Saturday 25 April 2015

Je,michezo huathiri ubikra wa wasichana?


Mwalimu mkuu wa shule moja ya kiislamu mjini Melbourne, Australia amedaiwa kuwazuia wasichana katika shule hiyo kutoshiriki katika maswala ya michezo kwa hofu kwamba huenda wakapoteza ubikira.
Wanafunzi wa kike katika chuo cha Al-Taqwa mjini Truganina pia walizuiwa kucheza soka kwa kuwa majeruhi huenda yakawafanya kuwa tasa kulingana na fairfax.
Wasimamizi wa shule hiyo kwa sasa wanachunguza madai hayo yaliowasilishwa dhidi ya Mwalimu mkuu Omar Hallak ambaye awali alizua hisia kali baada ya kusema kuwa wapiganaji wa Islamic state walikuwa wakiungwa mkono na mataifa ya magharibi.
Katika barua iliondikwa na wizara na kuchapishwa na The Age,mwalimu mmoja wa zamani alisema kuwa:''Anaamini kwamba iwapo wasichana wataruhusiwa kukimbia huenda wakapoteza ubikra wao.Mwalimu huyo pia ana ushahidi wa kisayansi unaosema kuwa iwapo wasichana watajijeruhi,kupitia kuvunjika mguu wakati wanapocheza soka huenda ikawafanya kuwa tasa''..
Mwalimu huyo amedai kwamba Bwana Hallak aliwazuia wanafunzi wa kike kutoshiriki katika mashindano ya wilaya ya mbio za marathon mwaka wa 2013 na 2014.
Share:

Ng'ombe awala kondoo Kenya.


Mkulima mmoja nchi Kenya anasema kuwa mmoja wa ng'ombe wake amesusia lishe yake ya kawaida na kuanza kuwala kondoo.
Charles Mamboleo, ambaye anamiliki shamba kusini magharibi mwa kaunti ya Nakuru aligungua kuwa ng'ombe wake amemla kondo siku moja asubuni.
Jitihada zake za kumpa ng'ombe huyo chakula na maji hazikufua dafu, na siku iliyofuata ng'ombe huyo alimla kondoo mwingine.
Kulingana na afisa mmoja wa kilimo ni kuwa , huenda tabia ya ng'ombe huyo huenda imetokana na ukosefu wa madini yanayopatikana kwa mimea mbichi.
Hali ya kiangazi ambayo ilimalizika hivi majuzi huenda imesababisha mifugo kukosa madini yanayopatikaan kwenye nyasi mbichi. Mwaka 2007 ndama mmoja nchini India alinaswa kwenye mkanda wa video akila kuku.
Share:

Wahamiaji:Wanahabari wa UK washtumiwa


Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Hussein, amekuwa akifadhaishwa sana na lugha ya magazeti ya Uingereza wanayotumia dhidi ya wakimbizi, lakini ni taarifa ya hivi punde iliyochapishwa na makala ya
‘The Sun’ iliyomghadhabisha zaidi.
Makala hiyo iliwaita wakimbizi mende, matamshi ambayo Hussein anasesema ni sawia na yale yaliotumika Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari.

Mkuu huyo wa Haki za Kibinadamu amesema taarifa hiyo ya The Sun ilikuwa mojawapo tu ya taarifa nyingi za chuki na za kibaguzi ambazo zimechapishwa kwa miongo mingi na magazeti ya Uingereza.
Alisema desturi hii ilikuwa inaongeza moto wa chuki na udhalilishaji wa binadamu wengine. Hussein alisema kuwa malalamishi kuhusu makala hizo tayari yamepelekwa kwa Polisi wa jiji na akataka kuchukuliwe hatua kali.

