Saturday 2 May 2015

Akatazwa shule kwa kuvaa sketi ndefu


Msichana mmoja muislamu amekatazwa kuingia darasani huko shuleni kwao Ufaransa kwa sababu alikuwa amevalia sketi ndefu.
Msichana huyo mwenye umri wa 15 alifurushwa kutoka shuleni hapo na utawala wa shule hiyo uliodai amekiuka sheria za nchi hiyo zinazokataza kuonesha waziwazi ishara za kidini.
Kwa kawaida msichana huyo aitwae Sara, huvua hijabu yake anapokuwa maeneo ya shule kama inavyoamuriwa lakini hakudhani kwamba sketi yake ndefu pia ingemuweka matatani.
Ni mara ya pili Mkuu wa shule hiyo amemrudisha nyumbani mshichana huyo baada ya kumpa barua awapelekee wazazi wake inayoagiza kuwa abadilishiwe mavazi ndio aruhusiwe kuingia darasani. .
Inavyoelekea mgongano huu unatokana na tafsiri hiyo ya sheria ya 2004 inayozuia raia wa nchi hiyo kuonesha wazi wazi kuwa ni waumini wa dini fulani.
Msichana Sara anasema sketi yake si vazi la kidini, lakini utawala wa shule unatafrisi sketi hiyo yenye urefu wa hadi juu kidogo tu ya kisigino, kuwa vazi la kiislamu.
Share:

Mayweather Vs Pacquiao:Nani bingwa?


Japo tayari ni tajiri ,Mayweather ambae jina lake la utani ni Money, inatarajiwa atapokea zaidi ya dolla millioni $150m na Pacquiao kama millioni $100m.

Pacquiao yeye ametoka jamii ya kimaskini huko Ufilipino na kuna wakati katika maisha yake ya utotoni ambapo hata angelala njaa.
Sasa wa kuangalia kwenye TV kando, wengi wa mashabiki wa huko Marekani wangependa kuona makonde yakirushwa 'LIVE' kwa hivyo wamekubali kutoa ada ya hadi $100 kwa kichwa kushuhudia wakiwa 'LIVE' nje ya ulingo.
Wenye uchu wa kushuhudia pambano hilo 'LIVE' lakini hawajapata tiketi wako tayari kuzipata kwa walionanazo huku dau likiwa limepandishwa kwa kiwango atakacho muuzaji huyo mchuuzi.
Wafilipino kumshangilia Pacquiao
Wakati huo huo wito umetolewa kwa wakaazi wa kisiwa kimoja cha Philippines kwamba watumie kawi kwa kipimo kidogo ili kuihifadhi ndio waitumie kumwangalia katika runinga zao hapo Jumapili shujaa wao m-Filipino mwenzao , Manny Pacquiao (36) atakapokuwa akipambana na Mmarekani Floyd Mayweather (38) kwenye ulingo wa shindano la ndondi linalotajwa kuwa kubwa zaidi mnamo siku za hivi karibuni.
Wakaazi hao wameshauriwa na kampuni ya umeme nchini humo Palawan kuzima vifaa vya matumizi mengine ya nyumbani kama friji, kutotumia mashine za kufua nguo, wala kutopiga pasi ili kuhifadhi kawi hiyo siku hiyo itumike tu kuwashia Runinga zao.
Ushauri huo umetolewa kwani kisiwa hicho hukumbwa na upungufu wa umeme mara kwa mara, hivyo ni sharti wafuate maagizo hayo ili wasikose kushuhudia na kumshangilia kinara huyo wao ataeshiriki pambano hilo litakalo fanyika huko Las Vegas Jumamosi usiku saa za Marekani.
Ndilo pambano lililovutia fedha zaidi kuwahi kutokea.
Share:

Ugaidi:Shindano lasitishwa Ujerumani


Polisi wa Ujerumani wamefuta mashindano ya kimataifa ya kuendesha baiskeli yaliyotarajiwa kufanyika ijumaa katika mji wa Frankfurt, kwa hofu ya shambulio la kigaidi.
Mume na mke wamekamatwa baada ya kupatikana na silaha katika makaazi yao ikiwemo kemikeli ya kutengeneza mabomu.
Polisi wanashuku kwamba wawili hao walikua na mpango, wa kufanya mashambulizi wakati wa mashindano ya kuendesha baiskeli ambayo yamevutia wachezaji wengi duniani.
Mwanamume na mwanamke wa miaka 30 walikua wakifuatwa na majasusi kwa majuma mawili baada ya kutumia majina bandia wakati wakinunua kemikali inayoweza kutengeneza mabomu.
Polisi waliamua kuvamia makaazi yao baada ya mwanamume mmoja anayeaminika kuwa na uhisiano na makundi ya kisiilamu yenye misimamo mikali kuonekana nje ya nyumba yao mara kadhaa.
Polisi walipata mabomba ya kutega mabomu, silaha na kemikali.
Haijabainika iwap wawili hao walikua wakishirikiana na mtandao fulani.

Share:

Niqab yapigwa marufuku Congo Brazaville


Jamuhuri ya Congo- Brazaville imepiga marufuku vazi la Niqab katika maeneo ya umma.
Aidha mamlaka hiyo imewaonya raia wa kigeni ambao ni waislamu kusalia misikitini nyakati za usiku.
Serikali imetetea hatua yake na kusema inanuia kukabiliana na ugaidi.Maelfu ya wakimbizi wa Kiislamu kutoka nchi jirani ya jamhuri ya Afrika ya Kati wamekimbilia Congo- Brazzaville na wamekua wakipata hifadhi misikitini.
Nchi hiyo ina chini ya asilimia tano ya raia waumini wa kiisilamu.
Hii ndio nchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hii.
Share:

Polisi wafunguliwa mashtaka Baltimore


Meya wa mji wa Baltimore nchini Marekani Stephanie Rawlings-Blake, anasema kuwa amehusunishwa na kuvunjwa moyo baada ya polisi sita kushtakiwa, kufuatia kifo cha mwananamme mweusi Freddie Gray.
Polisi mmoja anakabiliwa na mashtaka ya mauaji huku wengine watano wakikabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia na kukamata kuliko kinyume cha sheria.
Tangazo hilo lilisababisha watu kusherehekea kwenye mji wa Baltimore lakini wengine hata hivyo waliiendelea kuandamana.
Wakili anayewakilisha chama cha polisi katika mji huo, alilaani kile alichokitaja kuwa kuharakisha katika kuwafungulia mashtaka polisi hao.
Rais wa Marekani Barack Obama anasema kuwa, ni muhimu uchunguzi kubainisha ukweli kuhusu kile kilichosababisha kifo cha bwana Gray.
Share:

Jeshi la Nigeria lawaokoa mabinti 293


Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.
Jeshi limeiambia BBC kwamba wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."

Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "
Share:

Matumaini ya manusura yadidimia Nepal


Matumaini yanadidimia nchini Napal ya kuwapata manusura zaidi baada ya kutokea kwa tetemeko baya la ardhi wiki moja iliyopita .
Msemaji wa wizara ya ndani ya nchi hiyo (Laxmi Prasad Dhakal) alisema, anafikiri kuwa hakuna uwezekano wa kupata manusura zaidi waliofukiwa chini ya vifusi.
Alisema kuwa idadi ya waliokufa sasa imezidi watu 6,600. Maelfu ya watu bado hawajulikani waliko wakiwemo raia zaidi ya 1000 kutoka nchi za ulaya.
Takriban helkopta ishirini zinashiriki katika jitihada za uokoaji katika vijiji vya mbali maeno yaliyo kaskazini mwa nchi.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.