Tuesday 16 December 2014

Tahadhari:'Hatari za urembo bandia'.

Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa
Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.
Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii
Kwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''..........>>>INGIA HAPA<<<
Share:

Mtoto amuibia nyanyake na kuwashangaza wengi.


Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 aliiba maelfu ya dola kutoka kwa nyanyake na kisha kukodi taxi kumpeleka eneo la mbali kukutana na kijana mwenye umri wa miaka 16 ambaye walikuwa wakiongea naye tu kupitia mtandao wa Internet.
Wawili hao hawajawahi kuonana hata siku moja.
Msichana huyo Alexis Waller yuko salama na bukheri wa afya na hatakabiliwa na kesi yoyote baada ya kitendo chake ambacho kimewashangaza wengi.
Maafisa wanasema Waller aliiba dola elfu kumi kutoka kwa chumba cha nyanyake katika mji wa Bryant, jimbo la Arkansas.
Baada ya kitendo chake cha wizi, msichana huyo alikodisha taxi na kumtaka dereva kumpeleka kwa kijana huyo katika jimbo la Florida.
"nilisema nitaka kwenda mjini Jacksonville, Florida," Waller aliambia shirika la habari la KARK. "kijana huyo aliniuliza kama nina pesa na nikamwambia ndio. ''
Gharama ya safari yake ilikuwa dola 1,300.
Jarida la Arkansas Democrat-Gazette linasema kuwa Waller alikuwa tayari amesafiri umbali wa maili 500 kuelekea kwa kijana huyo lakini polisi waliweza kuwasiliana na dereva wa taxi hio na kuwafuata.
Wazazi wake walisema Waller aliwakasirisha sana lakini ni afunei kwao kwani mtoto wao aliweza kurejea nyumbani
Share:

Alipanda kreni kumposa mpenzi.Yalomkuta?


Mwanamume mmoja raia wa udachi amejikuta akikimbilia usalama wake baada ya jaribio la kutaka kumposa mpenzi wake kwa mbwembwe kwenda mrama.
Mtu huyo ambaye hakutajwa kwa jina anayeishi mjini Ijsselstein alikodisha 'kreni' au Crane na kuipanda akipanga kwamba kreni hilo imtoe chini na kumpanidhs hadi dirishani mwa mpenzi wake ambapo angemchezea wimbo na kisha kumposa.
Badala yake yaliyomkuta hakuyatarajia kabisa.Kreni hiyo ilianguka chini na kupita dirishani kwa mpenzi wake huku ikiangukia nyumba za majirani.
Mwanamume huyo alilazimika kukimbilia usalama wake na hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo lililowaacha wengi wakiangua kicheko.
Kwa mujibu wa jarida la Algemeen Dagblad, mpenzi wake mwanamume huyo alimkubali na kusema yuko radhi kuolewa naye licha ya tukio hilo.
Baada ya kuongea na polisi, wawili hao walisafiri kwenda mjini Paris Ufaransa kusherehekea.
Kreni hio ilianguka tena kwa mara ya pili ilipokuwa inainuliwa na hata kuharibu zaidi nyumba za majirani. Meya wa mji huo, amezomewa na wengi baada ya eneo hilo kusemekana kutokuwa salama.
Share:

Roboti zapata ajira mgahawani China


Hadimu hivi karibuni huenda wakakosa ajira maana roboti zimezinduka
Mgahawa mmoja nchini China umeanza kutumia Roboti badala ya kuwaajiri hadimu au wafanyakazi wa hotelini kuwapakulia chakula na vinywaji wageni.
Share:

Wafungwa Philippines waponda raha.


Polisi mjini Manila wamevamia gereza moja na kuushangaza umma wa Philippines baada ya kung'amua maisha ya anasa yanayoendelea ndani ya gereza hilo kwa kikundi cha baadhi ywa wafungwa wenye upendeleo wa kipekee.
Uvamizi huo umefanywa katika gereza hilo la Bilibid lenye wafungwa wengi nchini humo kufuatia taarifa kwamba mtandao wa dawa za kulevya nchini humo unafanya kazi katika gereza hilo kwa njia za panya.