Matamshi haya, hasa kutoka kwa afisa wa juu sana wa umoja wa mataifa, umeashiria wasiwasi ulioko kuhusu mjadala unaoendelea bara Uropa kuhusu wakimbizi wanaovukia Meditteranean kuingia Ulaya .
Mjadala ambao unasemekana unaendeshwa na hisia kali kwenye vyombo vya habari, na kwamba maoni ya uma huenda hayaungi mkono hatua zinazohitajika kuokoa maisha ya wanaokufa maji huko mediterrenean
Share:

Washukiwa wa ugaidi wakamatwa Italia


Polisi nchini Italia wanasema kuwa wamewakamata watu 18 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Islamic State kutoka nchini Afghanistan na Pakistan katika oparesheni kubwa ya kupambana na ugaidi.
Wanasema kuwa wawili kati ya washukiwa hao wanaaminiwa kuwa walinzi wa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden na wengine wanashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi nchini Pakistan likiwemo shambulizi lililotokea kwenye soko la Peshawar.
Oparesheni hiyo ilikuwa imeendeshwa kwenye kisiwa cha Italia cha Sardina .
Polisi walisema kuwa kundi linalofanyiwa uchunguzi lilikuwa limewapangia wanachama wake kuingia nchini Italia wakiwa na vyeti vya kufanya kazi au kama watafuta hifadhi.
Share:

Mwanaharakati maarufu auawa Pakistan


Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini Pakistan Sabeen Mehmud ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mji mkuu Karachi.
Alivamiwa na watu wasiojulikana alipokuwa akielekea nyumbani kwake baada ya kuandaa warsha kuhusu kuhusika kwa jeshi la Pakistan katika kuwatesa na kuwaua wanaharakati wa kisiasa nchini humo.
Bi Sabeen ambaye alikuwa na umri wa miaka 38, alikuwa pia mkurugenzi wa shirika moja la misaada na wa duka moja la vitabu ambapo mazungumzo kuhusu haki za binadamu yalikuwa yakifanyika.
Duka hilo lilikuwa moja ya maeneo machache mjini Karachi ambapo wanafunzi na wanaharakati walikuwa wakikutana kujadili changoto zinazoikumba Pakistan.
Share:

Google yazindua huduma mpya ya simu


Kampuni ya Google imatangaza kuwa itazindua huduma mpya nchini Marekani ambayo inaweza kutumiwa nyumbani na wakati wa safari za mataifa ya kigeni.
Huduma hiyo inayo fahamika kama Project Fi inatapatikana kwa simu za Smartphone za Google Nexus 6.
Huduma hiyo itatumia maeneo yaliyo na Wi-Fi sambamba na huduma zingine za mawasilianoi nchini Marekani za Sprint na T-Mobile na inaweza pia kutumiwa kwenye nchi 120 bila malipo ya ziada wakati mtu anaposafiri nje ya nchi.
Huduma hiyo itatolewa kwa malipo ya dola ishirini kwa mwezi kwa huduma za kawaida na dola kumi kwa mwezi kwa kila gigabyte ya data inayotumika.
Google inasema kuwa huduma hiyo huwa inajiunga moja kwa moja na zaidi maeneo milioni yenye huduna za Wi-Fi na mteja ana uwezo wa kuhamiswa kutoka kwa mtandao mmoja hadi mwingine kulingana na ni upi unaotoa huduma bora zaidi.
Share:

Sherehe za miaka 100 zafanyika Gallipoli


Sanamu za makumbusho Gallipoli

Sherehe zimefanyika eneo la Gallipoli nchini Uturuki kuadhimisha miaka mia moja tangu uvamizi wa kijeshi uliofanywa eno hilo na wanajeshi wa muungano wakati wa vita vya kwanza vya dunia.
Zaidi ya watu 100,00 waliuwa kwenye uvamizi huo ulioendeshwa dhidi ya ufalme wa Ottoman.
Wageni kutoka nchi zote zilizopigana walihudhuria sherehe hizo wakiwemo viongozi kutoka Uturuki , Australia na New Zealnd, ambazo zote zilipoteza watu wengi.
Sherehe pia zilifanyika mapema nchini New Zealand na pia mjini Sydney. Zaidi ya wanajeshi 10,000 wa Australia na New Zealand waliuawa kwenye vita hivyo vilivyofeli.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.