Saturday 27 June 2015

Misikiti 80 kufungwa Tunisia.


Utawala nchini Tunisia unasema kuwa utafunga misikiti 80 katika kipindi cha wiki moja inayokuja kwa madai ya kuhubiri chuki na jihad.
null
Hii ni kufuatia shambulizi lililofanyika kwenye hoteli moja hapo jana ambapo takriban watu 39 wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya ulaya waliuawa na mwanamme mmoja aliyejifanya kuwa mtalii.
Wapiganaji wanaoshirikiana na wanamgambo wa Kundi la kiislamu la Islamic State wamesema kuwa wao ndio waliotekeleza shambulizi hilo.
null
Miili ya watalii ilikuwa imetapakaa ufukweni
Waziri mkuu nchini Tunisia Hanib Essid anasema kuwa misikiti hiyo ndio iliokuwa ikitumika kueneza propaganda na kuunga mkono ugaidi.
null
Waziri mkuu ametangaza kuwa misikiti hiyo ndiyo imekuwa ikihubiri Jihad
Hali ya usalama umeimarishwa maradufu katika maeneo mengi mjini Tunis na karibu na majengo yenye watalii wengi.
null
Mpiganaji mmoja alijifanya kuwa mtalii kabla ya kuwafyatulia risasi watalii ufukweni
Tayari wanajeshi wa akiba wameamrishwa kuripoti mara moja katika kambi za jeshi zilizoko karibu nao.
Share:

Vuna mbegu za kiume mkiwa na miaka18.


Mbegu za uzazi wa wanaume zinapaswa kuvunwa na kuhifadhiwa pindi mtu anapotimiza umri wa miaka 18.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti wa maswala ya uzazi nchini Uingereza, manii ya mwanaume huwa katika hali bora zaidi wakati huo na hivyo zinapaswa kuvunwa na kisha kutumika kupandikiza wanawake katika siku za usoni.
Daktari Kevin Smith, ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Abertay kilichoko Dundee Uingereza anasema kuwa baada ya utafiti wa kipindi kirefu amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ilikuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
null
Daktari Kevin Smith ameorodhesha ugonjwa wa akili ''autism'', na ule wa kuchanganyikiwa ama ''schizophrenia'' miongoni mwa magonjwa mengine mengi.
Dakta Smith, anasema kuwa wizara ya afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi ilikupunguza visa vya maradhi aliyoorodhesha.
Maoni yake hata hivyo yanapingwa na muungano wa wauguzi wa uzazi ambao wanasema kuwa hilo halitakuwa suluhisho la kudumu.
Badala yake shirika hilo linaitaka serikali ya Uingereza iweke sera zitakazowasaidia waingereza waliofikia umri wa uzazi kupata ajira.
null
Takwimu zinaonesha kuwa wanaume wanaanza kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 33 ikiwa ni ongezeko kutoka kwa miaka 31 katika miaka ya tisini.
Akitetea wazo lake katika jarida la madaktari la ''The Journal of Medical Ethics, Dakta Smith nasema kuwa wale wanaotaka kupata watoto mapema basi wafanye hivyo lakini kwa wale ambao wamegonga maiaka 40 ni vyema watumie mbegu walizohifadhi kwa matokeo mazuri zaidi.
Profesa Adam Balen, wa shirika la British Fertility Society, ameonya kuwa mbegu ziliyohifadhiwa huwa hazina nguvu kama zile zinazotolewa moja kwa moja.
null
''Kwa mtazamao hawa vijana wanahitahitaji ajira na wapenzi basi watapata watoto pasi na matatizp yeyote.''alisema Profesa Balen
Wakati huo huo mwanasayansi mwenza Sheena Lewis, aliwashauri wanaume waanze kushughulikia swala la familia mapema katika ujana wao.
''ninataka kuwaelezea wazi kuwa umri mzuri wa kuzaa kwa wanaume na wanawake ni kati ya miaka ya 20 na 30."
Share:

Simba warejea Rwanda baada ya miaka 20..


Mfalme wa mwituni Simba ,atarejea Rwanda kwa mara ya kwanza tangu aangamie wakati wa mauaji ya kimbari mwaka wa 1994
Maafisa wanaowalinda wanyama pori wa Rwanda, wanasema kuwa simba watarudi nchini humo siku ya jumatatu kwa mara ya kwanza, tangu walipoangamizwa baada ya mauaji ya kimbari,ya mwaka wa 1994.
Simba wawili dume, na majike watano, wanasafirishwa kutoka mbuga ya wanyama ya Kwazulu Natal, Afrika Kusini, na Jumatatu watawasili Rwanda kwa ndege.
null
Simba hao saba watawekwa kwenye karantini kisha waruhisiwe kutembea huru katika mbuga ya wanyama.
Wanyama hao watapelekwa katika mbuga ya taifa ya Akagera.
Maafisa wakuu huko Rwanda walisema, kurejeshwa tena kwa simba nchini Rwanda ,ni Kilele cha juhudi kubwa ya kuhifadhi mazingira katika mbuga hiyo na kwa taifa zima kwa jumla.
null
Baada ya mauaji ya kimbari mwaka wa 1994, watu wengi waliokimbia makwao waliikalia mbuga hiyo ya Akagera.
Simba waliokuwa humo walikimbia au kuuawa, huku watu wakijaribu kulinda mifugo yao na maisha yao.
Share:

Siku 1 jela kwa kukojoa hadharani India.


