Thursday 27 November 2014

Saudia yawakataa mayaya wa Uganda........BBC



















Yaya wa Uganda aliyemtesa mtoto wa miezi 18

Mamlaka ya Saudia mjini Kampala imewaonya raia wake nchini Saudia dhidi ya kuwaajiri mayaya kutoka Uganda.
Onyo hilo linajiri baada ya kanda za video za CCTV kumuonyesha Jolly Tumuhiirwe,22,akimtesa mtoto wa miezi 18.
Bwana Haza Al-Otabi ,naibu wa ujumbe wa Saudi Arabia alinukuliwa na gazeti la kiingereza nchini saudi akiwaonya wawanchi wa taifa hilo dhidi kuwaajiri raia wa kigeni kutoka Uganda kuwa mayaya wao wenyewe.
''Uajiri ni sharti ufanyike kupitia makubaliano rasmi''bwana Al-Otaibi alisema.
Harakati ya gazeti la the monitor nchini Uganda kuwasiliana na afisa huyo ziligonga mwamba baada ya kudaiwa kuwa mikutanoni siku nzima.
Mtoto aliyechomwa na yaya aonyesha jareha alilopata

Inadaiwa kuwa Gazeti hilo la Saudia linasema kuwa bwana Al-Otaibi aliitoa kanda hiyo ya video kwa makusudi kwa kampuni zinazowaajiri wafanyikazi wa nje na ambazo mwezi mmoja uliopita ziliweka makubaliano na wizara ya wafanyikazi nchini Uganda ili kuwaajiri mayaya na madereva.
''Walioajiriwa kutoka Uganda hawatapewaza Viza kuingia nchini Saudia iwapo makubaliano hayo hayatafanyika kwa njia rasmi'',alinukuliwa akisema.
Katika mktaba huo kati ya Uganda na Saudia takriban viza 500 zilitarajiwa kupewa mayaya 400 wa Uganda na madereva 100 kufanya kazi nchini humo.
''Kumekuwa na matatizo na uajiri unaoshirikisha raia wa Uganda nchini Saudi Arabia.
Wengi ya mayaya wa Uganda wanaowasili Saudi Arabia huondoa mda mfupi baadaye na kushindwa kumaliza siku 20 n wafadhili wao'' mjumbe huyo alisema.
Amesema kuwa mayaya hao hulalamika kwa balozi yao kwamba wanahitaji haki zao za kifedha.Lakini Wafadhili wa saudia wanadai kwamba hawawezi kuwalipa kwa kuwa wameshindwa kufanya kazi kwa mwezi mmoja.
Lakini msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Uganda Fred Opolot ,amesema kuwa ubalozi wa Saudia haujatoa lalama yoyote kuwahusu.
Share:

Bi harusi wa miaka 14 ampa sumu mumewe....


Bi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.
Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.
Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.
Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho.
Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri.
Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5 mwezi Aprili,siku ambayo bwana Sani alifariki.
''Alisema kuwa panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia mahakama.Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u aliweka sumu hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana Sani.
Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani.
Jaji Mohammed Yahaya,katika mahakama ya Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa kesi mnamo mwezi Octoba ambapo alisomewa mashtaka.
Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.
Ushahidi wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo kwa mtoto huyo.
Jirani ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho kilichopikwa na Tasiu.''Nilipoletewa chakula hicho niliona vipande vipande vyeusi''aliiambia mahakama.
Alikula vipande vinne vya madonge vilivyotengezwa na maharagwe lakini hakupendelea ladha yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar pekee aliyeendelea kula.
Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.
Lakini alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho wamefariki kwa ghafla.
Viongozi wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi moja ya mauaji.
Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana na shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch.
Share:

Misikiti iliofungwa yafunguliwa Mombasa.........



Misikiti minne iliofungwa na maafisa wa polisi wiki iliopita baada ya kuchukuliwa na vijana wenye itikadi kali za kiislamu hatimaye imefunguliwa.
Hatua ya kuifungua misikiti hiyo ya Minaa,Sakina,Musa na Swafaa inajiri baada ya siku mbili za mazungumzo kati ya viongozi wakuu wa kiislamu,wataalam na uongozi wa kaunti ya Mombasa.
Maelezo ya mazungumzo hayo yalioandaliwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho na kaunti kamishna Nelson Marwa yamefanywa kuwa siri.
Kabla ya misikiti hiyo kufunguliwa ,viongozi wa kiislamu pamoja na wataalam walilazimika kuajiri kiongozi wa dini wa kila msikiti na kubuni kamati maalum ya kusimamia misikiti hiyo ya kisauni na majengo mjini Mombasa.





