Saturday 22 November 2014

Waliofanya shambulio la Mandera wasakwa...... BBC


Maiti za watu waliouliwa na al-Shabaab Jumamosi asubuhi nje ya mji wa Mandera, Kenya, karibu na mpaka wa Somalia, zilipelekwa na wanajeshi hadi mjini humo.
Serikali ilikuwa inajitayarisha kusafirisha miili hiyo hadi mji mkuu, Nairobi.
Basi lililokuwa limebeba abiria 60 lilitekwa nyara alfajiri na abiria 28 walipigwa risasi na kuuwawa.
Wengi waliouwawa ni kutoka maeneo mengine ya Kenya ambao wakifanya kazi Mandera.
Inasemekana kuwa wengi wao walikuwa waalimu na wafanyakazi wa wizara ya afya ambao walikuwa wanarudi nyumbani kuwa na familia zao wakati wa Noeli.
Msemaji wa wapiganaji wa Somalia, al-Shabaab, alidai kuwa walihusika na shambulio hilo.

Wanajeshi na polisi wametumwa huko kwenda kuwasaka wale waliohusika na shambulio hilo lakini hakuna taarifa kuwa wamekamatwa.
Share:

RAIS KIKWETE ATOLEWA NYUZI KATIKA MSHONO, AFYA YAKE YAZIDI KUIMARIKA......Global Publisher




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi.

























Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri.
Share:

BASI LA ABIRIA LAVAMIWA KENYA, WATU 28 WAUAWA.......source Global Publisher


 Habari kutoka Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya zinasema kuwa, abiria 28 wameuawa na wengine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuvamia basi walimokuwa wakisafiria leo alfajiri.
Habari zaidi zinasema wavamizi hao huenda ni wanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabab. Mashuhuda wa tukio hilo wanasema wavamizi hao walikuwa wa asili ya kisomali na waliwaua abiria ambao si Waislamu. Jambo hilo linalenga kuzusha vita vya kidini nchini Kenya.

Ikiwa itathibitika kuwa al-shabab ndio waliohusika na hujuma hiyo,  hilo litakuwa shambulizi baya zaidi la kundi hilo kutokea katika miezi ya hivi karibuni. Polisi ya Kenya imekataa kutoa taarifa kuhusiana na tukio hilo na kusisitiza kuwa, itatoa maelezo punde baada ya kuchunguza kadhia hiyo.
Share:

Al Shabaab lakiri kutekeleza shambulizi......source BBC


Kundi la Al Shabaab nchini Somali linasema kuwa limefanya mashambulizi ya abiria 28 katika basi moja kazkazini mashariki mwa kenya.
Basi hilo ambalo lilikuwa likiwabeba abiria 60 lilitekwa katika jimbo la mandera lilipokuwa likelekea mjini Nairobi.
Abiria mmoja ambaye alinusurika ameiambia BBC vile raia wasio wa Somali walitengwa na wengine na wale ambao hawakuweza kusoma aya ya Quran walipigwa risasi kwa karibu.
Katika taarifa yake al Shabaab limesema kuwa mashambulizi hayo ni ya kulipiza kisasi mauaji ya waislamu huko Mombasa yaliotekelezwa na vikosi vya usalama vya kenya.

Kenya imekumbwa na misururu ya mashambulizi ya risasi na mabomu yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la Alshabaa tangu vikosi vyake viingie nchini Somali
Share:

Ebola:Fuo za bahari kufungwa Liberia....source BBC


Polisi nchini Liberia wametangaza kuwa watafunga fuko zote za bahari kuanzia tarehe 29 mwezi Novemba hadi pale taifa hilo litakapo tangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umemalizwa..
Tarehe hiyo itakuwa ni siku ya taifa la Liberia ya kuadhimisha kuzaliwa kwa raisi aliyeiongoza Liberia kwa miaka mingi William Tubman.
Polisi wanasema kuwa yeyote atakayetumia fuo hizo za bahari atakuwa amekiuka amri hiyo na atachukuliwa hatua za kisheria.
Polisi pia wamepiga marufuku mikutano yote ya umma isipokuwa ya kisiasa.
Karibu watu 3000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.