Watu 109 wamehukumiwa kifungo cha siku moja jela kwa kukojoa hadharani huko India.
Polisi waliwakamata takriban watu 109 kwa kukojoa katika vituo vya usafiri wa umma na reli.
Wale wote waliokamatwa wanatuhumiwa kwa kupatikana na hatia ya kukojoa nje ama ndani ya vituo vya reli mjini Agra Kaskazini mwa India .
Waliokamatwa watahukumiwa kifungo cha saa 24 korokoroni ama walipe faini ya kati ya dola mbili na kumi au vyote.
null

Maafisa wa afya ya umma wanasema walifanya operesheni hiyo kwa ghafla ilikukabili uvundo wa mkojo unaoathiri afya ya mamilioni ya watu wanaotumia huduma hiyo ya reli nchini India.
Mkuu wa polisi katika eneo hilo GRP, Gopeshnath Khanna aliyeongoza operesheni hiyo anasema kuwa itaendelea hadi wahindi wanaolaumiwa kwa kuharibu mazingira kwa kutema mate ukutani baada ya kutafuna thambuu na tumbako iliyowekwa rangina kukojoa katika maeneo ya umma watakapo badili tabia zao.
Aidha wasafiri wa reli wanasemekana kupigwa na harafu mbaya ya mkojo pindi wanapoingia ndani ya vituo hivyo.
null
Operesheni hii ni sehemu ya kampeini ya Waziri mkuu mpya Narendra Modi ya kuimarisha afya ya umma al maarufu 'Swachh Bharat.
Operesheni hiyo ni sehemu ya kampeini ya waziri mkuu mpya wa India Narendra Modi ya kuimarisha afya ya umma al maarufu 'Swachh Bharat.
Waandishi wa habari katika eneo hilo la Agra wanasema hii ndio mara ya kwanza kwa maafisa wa kulinda afya ya umma kwa ushirikiano na serikali ya majimbo kuwakamata vikojozi.
Takwimu za afya nchini humo zinaonesha kuwa takriban watu milioni mia sita 600m ama nusu ya raia wa India hawana vyoo.
Share:

Kenyatta: al Shaabab yaishiwa nguvu..

Rais Kenyatta huku amevaa sare ya jeshi
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amelaani siasa kali za baadhi ya Waislamu Afrika Mashariki.
Aliuambia mkutano wa kanda kuhusu usalama unaofanywa Nairobi kwamba kundi la Waislamu la al-Shabab limeishiwa nguvu na kwamba mashambulio yake ni ya kuinusuru tu al-Shabaab yenyewe, siyo kushinda.
Hapo Ijumaa, wapiganaji hao walishambulia kambi ya askari wa Umoja wa Afrika katikati mwa Somalia.
Wanajeshi wa kuweka amani kama 50 kutoka Burundi inaarifiwa waliuwawa.
Piya inaarifiwa kuwa wanajeshi wa Kenya walipambana na wapiganaji Ijumaa karibu na mji wa Dhobley, kusini mwa nchi.
Share:

15 kati ya waliouawa Tunisia ni Waingereza.


Maelfu ya watalii wanaondoka Tunisia baada ya shambulio katika hoteli ya watalii iliyosababisha vifo vya watu 38 wengi wao wazungu.
Maelfu ya watalii wanaondoka Tunisia baada ya shambulio katika hoteli ya watalii iliyosababisha vifo vya watu 38 wengi wao wazungu.
Makampuni ya utalii pia yanavunja safari za kwenda huko.
Katika uwanja wa ndege wa Hammamet, karibu na Tunis, watalii wamepanga foleni kusubiri kuondoka nchini humo.
Serikali ya Tunisia inasema kuwa ulinzi umezidishwa katika maeneo ya utalii huku wanajeshi wa akiba wakitakiwa kuripoti kazini mara moja.
null
Aidha serikali imetangaza kuwa itafunga misikiti 80, inayodaiwa kuwa inafundisha utumizi wa nguvu na Jihad.
Islamic State imesema imehusika na shambulio hilo.
Mshambuliaji aliyekuwa na bunduki, baadae alipigwa risasi na kuuawa.
null
Maelfu ya watalii wanatoroka Tunisia kufuatia shambulizi la kigaidi
Wakati huo huo inaaminika sasa kuwa 15 kati ya wale waliouawa huko Tunisia ni raia wa Uingereza.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema shambulio hilo ni kumbusho la kikatili na kusitikisha, kwamba kuna tisho la ugaidi dunia nzima
"Nitahakikisha, tunafanya tuwezalo kusaidia, na kuwakinga watu na mashambulio ya kigaidi''.
null
''Tunawakumbuka na kuwaombea waliofiwa, na wale waliojeruhiwa''.
''Tunashirikiana na wakuu wa Tunisia, kujua idadi kamili ya Waingereza waliouliwa.''
Lakini wananchi wa Uingereza wanafaa kujitayarisha, kuwa wengi waliouwawa ni Wangereza."Alisema Cameroon.
Share:

