Wednesday 20 May 2015

Somalia:Majeshi ya Burundi kuondolewa?


Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amesema ikiwa hatua ya kuondoa majeshi ya Burundi itafanyika nchini Somalia itaathiri mapambano dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.

Mwanzoni mwa juma hili Marekani ilitangaza kupunguza kiasi cha pesa inachotoa kwa majeshi ya Burundi baada ya shutuma kuwa jeshi hilo limejihusisha katika vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu wakati wakizima vurugu zilizojitokeza katika jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza liliposhindwa.
Umoja wa mataifa ya Afrika AU, nayo imesita kupeleka kundi jingine la wanajeshi wa Burundi nchini Somalia.

Lakini Kay, ameiambia BBC kuwa majeshi ya Umoja wa Afrika yanahitaji msaada kuweza kupambana na Al Shabaab.
Aidha Kay ametahadharisha kuongezeka kwa mahitaji ya kibinaadamu nchini Somalia na kutoa wito wa jumuia ya kimataifa kuendelea kupeleka misaada nchini humo.
Share:

Burundi:Nkurunziza ahairisha uchaguzi..


Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi .
Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AFP kuwa kufuatia jaribio la mapinduzi juma lililopita na vurugu zilizofuatia ni bora kuahirisha uchaguzi huo kwa muda.
''Uchaguzi huo wa ubunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Mei lakini sasa inatubidi kuihairisha ili kuwasikiza washirika wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo pia inatumia muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya upinzani.'' alisema Nyamitwe.
Hadi kufikia sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanywa Juni tarehe 26 haijabadilika.
''Subiri tu'' Nyamitwe aliwaambia waandishi wa habari.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba amesema kuwa tayari rais Nkurunziza ametia sahihi amri hiyo ya kuhairishwa kwa uchaguzi.
Umoja wa mataifa ya bara Ulaya EU, na Umoja wa mataifa ya Afrika AU, yametoa wito kwa uchaguzi huo uliokumbwa na utata mkubwa uhairishwe ilikutoa fursa kwa mazungumzo ya upatanishi kuendelea .
Hapo jana Rais wa Afrika Kusini alitilia pondo hoja hiyo ya kuahirisha uchaguzi akisema ni bora uchaguzi huo uliopangwa ''uhairishwe''.
Takriban watu 20 wameuawa kufuatia makabiliano baina ya polisi na waandamani katika mji mkuu wa Bujumbura kilele ikiwa ni juma lililopita makamanda waasi walipotangaza jaribio la mapinduzi rais
Nkurunziza akiwa mjini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda uliolenga kutatua mzozo wa kisiasa nchini mwake.

Wapinzani wa rais Nkurunziza wanasema kuwa kutangazwa kwake nia ya kuwania muhula wa tatu unakiuka sheria na makubaliano ya amani ya mwaka wa 2006 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 13.
Nkurunzizakwa upande wake anashikilia kukutu kuwa ana haki ya kuwania muhula mwengine kwani muhula wa kwanza hakuchaguliwa na wanainchi bali wabunge.
Takriban watu laki moja wamekimbilia mataifa jirani wakihofia kutibuka upya kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Share:

Obama ajiunga na Twitter.


Rais wa Marekani Barack Obama amejiunga na mtandao wa twitter, ikulu ya White House imethibitisha.
Akitumia anuani @POTUS (President Of The United States) Obama tayari amewavutia wafuasi 1.7 milioni moja nukta saba.
"Hamjambo, Twitter!Ni Barack.
Kwa hakika baada ya miaka 6 hatimaye wameniruhusu kujiunga na mtandao wa Twitter''Obama alisema kwenye ujumbe wake wa kwanza.
Obama alikuwa na anuani tofauti inayomilikiwa na wahudumu wa ikulu yake .Anuani hiyo inawafuasi Milioni 59.3m.
Anuani hiyo @BarackObama ilizinduliwa mwaka wa 2007, na kila akituma ujumbe anaanza na BO.
" Anuani ya @POTUS itamruhusu Obama kuwasiliana moja kwa moja na mamilioni ya wafuasi wake'' ilisema taarifa ya White House .

