Friday 6 March 2015

Chanjo ya Ebola kujaribiwa Guinea..


Shirika la afya duniani WHO pamoja na wadau wake, mwishoni mwa wiki hii wanatarajia kuanza majaribio ya ufanisi wa chanjo dhidi ya Ebola nchini Guinea.
Chanjo hiyo aina ya VSV-EBOV imetengenezwa na wakala wa afya ya umma nchini Canada ambapo imeelezwa chanjo nyingine ya pili itaanzishiwa majaribio kadri shehena ya kutosha itakapo patikana.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt.Margaret Chan amesema majaribio yatafanyika kwenye maeneo ya Basse Guinée ambayo ndio yameathirika zaidi na Ebola kwa sasa nchini Guinea na utoaji wake utaanzia kwa wagonjwa wapya na wale wote ambao wamekuwa karibu nao.
Lengo la jaribio la sasa ni kutathmini iwapo chanjo hiyo itawapatia kinga dhidi ya Ebola watu waliokuwa na makaribiano na mgonjwa na pili iwapo utoaji wa chanjo utajenga kinga kwa wale waliopatiwa na hivyo kuzuia maambukizi zaidi.
WHO imesema imejitahidi kwa dhati kuhamasisha nchi zilizoathirika na ugonjwa huo pamoja na wadau ili kuendeleza mbinu za kinga na iwapo chanjo hiyo itafaa itakuwa ni hatua ya kwanza ya kinga dhidi ya Ebola.
Wadau wanaoshirikiana na WHO kwenye majaribio hayo ya chanjo ni pamoja na wizara ya afya ya Guinea, madaktari wasio na mipaka, MSF na taasisi ya afya ya umma, Norway.
Share:

Mkanyagano watokea katika kivuko Kenya..


Ripoti zinasema kuwa mkanyagano umetokea katika kivukio cha Ferry katika eneo la Likoni huko Mombasa Kenya na kuwajeruhi watu kadhaa
Tukio hilo limejiri baada ya ferry tatu zinazoendesha oparesheni zake katika kivuko hicho kukabiliwa na matatizo ya kiufundi.
Kulingana na ripoti hizo Ferry zilizosalia zimeshindwa kuhudumia idadi kubwa ya watu wanaotumia kivuko hicho pamoja na ile ya magari.
Hatua hiyo imesababisha msongamano mkubwa wa watu katika kivuko hicho.
Share:

Dereva Mpalestina awagonga Waisraeli....


Polisi nchini Israeli wanasema kuwa dereva ambaye anaaminiwa kuwa Mpalestina amevurumisha gari katikati ya kundi la watu kwenye mtaa mmoja mjini Jerusalem.
Wanasema kuwa mwamamume huyo aliwajeruhi takriban wapita njia wanne na kisha akajaribu kumchoma kisu mtu mwingine kabla ya kupigwa risasi na kujeruhiwa na maafisa wa usalama.
Msemaji wa polisi amekitaja kitendo hicho kuwa shambulizi la kigaidi.
Kulishuhudiwa visa vingine kama hivyo mwaka uliopita vilivyoendeshwa na madereva wa Kipalestina ambapo watu watatu waliuwa.
Share:

Oxfam:Wanajeshi wa DRC ni wanyanyasaji...


Shirika la kutoa misaada la Uingereza Oxfam limesema kuwa dhuluma zinazoendeshwa na wanajeshi mashariki mwa jamhuri ya demokrasi ya Congo ni mbaya sawa na zile zinazoendeshwa na waasi.
Wanavijiji wamelalamikia kukamatwa bila sababu, kuporwa na kulazimishha kufanya kazi pamoja na kutozwa ushuru kwa lazima.
Wengine wanasema kuwa wamelazimishwa kulipa ili kuweza kupitia kwenye vizuizi haramu na kupigwa ikiwa watakataa.
Makubaliano na kundi la M23 ya mwaka 2003 yalinuia kuleta amani katika eneo hilo na makundi ya waasi likiwemo lile la FDLR yanaendelea na harakati zao.
Share:

Thursday 5 March 2015

Ford yazindua baiskeli ya kielektroniki..



Kampuni ya kutengeza magari ya Ford imezindua baiskeli ya kielektroniki kwenye mkutano mkubwa................ >>>>>INGIA HAPA..<<<<<
Share:

Balozi wa Marekani ashambuliwa...




Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akibwata kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya jumuiya yao.
Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.
Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote .
Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kam hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa polisi Yoon Myung na amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine kumhusu .

Naye msemaji wa baraza la maridhiano na ushirikiano ambaye alikuwa ndiye muandaaji wa mkutano huo, ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi madhubuti .
Balozi Lippert, ni mshauri wa muda mrefu wa Raisi Obama na mambaye pia aliwahi kuwa msaidizi wa katibu mkuu wa ulinzi katika masuala ya mahusiano na bara la Asia,na alipata nafasi ya kuwa balozi Korea Kusini mwezi October mwaka wa jana.
Lippert amewahi pia kushika wadhifa wa afisa wa usalama wa taifa katika paresheni maalum na alitwaa medali ya nyota ya shaba nyeusi wakati alipoitembelea Iraq.
Korea Kusini na Kaskazini walitengana tangu mwaka 1950-53 baada ya vita vya Korea nab ado kiufundi wako vitani kwakuwa mapigano yalisitishwa kwa suluhu .
Marekani na Korea Kusini wameunganisha nguvu za kijeshi na wiki hii wako katika mazoezi kufuatia hali tata ya kiusalama kutoka kwa wakomunisti walioko Kaskazini .
Pyongyang wanadai kuwa wana fanya mazoezi kwa kujiweka tayari na uvamizi wowote utakao tokea wakati huo huo Korea Kusini na Marekani wao wanadai kuwa mazoezi yao ni kwa kujihami tu .
Marekani inakadiriwa kuwa na vikosi vya askari wake wapatao30,000 vya kudumu vilivyopiga kambi Korea Kusini.
Share:

Viapo vya ndoa havitekelezeki...


Ahadi ya kuwa pamoja maishani katika shida na raha,taabu na shida viapo hivi ama ahadi hizi zinaonekana kuchukuliwa kirahisi mno na wanandoa wapya, lakini kwa muujibu wa utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni unathibitisha kuwa ni rahisi mno kutamka kuliko utekelezaji wa viapo vyenyewe .
Mtafiti uliofanywa kwa wanandoa wenye bahati 2,700 waliooana umegundua kwamba ,ikiwa mwanamke katika ndoa hiyo ataugua kwa muda mrefu asilimia sita hukaribia kupewa talaka kuliko wale ambao wana afya njema .
Ukilinganaisha na wanaume ambao huugua wakiwa kwenye ndoa,hatari ya kuvunjika kwa ndoa ni ndogo mno,hatahivyo upendo huendelea hadi hapo mmoja wao atakapo baki kuwa mgane ama mjane.
Utafiti ulioongozwa na wanazuoni wa chuo kikuu nchini Marekani,kinapendekeza kwamba kwa asili, wanawake wao wameumbwa kutoa huduma katika familia zao nah ii inamaanisha kwamba wanaume wao huwa hawana uvumilivu wake zao pindi wanapokumbwa na maradhi ya muda mrefu ,ambayo pia yanweza kuwa hayatabiriki kuyakabili.
Walifanyiwa utafiti wanandoa nchini Marekani,ambao wote walikuwa na umri wa miaka 50, mnamo mwaka 1990 ambao waliulizwa juu ya afya zao kuhusiana na maisha yao wakichnugza kwa miaka miwili,miwili ndani ya utafiti uliofanywa kwa miaka ishirini.
Asilimia thelathini na mbili ya ndoa ziliishia kwa kuachana na asilimia ishirini na nnenzilivunjika kutokana na vifo vya mmoja wa wanandoa.
Kikosi cha utafiti kiliongozwa na Amelia Karraker, ambaye ni profesa msaidizi juu ya masuala ya maendeleo ya binaadamu na utafiti juu ya familia kutoka katika chuo cha Iowa State University,analinganisha matukio ya namna nne kansa,magonjwa ya moyo,kiharusi na magonjwa ya njia ya hewa kwa wanawake na wanaume na matokeo ya ndoa.

