Saturday 28 February 2015

Utafiti:Wanawake huwa na mpango m'badala..


Nusu ya wanawake huwa na mpango mbadala ama wa kando ambao wanaweza kukimbilia iwapo uhusiano wao utaharibika.
Utafiti uliofanywa miongoni mwa wanawake 1000 uligundua kuwa asilimia kubwa imeweza kuwaweka wanaume mbadala pindi tu uhusiano walionao unapoharibika.
Cha kushangaza ni kwamba wanawake waliomo katika ndoa huwa na mpango mbadala ikilinganishwa na wale walio katika uhusiano wa kawaida.
Pia imebainika kuwa mpango huo wa kando huenda akawa rafiki wa zamani ambaye amekuwa akimpenda mwanamke huyo.
Wengine huwa wapenzi wa zamani ama hata mume waliyeachana naye,rafiki ama mtu ambaye walikutana katika eneo la mazoezi.
Utafiti huo ulifanywa na kampuni ya utafiti wa mtandaoni wa Onepoll

Share:

Facebook kupambana na vitendo vya kujiua..


Mtandao wa Facebook umeanzisha Nyenzo mpya nchini Marekani kuwasaidia watumiaji wenye mashaka na marafiki ambao wako hatarini kujiua.
Nyenzo hii itawasaidia watu kuripoti ujumbe ambapo ripoti hizo zitaufikia mtandao wa facebook kwa haraka.
Afisa Mkakati wa Mtandao wa Facebook, Holly Hetherington amesema mara nyingi Marafiki na Familia wamekua wakishuhudia hali ya hatari kupitia ujumbe unaowekwa lakini wamekuwa wakishindwa kujua cha kufanya.
Awali watumiaji wa facebook walikuwa wakiandika ujumbe kwenye kurasa zao kuhusu kujitoa uhai lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wakati.
Share:

Wanaolala sana kushikwa na kiharusi..


Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajua sababu yake.
Utafiti uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.
Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi.
Hatahivyo haijabainika kutoka kwa utafiti huo iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi ama iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa yasiojulikana.
Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya miaka 42 na 81.

Watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi.
Baada ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu waliosema wamekuwa wakilala kwa zaidi ya masaa manane walipatikana na hatari ya asilimia 46 kupatwa na ugonjwa huo.
Wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana na hatari ya asilimia 18
Share:

Mafuriko yawaua watu 14 Madagascar..


Watu 14 wameuawa kwenye mafuriko nchini Madagascar ambapo pia wengine 20,000 wamelazimika kuhama makwao.
Mafuriko hayo yaliukumba mji mkuu Antananarivo na maeneo yaliyo karibu.
Utawala unasema kuwa mvua nyingi siku zijazo huenda ikasababisha madhara zaidi.
Mvua kubwa imenyesha nchini humo kwa takriban wiki mbili.
Mwezi uliopita kimbunga Chedza kiliwaua watu 80 nchini Madagascar.
Share:

Rwanda:Serikali yaagizwa kuishtaki BBC...


Tume ya uchunguzi nchini Rwanda imebaini kwamba kipindi cha shirika la habari la BBC kilichopeperushwa hewani na kuuliza maswali mengi kuhusu mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 hakikufikia kiwango kinachohitajika cha kitengo cha uhariri cha shirika hilo.
Mkuu wa tume hiyo Martin Ngoga alipendekeza serikali ya Rwanda kuanzisha kesi ya jinai dhidi ya shirika hilo.
BBC imesema kuwa imesikitishwa na matokeo ya uchunguzi huo na inatathmini athari zake.
Serikali ya Rwanda ilisimamisha matangazo ya shirika la BBC kupitia huduma yake ya kinyarwanda baada ya kipindi hicho kilichopeperushwa na runinga ya BBC na kuwashtumu watayarishaji wake.
Share:

Mbunge John Komba wa Tanzania afariki...






marehemu Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake Mbezi tangi Bovu akielezea kuimarika kwa afya yake aliporejea kutoka India kwenye matibabu, Julai 27, 2012.

Mbunge na Mwimbaji maaarufu wa nyimbo za Siasa nchini Tanzania, Keptain John Komba amefariki dunia siku ya jumamosi jioni.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa Chama tawala cha Tanzania chama cha Mapinduzi Nape Nnauye Mbunge huyo ambaye alikuwa maarufu kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za kampeni za chama hicho kifo cha chake kimetokea siku ya jumamosi majira ya jioni.
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.
Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.
Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.