Burundi:''Uchaguzi utafanyika Jumatatu''


Balozi wa Burundi katika umoja wa mataifa amekariri kuwa uchaguzi utaendelea mbele Jumatatu licha ya shinikizo uahirishwe
Balozi wa Burundi kwenye umoja wa mataifa amesema kuwa uchaguzi utaendelea jinsi ulivyopangwa siku ya jumatatu licha ya ombi kutaka uahirishwe kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon.
Ban anasema kuwa ana wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Burundi kufuatia mzozo wa kisiasa unaoendelea huko.
null
Balozi Albert Shingiro aliuambia mkutano wa usalama wa umoja wa mataifa kuwa watu wanataka uchaguzi ufanyike.
Balozi Albert Shingiro aliuambia mkutano wa usalama wa umoja wa mataifa kuwa watu wanataka uchaguzi ufanyike.
Vyama vya upinzani na mashirika yasiyokuwa ya serikali tayari yametangaza kuwa watasusia uchaguzi huo.
Waandamanaji wanapinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania urais kwa muhula wa tatu wakidai kuwa inakiuka katiba ya Nvhi hiyo.
null
Uchaguzi wa ubunge unatarajiwa kufanyika Jumatatu
Rais Nkurunziza naye anashikilia kuwa awamu ya kwanza aliteuliwa na wajumbe wala sio raia kama vile inavyohitajika kwenye katiba iliyoundwa baada ya makubaliano ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenye nchini humo.
Takriban watu 50 wameuawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka huu wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu.
null
Maelfu ya raia wengine wa Burundi nao wamehamia mataifa jirani kwa hofu ya kuzuka mamchafuko zaidi.
Uchaguzi wa ubunge unatarajiwa siku ya Jumatatu huku uchaguzi wa urais ukipangiwa kufanyika tarehe 15 Julai mwaka huu.
Share:

Ulaya yakataa kuiongeza Ugiriki muda zaidi.


Mawaziri wa fedha wa mataifa ya ulaya wamekatalia mbali ombi la Ugiriki la kutaka iongezewa muda zaidi wa kulipa deni lake kutoka Jumanne ijayo.
Ugiriki ina hadi Jumanne ijayo kulipa deni lake la zaidi ya dola bilioni moja nukta saba.
Serikali ya Uigiriki chini ya Alexis Tsipras ilikuwa imeombamuda wa majuma mawili iliiandae kura ya maoni
kuhusu makubaliano yaliyopendekezwa na wakopeshaji wa kimataifa wa nchi hiyo.
null
Waziri mkuu nchini Ugiriki Alexis Tsipras,anatarajiwa kuomba muda zaidi wa kulipa deni la IMF
Ikiwa itaidhinishwa kura hiyo itafanyika tarehe tano mwezi Julai.
Awali wagiriki walipiga foleni nje ya mabenki wakihofia kuwa watawekewa masharti dhidi ya kutoa pesa zao.
Mwandishi wa BBC mjini Athens anasema kuwa kulikuwa na uvumi kuwa kiwango kipya cha pesa ambacho mtu anaweza kutoa kwa benki kinaweza kuwa euro 80.
Bunge la Ugiriki nalo liliandaa kikao cha dharura kujadili pendekezo ya kufanyika kwa kura hiyo ya maoni.
Waziri mkuu nchini Ugiriki Alexis Tsipras, anasema kuwa masharti hayo yanayotaka kupunguzwa kwa matumizi ya umma hayawezi kustahimiliwa.
null
Watu nchini Ugiriki wameanza kupanga foleni nje ya mabenki wakihofia kuwa watawekewa masharti dhidi ya kutoa pesa zao
Baadaye atakutana na waziri wa fedha wa nchi za ulaya mjini Brussels kuomba kuongezwa muda zaidi wa kulipa kwa mkopo wa sasa wa Ugiriki.
Muda unazidi kuyoyoma kwa bwana Tsipras kuwa amelipa deni la dola mbilioni 1.7 kwa shirika la IMF ifikapo jumanne ijayo..
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.