Utafiti huo umebainisha kwamba , kuna tofauti ya kujisikia mgonjwa sana na huwezi kupika chakula cha jioni, ama unahitaji mtu hasa wa kukulisha masuala haya yanaweza kubadili upepo ndani ya ndoa .
Katika hali hiyo,utafiti huo hauoneshi dhahiri kuwa mume ama mke anadai talaka,takwimu kamili zinaonesha kwamba wanawake ni wepesi zaidi kuomba talaka kuliko wenza wao.
Bi Karraker anasema amegundua kwamba kwamba inawezekana baadhi ya wanawake ambao huachwa kwasababu ya huduma zao ama kushindwa kuhudumia
Tafakari juu ya Uhai ama kifo husababisha watu wajitafiti wenyewe na kujiuliza maswali muhimu kuwa ni nini muhimu maishani mwao? Anaeleza mtafiti huyo.
Wanawake wakati mwingine huribuka kwa kusema kuwa waume zao hawawajali,na hawafurahishwi na suala hilo ama husema sikufurahishwa na mwanzo wa mahusiano yao, na wansema kwamba wako radhi kubaki peke yao kuliko kujitosa katika ndoa isiyofaa.
Share:

Wadaiwa kushirikiana na Al-Shabaab...




Mamlaka nchini Somalia imewakamata wanajeshi wake wa ngazi za juu na kuwatuhumu kwa kushirikiana na wapiganaji wa kundi la Al-shabaab.
Tayari maafisa 12 wanachunguzwa kwa madai ya kuwasaidia wapiganaji hao kushambulia hoteli ya The SYL katika mji mkuu wa Mogadishu mnamo mwezi Januari.
Ujumbe kutoka Uturuki ulikuwa ukiishi katika hoteli hiyo ukisubiri ziara ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Watu watatu waliuawa katika shambulizi hilo la bomu.
Jeshi la serikali ya Somali linalosaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika linajaribu kulishinda kundi la Al-shabaab
Share:

Kikwete akutana na viongozi wa albino...


Baadhi ya walemavu wa ngozi yaani albino mapema Alhamisi walifanya vurugu nje ya Ikulu ya Tanzania wakati viongozi wao wakisubiri kuingia katika kikao na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete alikuwa akitarajiwa kufanya mkutano na viongozi wa Albino Tanzania TAS, aliowaalika kuzungumzia hoja zao kutokana na mauaji ya walemavu hao yanayoendelea nchini humo.
Kutokana na vurugu hizo maafisa wa Ikulu waliwatawanya walemavu hao kutoka nje ya geti.
Share:

Wanne wahukumiwa kifo Mwanza...


