Sunday 14 December 2014

Vikosi vya Libya vyatibua shambulizi.


Wapiganaji wazidi kushambuliana nchini Libya tangu kuanguka kwa utawala wa Muamar Gadaff....

Shambulizi lililolenga kituo muhimu cha mafuta mashariki mwa Libya halikufua dafu kutokana na mashambulizi ya angani yaliotekelezwa na vikosi vya serikali vinavyotambuliwa kimataifa.
Kamanda mmoja wa jeshi la wanahewa anasema kuwa mashambulizi ya angani yaliwalenga watu wenye silaha waliokuwa wakisonga mbele katika kituo cha mafuta cha Al-Sidra ambapo watu wengi waliuawa.

Zaidi ya miaka mitatu tangu kuanguka kwa utawala wa kanali Muamar Gadaffi serikali hasimu bado zinapigania madaraka nchini Libya.
Share:

Jenerali aliyempinga Museveni arudi UG........























Jenerali Sejusa aliyeitoroka uagnda baada ya kutofautiana na rais Musevenei hadharani

Mwanajeshi wa Uganda ambaye alitofautiana hadharani na rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni mwaka uliopita amerejea nchini Uganda bila kutarajiwa kutoka nchini Uingereza ambapo alikuwa amekimbilia uhamishoni.
Jenerali David Sejusa aliitoroka Uganda baada ya kumshutumu rais Museveni kwa kujaribu kubuni familia ya kifalme akitaka kumkabidhi uongozi mwanawe wa kiume.
Sejusa pia alidai kuwa kulikuwa na njama ya kuwaua watu fulani katika serikali na jeshini ambao walikuwa wakipinga mpango huo.





















Rais Museveni anayedaiwa kumtayarisha mwanawe ili kuchukua utawala wa Uganda

Alipowasili mjini kampala Jenerali Sejuse alikutana na mkuu wa ujajusi ambapo pia aliwaambia waandishi wa habari kuwa rais Museveni alifahamu kuhusu kurejea kwake.
Share:

Zaidi ya abiria 100 wazama DRC.....















Ripoti kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinaeleza kuwa watu zaidi ya 100 wanafikiriwa kuwa wamekufa katika ajali ya feri.
Jahazi iliyojaa abiria imezama katika Ziwa Tanganyika kusini-mashariki mwa nchi siku ya Alkhamisi.
Waziri wa usafiri wa jimbo hilo la Katanga, Laurent Sumba Kahozi), aliliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa miili kama 129 imepatikana.
Inaarifiwa watu 232 walinusurika.
Ajali hiyo ilitokea Alhamisi usiku kaskazini mwa jimbo la Katanga baina ya miji ya Moba na Kalemie.
Waandishi wa habari wanasema ajali kama hizo zinatokea kawaida kwa sababu feri mara nyingi zinakuwa zimejaa mno.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.