Wednesday 26 November 2014

Lawama kwa viongozi wa kiisilamu Kenya.............BBC


Baraza makanisa nchini Kenya(NCCK) limewalaumu vongozi wa kiislamu na serikali kushindwa kuzuia mashambulizi dhidi ya wakristu.
Wakizungumzia mauaji yanayosemekana kutekelezwa na kundi la Al-Shabaab na kuwaua wakristu 28 Jumamosi asubuhi.
Baraza hilo limesema kuwa halitafanya mazungumzo mengine na viongozi wa dini ya kiislamu kwa sababu wameshindwa kuwathibiti waumini wao ambao NCCK inadai kuwa wamekuwa wakiwashambulia wakristu kwa maeneo ya ibada na kwingineko.
Kwa siku nyingi baraza la makanisa limekuwa likichukua msimamo wa kadri kunapotokea mashambulizi nchini Kenya ama kwa jumla kuhusu suala la usalama.
Ila leo walikuwa na msimamo mkali sana kuhusiana na mauaji yaliyotokea Mandera wakalaumu kwana viongozi wa kiislamu kwa kutokuwa wakakmavu kuwashauri waumini wao.
Huyu hapa katibu Mkuu wa baraza hilo Peter Karanja alisema kuwa wamekuwa na mikutano mingi na viongozi wa dii ya kiislamu lakini kumekuwa na mshambulizi mengi yanyowalenga wakristu
Japokuwa walionyesha kukerwa na tukio la Mandera, viongozi hao wamesema kuwa serikali na viongozi wa kiislamu hawajashughulikia tatizo la vijana wanaoshikilia mismamo mikali ya dini katika maeneo ya Pwani na Kaskazini ya nchini ambao wamekuwa hatari kwa usalama




Hata hivyo viongozi wa kiislamu hawajachukulia kwa wepesi sula hilo. Dr Hassan Kinyua ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya kidini katika baraza kuu la waislamu(SUPKEM) anataka NCCK iendelee kufanya mazungumzo na SUPKEM.
Ameongeza kuwa ni makosa kila mara kuhusisha suala la ugaidi na dini ya kiislamu
Lakini viongozi hao wanapoishambulia serikali hususan vikosi vya usalama kwa kulegea katika vita dhidi ya ugaidi Rais uhuru Kenyatta amewatetea maafisa wa usalama akisema kuwa suala la usalama ni la wakenya wote.
Na hata watu wanapotaka wakuu wa usalama wajiuzulu Rais Uhuru anasema vikosi vya usalama havitavumilia dini kutumia majengo ya ibada kuendeleza ugaidi
Hapo jana makundi kadhaa ya kutetea haki za binadamu yaliandamana yakimtaka Rais Uhuru Kenyatta kuwaachisha kazi wakuu wa uslama kwa kushindwa kuzuia mashmbulizi dhidi ya wakenya.
Kumekuwa na mashmbulizi mengi nchini Kenya tangu jeshi la Kenya liingie Somalia kuwakabili wanamgambo wa Al Shabaab ambao wanadhaniwa kuwa wamekuwa wakitekeleza mashambulizi nchini Kenya na kutorokea Somalia.
Baadhi ya mashambulizi makubwa kuwahi kufanyika lile la Westgate jijini Nairobi ambako zaidi ya watu sitini waliuawa na huko Mpeketoni katika pwani ya Kenya.
Serikali ya Kenya imesisitiza kuwa jeshi la Kenya liliwaua zaidi ya wapiganaji 100 wa Al-shabaab wanaodaiwa kuhusika na mauji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi kutoka Mandera kuelekea katika sehemu nyingi za nchini ila baadhi wananchi wanatilia shaka kauli hiyo.
Share:

Kauli ya Bi Maria Nyerere kuhusu Escrow........BBC


Mjane wa Hayati Baba wa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Maria Nyerere, amezungumzia sakata ya ESCROW iliyozungumziwa bungeni mjini Dodoma na kupendekeza ripoti ya mgogoro huo wa IPTL kujadiliwa kwa uwazi ili kupata ufumbuzi na wahusika kuwajibishwa kwa manufaa ya umaa.
Share:

Vyuo vya Tanzania vyafeli katika mjadala........ BBC


Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania ambavyo vilishiriki katika mashindano ya mjadala wa Afrika kuhusu Sheria za kimataifa za haki za kibinaadamu yalioandaliwa na kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC vimeshindwa kufika katika raundi ya mwisho.
Badala yake vyuo hivyo viliondolewa katika raundi za mapema ambapo mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa mjini Arusha.
Kulingana na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, vyuo vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo kikuu cha Zanzibar.
Katika raundi ya mwisho ya mashindano hayo yaliofanyika mwishoni mwa wiki katika mahakama maalum ya kimataifa inayochunguza mauaji ya kimbari nchini Rwanda ICTR mjini Arusha,chuo cha Strathmore University kutoka Kenya kiliibuka mshindi na kufuatiwa na chuo cha Christian University kutoka Uganda huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka Zimbabwe kikiibuka mshindi wa spika bora.
Raundi ya mwisho ya mjadala huo ilisimamiwa na jaji wa mahakama hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji wa mahakama ya haki katika Afrika mashariki Fanstin Ntezilyayo,John Joseph Wamwara na Mutsa mangezi kutoka ICRC.
Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi kwa washindi aliyapongeza mashindano hayo kama kifaa cha kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya sheria na kwamba itasaidia kuimarisha maono yao katika siku za usoni.
Share:

Kashfa ya ESCROW vigogo watajwa TZ..........

Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.
Sakata hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu umezusha mjadala mzito katika bunge la Tanzania.
Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya viongozi.
Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.