Monday 22 December 2014

Ndoto ya mjasiriamali


Hii ni Makala ya mwisho katika mfululizo wa ndoto ya Africa Makala ambayo ilikuwa ikiwaangazia wajasiriamali wa bara hili kwa muda wa wiki nane sasa.kila Makala ilikuwa na changamoto zake mwanzoni mwa biashara,hivyo muda wote wa mfululizo huu,ulikuwa na fursa ya kujifunza namna ya kuifikia ndoto yako, ama ndoto zao,na kama walifaulu,na inawezekanaje kwa wengine pia.
Binti huyu alionja ladha ya tasnia ya vyombo vya habari akiwa na umri mdogo wakati huo akimsindikiza babake.hata hivyo binti huyo amehitimu masomo ya sheria Kemi Adetiba baada ya muda mfupi alijitosa katika burudani na kuwika nchini mwake Nigeria nan chi zote za ukanda wa Jangwa la Sahara.
Leo hii tunapomzungumzi Adea Kemi, amekwaa tuzo ya uongozaji,mzalishaji na upigaji picha bora mjini Lagos, Nigeria Kemi anamiliki kampuni ya masuala ya filamu iitwayo K-Alpha Innovations. Na hapa anatumegea kidogo siri ya mafanikio katika biashara ya tasnia ya burudani.
Tuanze na suala ambalo liko katika vichwa vya watu wengi.ni kawaida kusikia katika tasnia ya burudani kinachogomba ni UNAMJUA NANI , wengine wana dhana kuwa ukimjua mtu ndio umefanikiwa na kumjua mtu hii inafanya kazi hata kama huna muingiliano na watu wengi.sio kweli.kama biashara zingine zote,inategemea juhudi zako binafsi changanya na uvumilivu.
Tuanze kuzitazama njia za mafanikio na kuitendea haki ndoto yako.

HATUA YA 1
Andaa mpango kazi amba unaainisha misingi ya awali kampuni ya kampuni ya kuandaa picha za video,ujuzi ulionao kama mzalishaji (producer) na pia mgango wa mauzo.Ambatanisha na orodha ya vitendea kazi unavyomiliki ambavyo unajua kuvitumia pia na bajeti ya kununua mifumo ya utendaji kazi kama ya uhariri wa picha za video,mashine za kurudufu kazi zako na taa.

HATUA YA 2
Andaa vyanzo vya mapato.pata orodha ya makato ya kodi mapema.

HATUA YA 3
Nunua vifaa vya kazi. Mzalishaji wa picha za video anapaswa kuwa na camera mbili hadi tatu ,microphone isotumia waya ,taa,komputa ya uhariri ambayo imewekewa mfumo wa final cut , ama adobe primier na lenzi tofauti tofauti kwa muujibu wa kamera ulizonazo.pia itategemea na vifaa ulivyonavyo kampuni ya uzalishaji picha za video inakadiriwa kuanza na mtaji wa dola za kimarekani 15,000 kwa kuwa na vyombo hitajika kwa ujumla wake .

HATUA YA 4
Tayarisha alama ya utambulisho ya kampuni yako,businesscard na mtandao ambao utakuwa ukionesha kazi zako ulizozifanya za video.

HATUA YA 5
Andaa kazi yako ya video yenye urefu wa dakika tatu hadi tano.tumia kamera nzuri lakini pia kuwa mbunifu katika namna ya upigaji picha zako kwa jicho la tofauti,nenda kapige picha nje ya eneo lako la kazi ili uongeze uhifadhi maktaba.

HATUA YA 6
Buni bei za bidhaa zako.hii ina maana utaanza kutoza bei kwa huduma kuanzi saa moja ama kwa bidhaa.toa huduma ya kazi iliyokamilika,ikiwezekana fanya video ya familia ya mteja na kuzirudufu.

HATUA YA SABA
Weka mfumo wa utembezaji kazi zako za video gurudumu litakalo muwezesha mteja kupitia kazi zako bila usumbufu ,lazima uwe na mtandao na wateja wako, na uwasambazie kadi zenye maelezo ya kazi zako na watakavyokufikia yakiwemo mawasiliano.picha,michezo ya kuigiza,kwa wapenzi wa huduma zako kwa mtindo wa DVD.

Share:

Kwa wivu,Mume amjeruhi mkewe kwa shoka.






















Mama mwenye watoto watatu anapata matibabu hospitalini nchini Malaysia baada ya mumewe kuvamia mikono yake na miguu nakumcharanga kwa shoka la kucharangia nyama,na baadaye mwanamume huyo kujinyonga .
Mama huyo anatajwa kama K Menaga,amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Kluang upande wa kusini mwa jimbo la Johor baada ya shambulio hilo hatari lililotokea mapema mwezi huu.
Ingawa taarifa kutoka hospitalini hapo zinaarifu kuwa mama huyo ameshatolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya hali yake kuendelea vyema,na amelazwa katika wodi ya wagonjwa wa kawaida.
Inasemekana mume wa mwanamke huyo ana umri wa miaka 47 na asiye na kazi maalumu baada ya kumcharanga mkewe na kuona damu tele imtokayo mkewe, aliamua kunywa sumu na baadaye kujinyonga .Mke wa bwana huyo alikuwa akifanya kazi ya kuosha vyombo huko Singapore kwa muda wa miaka 15 sasa .
Majirani wanaeleza kuwa familia ya mwanamke huyo ilikuwa inaishi kwa kutegemea mshahara wa mwanamke huyo, wakati mumewe alikuwa hana chanzo cha mapato.Na mwanamke huyo alikuwa na utaratibu wa kurejea nyumbani kwake mara moja kwa mwezi kuwaona watoto wake akiwemo mama mkwe wake.
Mashuhuda hao wanasema kwamba,kila mwanamke huyo arejeapo kutoka kibaruani, mumewe alikuwa akimshutumu kwa kukosa uaminifu na kumshutumu kuwa ana bwana ambaye humrejesha kutoka Singapore,nao polisi wameeleza kuwa matokeo ya tukio hilo ni wivu wa mwanamume huyo,na baada ya tukio hilo kaka wa mwanamke huyo anaeleza kuwa watoto wa mwanamke huyo wamechukuliwa na jamaa zao kwa matunzo.
Share:

Rais Kikwete azungumza na wazee.


Rais Jakaya Kikwete ametengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kupitia hotuba aliyotoa kuzungumzia kashfa ya upotevu wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa na vyombo vingine.
Uchunguzi uliofanywa na kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku chache zilizopita Profesa Tibaijuja aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Hata hivyo Rais Kikwete hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila mtuhumiwa.
Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali ya TANESCO.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.