Thursday 4 December 2014

Mtu azikwa ndani ya gari lake Nigeria.......source BBC


Katika siku za hivi karibuni picha za mtu ambaye alizikwa ndani ya gari aina ya Hummer SUV Jeep nchini Nigeria zimekuwa zikienea katika mitandao ya kijamii na kuzua mjadala miongoni mwa raia wengi wa taifa hilo.
Picha hizo zilitoka katika mtandao wa twitter wa msichana mmoja raia wa Kenya anayetumia jina @Sankorie katika mtandao wake ambaye alishangazwa na kusema kuwa wanaume wa Nigeria ni matajiri hadi wengine huzikwa ndani ya magari yenye thamani ya juu,swala ambalo haliwezi kufanyika nchini Kenya.
Je, unadhani ni kweli kwamba mtu anaweza kuzikwa ndani ya gari lake?
Share:

Ndege ya KDF yaanguka Somalia...............


Ndege ya jeshi la KDF nchini Kenya imeanguka katika eneo la Kismayu nchini Somali.
Ndege hiyo ilianguka siku ya Alhamisi mwendo wa saa tisa na robo ilipokuwa ikirudi Kenya baada ya kutekeleza mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somalia.
Kulingana na msemaji wa Jeshi kanali david Obonyo: ''Ndege ya KDF iliokuwa ikirudi nchini Kenya baada ya kufanya mashambulizi katika eneo la Jamaame kusini mwa Somali,ilikumbwa na matatizo ya kiufundi na kuanguka katika eneo la Kismayu .
Kanali Obonyo hata hivyo hakusema iwapo kulikuwa na majeruhi yoyote.
Jeshi la Kenya limesema kuwa ndege hiyo ilianguka kutokana na hitilafu za kimitambo baada ya kufanya oparesheni katika eneo la Jamaane Kusini mwa Somalia.
Hata hivyo baadhi ya mitandaoa iliyohusishwa na kundi la AL shabaab imechapisha habari kuwa AL shabaab wamedai kuwa ndio waliodungua ndege hiyo mwendo wa saa tisa Alasiri, Afrika Mashariki.
Msemaji wa kiksoi cha kivita cha Al shabaab Sheikh Abdi Azizi Abu Musab amenukuliwa akisema kuwa walishambulia ndege hiyo kwa kombora baada ya kulipua kijiji cha Bulaguduud.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa idhaa ya kisomali, ni vigumu kwa Al Shabaab kufanya shambulio kama hilo katika mji wa Kismayu kwa kuwa eneo hilo zima limefurika vikosi vya usalama vya AMISOM.
Mnamo mwaka wa 2012, majeshi ya Kenya yaliuteka mji wa bandari wa Kismayu, unaotazamiwa kuwa mji muhimu sana wa kiuchumi katika eneo zima la Somalia kutoka kwa wanamgombo hao wa Al shabaab.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.