwingine wowote. Hadi kufikia kuvunjika kwa kikao hicho ilikuwa ni
saa 4.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Spika wa Bunge hilo Anne
Makinda karibu muda wote wa kikao hicho alijikuta akitoa tahadhari
kwa wabunge wake kujilinda na hatua za kuingilia mihimili mingine ya
utawala ya Tanzania ambayo ni Mahakama na Serikali. Hatua hiyo kwa
namna Fulani iliamsha hisia tofauti kutoka upande wa kambi ya
upinzani pamoja na wajumbe wa kamati ya hesabu za Serikali ambao
walitishia kutoka nje hadi viongozi wanaodaiwa kulindwa na bunge hilo
wawajibike wenyewe. Bunge hilo linategemewa kuendelea na kikao chake
hapo kesho.
0 comments:
Post a Comment