Baada ya uvamizi huo maafisa wa polisi walikuta wafungwa hao wakiwa wamefunga viyoyozi,mabafu ya kuogea ya kisasa yenye marumaru na kupambwa kwa mawe ya thamani,makasha ya kuhifadhia fedha,saa za gharama na fedha lukuki.
Wafungwa hao walifanikiwa pia kununua pombe kali za gharama kubwa ,komputa na hata simu za kisasa za gharama kubwa.kufuatia tukio hilo serikali ya Philippine imeahidi kufanya uchunguzi wa kina.
Share:

''Niliokoa Kenya 2013'' asema Moreno Ocampo.


Kiongozi wa zamani wa mashitaka katika mahakama ya jinai ya ICC, ameteta uamuzi wake wa kumshitaki Rais Uhuru Kenyatta licha ya kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Bwana Luis Moreno Ocampo anasema kua mashitaka hayo dhidi ya Uhuru yalizuia ghasia kutokea tena katika uchaguzi wa mwaka 2013.
Kenyatta alishinda uchaguzi huo baada ya kugombea kwa tiketi ya chama cha TNA, huku akiituhumu mahakama hiyo kwa kuingilia maswala ya ndani ya Kenya.
Alishtakiwa kwa kosa la kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007.
Wiki jana mrithi wa Ocampo, Fatou Bensouda, alitupilia mbali kesi hio dhidi ya Kenyatta akisema amekosa kupata ushahidi wa kutosha kuthibitisha mashitaka dhidi ya Uhuru.
Kenyatta hata hivyo tangu mwanzoni alikanusha madai ya kutenda uhalifu dhidi ya Binadamu.
Alikuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kuwahi kufikishwa katika mahakama hio ambayo wengi wanasema ni ya kisiasa.
Watu 1,200 walifariki na wengine 600,000 kutoroka makwao katika ghasia hizo ambazo ndio mbaya zaidi kuwahi kushuhdiwa nchini humo tangu ijinyakulie uhuru.
Ocampo aliambia BBC kwamba kushitakiwa kwa Uhuru kulizuia ghasia kutokea tena nchini Kenya, wakati wa uchaguzi mwaka 2013. ''Mahakama ya ICC ilibadilisha siasa za Kenya, '' alisema Ocampo.
Wiki jana Rais was Uganda Yoweri Museveni alirejelea wito wake kwa mataifa ya Afrika kujiondoa ICC akisema kuwa mahakama hio inakandamiza mataifa ya Afrika.
Hata hivyo Ocampo amesema mahakama ya ICC ilikuwa kizingiti kwa viongozi kumi ambao walitegemea na kutumia sana ghasia ili kusalia mamlakani.
Share:

Idadi ya waliouawa Pakistan yafika 130.



Vikosi vya usalama nchini Pakistan vinakabiliwa na hali ngumu kuweza kudhibiti shule iliyovamiwa na wapiganaji wa Taliban katika jimbo la Peshawar Kaskazini Magharibi mwa Pakistan
Takriban watu miamoja na thelathini wamefariki , wengi wao wakiwa watoto.
Msemaji wa jeshi anasema washukiwa sita wameuawa huku operesheni hio ikiendelea.
Shule hio inasimamiwa na jeshi na wanafunzi wengi ni watoto wa wanajeshi.
Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana kujeruhiwa japo idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi.
Maafisa mjini Peshawar wanasema kuwa wanaume watano ama sita waliokuwa na silaha waliingia shuleni humo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi .


Wanafunzi mia tano na waalimu walikuwa katika shule hiyo ya umma ya kijeshi wakati sham,bulizi hilo lilipotokea .
Wakazi wa eneo hilop wanasema kuwa walisikia milio ya bunduki iliyodumu kwa dakika kadhaa .
Wanasema pia kuwa walisikia sauti za kelele za wanafunzi na waalimu .


Haijabainika wazi ni kwa namna gani wanamgambo wa Talebain waliweza kupenya hadi kuingia ndani ya majengo hayo yanayomilikiwa na jeshi.
Jeshi la Pakistan limesema operesheni ya uokozi ilikuwa ikiendelea na kwamba wengi wa wanafunzi na waalim wameokolewa toka eneo la hatari.
Shambulio hilo limetokea wakati operesheni kubwa ya kijeshi ikiendelea dhidi ya wapiganaji wa Taleban wa Pakistan na wanamgambo wengine wanaoendesha harakati zao kaskazini mwa jimbo la Waziristan.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.