Mahakama kuu ya Tanzania Mwanza imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne akiwemo mume wa marehemu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua zawadi Mangidu [22] wa kijiji cha Nyamalulu kata ya Kaseme wilayani Geita.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Joaquine De-Mello katika ukumbi uliokuwa umefurika wasikilizaji wakiwemo ndugu wa upande wa washtakiwa na baada ya kutolewa hukumu baadhi ya ndugu wa washtakiwa walitokwa na machozi
Waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa ni Masalu Kahindi[54]Ndahanya Lumola[42]Singu Nsiyantemi[49]na Nassor Said[47] ambaye alikuwa mume wa marehemu Zawadi Mangindu wote wamepatikana na hatia ya kula njama na kushiriki kumuua zawadi kwa kukusudia ambaye alikuwa mlemavu wa ngozi.
Katika hukumu yake Jaji De-mello alisema alikuwa amezingatia kwa makini na tahadhari kubwa katika kufikia uamzi huo baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mashahidi 12 waliitwa na kutoa ushahidi pamoja na ule wa Utetezi na kisha kujiridhisha kuwa pasipo kuacha shaka yoyote washtakiwa walitenda kosa hilo.
Aliongeza kuwa katika hukumu zilizotangulia pia zimebainisha kuwa mauaji ya walemavu wa ngozi yamekuwa yanatekelezwa na mtandao mkubwa na siyo rahisi kuubani bila umakini na kuomba katika kesi zijazo pia wanunuzi wa viungo na wagangawanaopiga ramili nao wafikishwe mahakamani kwani uzoefu unaonyesha wauaji hufikishwa mahakamani kwani nao ni wauaji.
Huku wasilikizaji wakifuatilia kwa umakini hukumu hiy wakati akiisoma Mheshimwa Jaji De-mello aliisisitiza kuwa Ushahidi uliotolewana Magdalena Shimba mama mzazi wa marehemu na shahidi Semeni [14]waliothibitisha mahakamani kuwaona na kuwatambua washtakiwa wa kwanza na wanne kwenye eneo la tukio pamoja na mazingira yaliyoelezwa mahakamani yanaifanya mahakama pasipo kuacha shaka yoyote.
Awali upande wa Mashtaka wakati ukiongozwa na wakili wa serkali Hezron Mwasimba akisaidiana na wakili Janeth Kisibo ulidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa kwa pamoja kwa makusudi walishirikiana kula njama na kutenda kosa la kumuua Zawadi Mangidu[22] aliyekuwa mlemavu wa ngozi hapo Machi 11 mwaka 2008 saa moja usiku katika kijiji cha Nyamalulukata ya Kaseme Wilayani Geita walitenda kosa hilo na pia kumjeruhi mtoto Chausiku aliyekuwa na umri wa miezi 9 wakati huo kwa panga katika mkono wake akiwa mtoto wa mareheu.
Upande wa mashtaka uliendelea kudai washtakiwa walikamatwa kwa nyakati tofauti baadaye na taratibu za kisheriazilizingatiwa ikiwemo kupewa nafasi ya kutoa maelezo ya onyo na kutoa Ungamo na baadaye walifikishwa mahakamani ambapo Jamhuri iliwezakuita mashaihdi 12 na kutoa ushahidi hivyo kuiomba mahakama kuu kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili kuwa fundisho kwa watu wengine aina hiyona kuwa ilidaiwa viungo hivyo hutumiwa kuwawezesha watu kupata utajiri ikiwemo wa madini.
Hata hivyo wakati wa kesi hiyo malumbano makubwa yalitokea wakati upande wa utetezi ukipinga maelezo ya Ungamo na Onyo kutopokea kama kilelelezo na mahakamawkwa madai wastahkwia walishinikizwa kukiri maelezo hayo hatua iliyomfanya Jaji kuingilia kwa kusema kuwa mazingira ya yaliyochukuliwa maelezo hayo ya ungamo na Onyo yanaashiria washtakiwa hawakulazimishwa hivyo mahakama kuu kuyapokea kama sehemu ya ushahidi.

Wakati kesi hiyo ilidaiwa na upande wa mashatka kuwa washtakiwa wanadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 250,000 kati ya shilingi 1,250,000 kutoka kwa wakala wa kununua viungo hivyo baada ya kuvifikisha ilibainika viungo vya marehemuhavikuwa na kiwango cha ubora unaotakiwa hivyo Wakala wao alikataa kumalizi a kaisi cha shilingimilioni 1 kilichokuwa kimebakia ambaye alitajwa mahakamani kwa jina la Hamis Hamad mkazi wa mkoani Shinyanga ambaye hakuweza kupatikana.
Ilidaiwa kuwa baada ya mlemavu wa ngozi kuuawa viungo vyake hufanyiwa utambuzi wa ubora wa viungo vyake ambapo wembe,radio na sarafu ya shilingi kumi hutumiwa katika kutambua ubora wake na kiungo kikigusishwa kwenye radio ,radio hukwaruza kwa kupiga kelele na hata kuzima ubora huo ndio unaotakiwa lakini kisipotoa ishara hizo basi kinakuwa hakina kiwango cha ubora unaoatakiwa hakihitajiki.
Jaji De-mello alihitimisha kwa kuamru washtakiwa kunyongwa hadi kufa ,..na haki ya kukata rufafa ilkuwa wazi kwao hivyo kuufanya ukumbi mzima kukaa kimya na baada ya kutoka nje ya ukumbi wengi walijitokeza kuunga mkono hukumu hiyo,na imekuja huku kukiwa na tukio la mtoto Yohana bahati naye kuuawa mkoani humo.
Share:

B Fasso:Mwili wa Sankara kufukuliwa....


Serikali Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara .
Watu wa familia ya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani.
Mjane wa marehemu Miriam,akizungumza kupitia njia ya simu kutoka Paris amesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji yake.
Bwana Sankara aliuawa mnamo mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaore kuchukua mamlaka.
Blaise Campaore aliondolewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita.
Serikali mpya inayoongozwa na Michael Kafando ,ilisema kuwa italiangazia suala hilo wakati ilipochukua madaraka.
Mwili wa Sankara ulizikwa katika kaburi lisilotambulika miongoni mwa makaburi yaliopo mashariki mwa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.