''Hatutaki wajisikie kana kwamba serikali ina wakandamiza.Tumewapa mda wa kuzungumza na kuamua kuhusu kamati za misikii hiyo na viongozi w dini ambao watakuwa wakisimamia ibada.Watatupatia majina na kufikia kesho{leo} misikiti hiyo itafunguliwa'',alisema bwana Marwa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya usalama kaunti ya Mombasa.
Duru zinaarifu kuwa miongoni mwa wale walioalikwa katika mazungumzo hayo ni viongozi wakuu wa kiislamu wakiwemo wawakilishi kutoka baraza kuu la waislamu nchini Kenya SUPKEM,barasa kuu la ushauri wa maswala ya kiislamu na baraza la maimamu na wahubiri nchini Kenya CIPK.
Misikiti hiyo ilifungwa wiki iliopita na maafisa wa usalama baada ya uvamizi katika Msikiti wa Musa pamoja na msako wa kuwanasa zaidi ya watu 250 ambao baadaye walishtakiwa kwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi.
Maafisa wa polisi pia walionyesha baadhi ya silaha na nakala ambazo wanasema zilipatikana katika msikiti huo.
Muda mchache baada ya kukamatwa kwao,magenge ya vijana walizua ghasia na kuanza kuwashambulia raia wasio kuwa na hatia katika vituo vitatu vya mabasi pamoja na makaazi katika eneo la kisauni.
Wakati wa ghasia hizo watu watatu walidungwa visu na kufariki huku wengine saba wakijeruhiwa vibaya.
Viongozi wa kiislamu mjini Mombasa na maeneo mengine ya nchi wamekuwa wakitaka kufunguliwa kwa misikiti hiyo ambayo imekuwa katikati ya utata kuhusu madai kwamba ilikuwa inatumiwa kuwafunza vijana itikadi kali mbali na kuhifadhi silaha kinyume na sheria.
Share:

Chanjo ya Ebola yaonesha matumaini...........BBC


Wanasayansi wamepongeza matokeo ya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, na kusema dawa zinaonesha kuwa salama na itasaidia mfumo wa kinga ya mwili kuvitambua virusi hivyo.
Watu 20 waliojitolea kutoka nchini Marekani, walipatiwa kinga maradhi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola.
Utafiti wa chanjo hiyo ya ebola kama huenda ikaokoa maisha wa maelfu walio hatarini kuambukizwa virusi hivyo. Dr Anton Fauci ni mkuu wa Taasisi ya Marekani ya magonjwa ya kuambukiza :
"Kwa upande wa usalama na uwezo wa kuleta matokeo mazuri nadhani tunaweza kuita majaribio haya ya chanjo haikufanikiwa. Japokuwa katika mkondo wa awali imeonyesha mafanikio makubwa." Amesema Fauci
Hata hivyo watafiti wanasema matokeo hayo sio uthibisho kwamba chanjo hiyo inafanya kazi lakini kama majaribio ya awali yamekuwa na mafanikio basi chanjo ya ebola itatolewa kwa maelfu ya wafanyakazi wa afya huko Afrika Magharibi kuanzia mwezi Januari mwakani.
Zaidi ya watu elfu tano mia tano wamefariki kutokana na kuambukizwa virusi vya ebola.Kwa sasa chanjo imekuwa ikifanyiwa utafiti na kampuni GlaxoSmithKline.
Dr Colin Brown ni mtaalamu wa magonjwa ambaye amepokea habari za chanjo hiiyo kama habari njema.
"Kwa vile suala la usalama limepewa umuhimu tunayo furaha kwamba hakuna madhara yaliyotokana na chanjo. Ambapo imeonyesha wagonjwa wa awali wapatao 20 wakuwa na tatizo lolote. Ninadhani tutarajie kuona itasaidia hasa kwa upande wa wafanyakazi wa afya kujilinda wakiwa kazini. " Alisema Bwana Brown
Share:

Baridi yagandisha breki za ndege Siberia.....


Abiria waliokuwa wanafanya safari na shirika ka ndege la Serbia walilazimika kushuka katika ndege hiyo na kuisukuma baada ya breki zake kuganda na kushindwa kuondoka.
Ndege hiyo ilikuwa inaanza kuruka kutoka katika mji wa Kirusi wa Igarka,lakini ilishindwa kusogea baada ya hali ya hewa kuwa -52C.
Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo idadi yao kubwa walikuwa wafanyakazi wa ndege hiyo waliombwa kutoa msaada wa dharura wa kuisukuma ndege hiyo kwa hofu ya kutowachelewesha endapo watasubiri msaada Zaidi.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Katekavia baada ya muda ilimudu kuendelea na safari zake na baadaye kutua salama katika mji wa Krasnoyarsk.kwa muujibu wa mashuhuda wa tukio hili kiwango cha baridikwa muujibu wa mashuhuda wa tukio hili ,wanaeleza kuwa kiwango cha baridi kilishuka hadi kufikia nyuzi joto 52, na kugandisha mfumo wa breki za ndege hiyo .
Mkuu wa kitengo cha huduma za ndege hiyo Oxana Gorbunova, anaeleza kwama abiria hawakulazimishwa kuisukuma ndege hiyo bali kwa hiyari waliamua kusaidia kuisukuma ,japokuwa kitendo hicho hakiruhusiwi kwakuwa kitendo hicho kinaweza kuathiri bodi ya nje ya ndege hiyo ,na wanasheria nao wanachunguza endapo uwanja wa ndege,shirika la ndege,wafanyakazi wa ndege ama abiria endapo wamevunja sheria za usalama wa anga.
Uwanja huo wa ndege unatumiwa na abiria takribani elfu moja kwa mwaka ,wengi wao hufanya kazi katika makampuni ya mafuta yanayomilikiwa na Urusi.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.