Wednesday 6 May 2015

Saa za Apple zakosolewa

  
Kampuni ya Apple imekiri kwamba 'tattoo' za kifundo cha mkononi zinaweza kuathiri uangalizi wa moyo wa binaadamu katika saa za kampuni hiyo ,siku chache tu baada ya malalamishi kutoka kwa watu walio na 'tatoo' kwamba saa hizo aina ya Smartwatch haziweza kusema iwapo wako hai ama la.
Tatizo hilo limezuka kwa sababu saa hiyo hutumia miale ya rangi ya kijani inayong'ara ndani ya ngozi ili kubaini kiwango cha moyo unavyopiga.
Lakini kwa watu walio na 'tattoo' katika kifundo cha mkono ,wino unaotumika huzuia mwangaza huo wa kijani kibichi na hivyobasi kutoa matokeo mabaya.

Kampuni ya Apple hatahivyo haijatoa tamko lolote kuhusu habari hiyo lakini imearifu ukurasa wa usaidizi wa saa hiyo kubaini tatizo hilo.
Huku kampuni hiyo ikiwa imeliangazia swala la kiwango cha moyo wa binadaamu unavyopiga,na kusahau kwamba wateja wake wamekuwa wakilalamika kuhusu sensa ya ngozi katika saa hiyo,ambayo inachukua habari za iwapo saa hiyo imevuliwa na inawabidi watumiaji kuweka neno la siri.
Share:

Mzee amchoma mkewe wa miaka 16 Kenya


Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 aliyemchoma mkewe mwenye umri wa miaka 16 mjini Mandera kazkazini mashariki mwa Kenya amekamatwa.
Mke huyo aliyelazimishwa kuingia katika ndoa mwaka 2014 amelazwa katika hospitali kuu ya Mandera akiwa na majeraha mabaya ya kifuani pamoja na mikononi, kiongozi mmoja wa wanawake Ubah Gedi amethibitisha.
Mwanamke huyo sasa tayari amesafirishwa hadi jijini Nairobi kwa matibabu zaidi.
Ufichuaji huo uliofanywa kuhusu shambulizi hilo ni wa kushangaza kwa kuwa maswala mengi ya kijinsia Kazkazini mwa Kenya yameendelea bila kuripotiwa.
Share:

Mahakama yaruhusu Nkurunziza kuwania urais


Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .
Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.
Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali.
Share:

Wafghan 4 kunyongwa kwa mauaji


Jaji wa Mahakama ya Afghan amewahukumu wanaume wanne adhabu ya kifo kwa kumuua kwa kumshambulia mwanamke mmoja mjini Kabul.
Mwanamke huyo anayeitwa Farkhunda alipigwa hadi kufa na kundi la watu wenye hasira baada ya kutuhumiwa kimakosa kuchoma kitabu cha Koran.
Mwili wake ulichomwa mwoto. Watu wengine 49 wanaendelea na kesi, wakiwemo polisi 19 wanaotuhumiwa kwa kushindwa kuingilia kati kumwokoa mwanamke huyo.
Mauaji hayo yalisababisha hasira kutoka maeneo mbali mbali duniani ambayo pia yalisababisha maandamano nchini Afghanistan kupinga jinsi mwanamke huyo alivyotendewa.
Share:

Khan wa Bollywood kwenda jela miaka 5


Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa mjini Mumbai.
Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo.
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa jaji wa mahakama hiyo mwigizaji huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Share:

Milipuko yatokea jeshini Sudan.


Kumetokea milipuko katika maeno ya jeshi nje ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Wakazi katika wa eneo la Omdurman la ukanda wa magharibi wa mto Nile wamesema mapema usiku wa manane walisikia mlipuko wa kwanza na baadae makombora ya kutungulia ndege kutoka upande wa majeshi ya serikali.
Msemaji wa serikali ya Sudan amethibitisha askari wake walifanya mashambulizi na kulenga kundi wasilolifahamu lakini akakanusha kikosi chake na vifaa vyao vya kijeshi kushambuliwa.
Miaka mitatu iliyopita Sudan iilituhumu Israeli kwa kufanya mashambulizi ya anga kwenye kiwanda cha silaha mjini Khartoum ambapo pia kuna taarifa kuwa ndege za Israel pia zilifanya mashambulizi kwenye misafara ya silaha zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Gaza.
Israel haijatoa taarifa zozote rasmi kujibu shutuma hizo.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.