"Rais Obama angependa serikali yake iwe ya wazi @POTUS na hii ndio jukwaa mwafaka ya mazungumzo."
Kwa sasa rais Obama amewafuata watu 65 wakiwemo rais wa zamani wa Marekani ,Bill Clinton, George Bush na mkewe mwenye anuani ya kipekee @FLOTUS.
Hata hivyo hajamfuata Hillary Clinton wala waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
Tayari mawasiliano yake na Bill Clinton yamezua mjadala Clinton akimtania kwa kumuuliza iwapo ataondoka na anuani hiyo atakapo achia ngazi naye akam
Share:

Kinyesi cha panya na mkojo ndani ya vipodozi..


Je wewe ni mnunuzi wa bidhaa za urembo ?
Tahadhari .
Kinyesi cha panya na mkojo wa binadamu ni baadhi ya viungo vinavyotumika kutengeza bidhaa ghushi za urembo.
Utafiti wa bidhaa za urembo zinazouzwa kwa njia ya mtandao nchini Uingereza umebaini kuwa bidhaa hizo zina tengezwa kwa njia isiyofata maadili na kulinda afya ya binadamu.
Utafitri huo uliochunguza bidhaa za urembo kama vile vipodozi marashi na mafuta ya kujipaka iligundua kuwa zinaongezwa madini ya sumu kama vile arsenic.
Kwa mujibu wa Polisi waliotekeleza uchunguzi huo, mfumuko wa bei ya bidhaa kwa njia za kielektroniki kumechangia pakubwa ongezeko la mauzo ya bidhaa gushi.
''ni vigumu sana kubaini uhalali wa bidhaa haswa unaponunua kwa njia ya kielektroniki kwa sababu unachokiona hapo mtandaoni ni picha tu ya bidhaa halali''
''sasa bidhaa hiyo inapokufikia huwa tayari umekwisha lipia na ni vigumu sana kwako kurejesha bidhaa hizo pindi unapokuwa hujaridhia ubora wake'' alisema afisa aliyesimamia uchunguzi huo.

Bidhaa za kielektroniki zinazopendelewa na wafanyibiashara walaghai ni kama zile zile zinazosokota nywele na pia zingine zinazotumika kwa ususi.
Hata hivyo bidhaa hizo haziwezi kuhimili matumizi ya muda mrefu na hivyo zinahatarisha maisha ya watumizi kutokana na hatari kulipuka.
Isitoshe Polisi wanasema kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa marashi ghushi yanayouzwa London yanajumuisha sumu aina ya Cyanide na mkojo wa binadamu.
Vipodozi vimepatikana na sumu aina ya arsenic madini yenye sumu ya zebaki na risasi .
Vipodozi hivyo vinaweza kusababisha kujikuna,vipele visivyokwisha na maradhi mengine ya ngozi.
Bi Maria Woodall, anayeongoza kitengo cha uchunguzi wa hati miliki ya bidhaa alionya kuwa watu wengi hawafahamu madhara ya kutumia bidhaa ghushi.
Share:

Magari milioni 34,kurejeshwa viwandani.


Takriban magari milioni thelathini na nne 34,000,000 yanatarajiwa kurejeshwa viwandani nchini Marekani kufuatia hitilafu ya kiufundi kwenye mifuko ya hewa ya usalama.
Kampuni inayotengeneza mifuko ya hewa ya usalama ya magari inachukua hatua hiyo baada ya malalamiko kuwa hitilafu ya muundo wake imesababisha vifo vya watu wapatao watano.
Tukio hili la urejeshwaji wa magari viwandani kutokana na kasoro za kiufundi ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani.
Kampuni ya kutengeneza vifaa vya magari ya Japan, Takata, imekiri mifuko ya hewa kulinda usalama wa watumiaji wa magari kuwa na kasoro.
Baadhi ya mifuko hiyo ya hewa imepasuka kwa nguvu kupita kiasi na kusababisha kurusha vipande vya chuma kwa madereva na abiria wanaokaa viti vya mbele.
Waziri wa Usafirishaji wa Marekani, Anthony Foxx, ametangaza kurejeshwa kwa magari yenye hitilafu ya mfumo huo kote nchini humo.
Bwana Foxx amesema urejeshwaji wa magari hayo ni kazi kubwa.
Tangazo hilo limetolewa na Utawala wa usalama wa taifa nchini Marekani katika barabara Kuu baada ya mazungumzo marefu na kampuni ya Takata.
Magari yanayorejeshwa yanahusu kampuni kumi na moja za kutengeneza magari zikiwemo za Honda, Toyota na Nissan.
Urejeshwaji viwandani kwa magari mapya hufanyika baada ya kugundulika hitilafu lolote la kiufundi linaloweza kuhatarisha usalama wa watumiaji wa magari hayo.
Share:

Jinamizi la mihadarati G Bissau awamu ya {2}


Likijulikana kama taifa la kwanza lililotambulika kwa ulanguzi wa mihadarati barani Afrika ,taifa la Guinea-Bissau limekuwa kitovu cha kimataifa cha biashara ya mihadarati kwa karibia muongo mmoja.
Ikiwa ni taifa lililokumbwa na mapinduzi ya kijeshi pamoja na ufukara,hutumiwa na walanguzi wa mihadarati kutoka Marekani Kusini kama njia ya kusafirisha dawa aina ya Coccaine hadi Ulaya.
'Hooked' kama inavyojulikana ni riwaya ya athari zinazosababishwa na biashara hiyo kwa binaadamu.
Share:

Poroshenko amnyooshea kidole Putin


Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameiambia BBC kuwa hamuamini kiongozi wa Urusi Vladimir Putin katika harakati za kuleta amani Mashariki mwa Ukraine.
Poroshenko anasema anahofia kwamba huenda kukawa na kutokuelewana kati ya mataifa hayo mawili.

Vladimir Putin
Hata hivyo ameielezea hali hiyo kuwa ni vita kamili kati ya nchi hizo.
Ameongeza kuwa awali waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry alifanya mazungumzo na kiongozi huyo kabla ya mazungumzo yao na rais wa Urusi Putin.
Share:

Wahamiaji waliokwama baharini waokolewa


Hatimaye Malaysia, Thailand na Indonesia zimekubaliana kuwapa makazi ya muda wahamiaji elfu saba waliokwama kwa siku kadhaa kwenye pwani ya mataifa hayo.
Hayo yameafikiwa na mawaziri wa mashauri ya kigeni wa mataifa hayo katika mkutano uliokuwa ukiendelea mjini Kuala Lumpur.
Mawaziri hao wamesema kuwa hatua hiyo ya muda ya kuwapa usaidizi wakimbizi hao,wanaotoka kwa kabila dogo la waislamu wa Rohingya kutoka Mynmar na Bangladesh,

kutaipa muda jamii ya kimataifa kuwatafutia sehemu ya kudumu, katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Mataifa hayo matatu ya Malaysia, Indonesia na Thailand, yamekosolewa sana kwa kukataa kuwaruhusu wahamiaji hao kuingia katika mataifa yao.
Mynmar ilikataa kuhudhuria mkutano huo na badala yake ikaandika barua ikielezea namna ya itakavyokabiliana na swala hilo la uhamiaji.
Msemaji wa shirikisho linalosimamia maswala ya wahamiaji ILO Jeff Labovitz ameiambia BBC kuwa hatua hii ya dharura itasaidia sana kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi ambao wamekuwa wakihangaika baharini bila chakula wala muundo msingi wa afya.
Wavuvi nchini Indonesia waliwaokoa zaidi ya wahamiaji 100 siku ya jumatano
Bado kuna hofu kuhusu usalama na afya ya wale waliokwama baharini ambao wanahitaji chakula na maji.

Maelfu ya raia kutoka Bangladesh na Waislamu jamii ya Rohingya wamekuwa katika bahari ya Andaman kwa majuma kadhaa sasa baada ya serikali ya Indonesia kubadili sheria ilikukabiliana na walanguzi wa watu kupitia bahari na ardhi yake.
Thailand,Malaysia na Indonesia zilikuwa zimekataa kuwaruhusu wamahiaji kuingia katika pwani za nchi zao
Huku hayo yakijiri, mashua moja iliyokuwa imewabeba wahamiaji mia nne, na ambayo ilikuwa imenyimwa ruhusa ya kutia nanga katika mataifa matatu ya bara Asia, sasa imewasili katika kisiwa cha Aceh, nchini Indonesia.
Mashua hiyo imekuwa baharini kwa miezi miwili unusu ikiwa imewabeba wahamiaji wa kiislamu wa kabila la Rohingya kutoka nchini Myanmar.
Mashua hiyo iliyopigwa picha na BBC juma lililopita ilipokuwa imekwama katika maji ya mipaka ya Thailand, ilikuwa na tatizo la Injini.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.