Sunday 30 November 2014

MHESHIMIWA PROF. ANNA TIBAIJUKA BORA UJIUZULU KULINDA HESHIMA YAKO NA CHAMA........source GLOBAL PUBLISHER












Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.

Mheshimiwa Bi. Anna Tibaijuka (Mb), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni moja wa viongozi wachache sana wenye ujasiri na kiongozi muwazi katika sakata zima la akaunti ya Tageta Escrow, kwani kiongozi huyu amekiri wazi kuwa amepokea fedha shilingi billion 1.6 kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering Bw. James Rugimalira.
Si jambo jema kumhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka, lakini siyo vibaya kumshauri kwa kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili, basi lingekuwa jambo la maana sana kama angejiuzulu madaraka aliyonayo katika serikali ili kulinda heshima yake na ya chama tawala.
Msomi yoyote yule anapofikia kuitwa Profesa na tena Waziri mwenye kushika dhamana ya nchi na wananchi yaani, Ardhi na Makazi, halafu akakubali kupokea fedha ya kiasi kikubwa hivyo bila ya kutia shaka yoyote kama ananuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana na dhamana ya cheo chake, litakuwa ni jambo jema kwake kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora kuwa yeye ni kiongozi mkweli na viongozi wengine wafuate nyao.
Msomi aliyefikia daraja la juu kabisa tunamwona kama kiongozi anayejua wazi kuwa yeye ni mojawapo wa Mawaziri wachache ambao Wizara zao zina dhamana kubwa ya nchi, leo hii akikubali kununuliwa kiurahisi au kufanya biashara akiwa katika madaraka mazito, tuna mashaka naye ikiwa atandelea kututumikia wananchi katika Wizara ambayo pia inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi.
Watanzania tunajiuliza, hivi Mhe. Anna Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma tena na huku akiwa Mkurugenzi wa Mashirika au Shule na miradi binafsi, ndiyo kusema cheo chake cha utumishi wa umma ndio dhamana ya biashara zake?
Hivi kuna hosptali ngapi hapa nchini hazina dawa? Je wakina mama wangapi wajawazito wanafariki wakati wa kujifungua kwa ukosefu wa vifaa vya mahosptalini? Shule ngapi za serikali hazina madawati?
Leo Mheshimiwa mabilioni ya fedha na kusema kuwa hakujua kama ni fedha chafu. Kwa vipi Watanzania tusiwe na mashaka naye?
Professor Anna Tibaijuka anafahamu wazi kuwa amevunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma "(Sheria namba 13 ya mwaka 1995) ambayo inawataka viongozi watoe taarifa ya zawadi wanazopokea au malipo wanayolipwa."
Hivyo, sisi wananchi wenye kuiamini serikali hii hautuwezi kabisa kukubali au kuona kiongozi tena msomi anavunja dhamana ya wananchi na kumvunjia heshima mkuu wa nchi ambaye ndiye alimteua.
Litakuwa jambo la busara sana Mhe. Anna Tibaijuka ujiuzulu ili kulinda heshima yako kama msomi Professor, pia kulinda heshima serikali na Chama tawala. Huwezi kutumikia ofisi mbili, yaani utumishi wa umma na biashara.

Wanachi tunasikitika sana kuona katika sakata la fedha za umma mpaka baadhi watumishi wa Mungu ambao ni viongozi wa Kanisa nao wanahusika na bila ya woga. Wanapokea fedha bila ya hofu ya kujenga udini.
Share:

Helikopta ya maliasili(TANAPA) yadondoka Jijini dar....

Helikopta ya maliasili(TANAPA) Imedondoka maeneo ya Gongo la mboto, Moshi Bar jijini Dar na kuwa watu wote watano wakiwemo Rubani na Polisi



Share:

housegirl(dada wa kazi) aliyempiga mtoto uganda.....























Baada ya habari za yule msichana anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya kimataifa Duniani, leo kipo alichkizungumza kwa mara a kwanza.

Jolly Tumuhiriwe ambaye kwa sasa amekamatwa na polisi, alisema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi,ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye aikua anaumwa.

Amesema anajiona ni mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.

Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekua wakimtenga sana na wakitaka kumpiga.
Share:

WHO:Watu 7000 wamefariki na ebola........






















Hesabu mpya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO inaonyesha kuwa karibu watu 7000 wameaga duian kutokana na ugonjwa wa Ebola wengi wakiwa eneo la Afrika magharibi.
Hili ni ongezeko la zaidi ya watu 1000 tangu WHO itoe hesabu yake ya mwisho siku nne zilizopita.
Sehemu kubwa ya ongezeko hilo iliripotiwa nchini Liberia
Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa unaohusika na ugonjwa wa Ebola Antony Banburry anasema kuwa kwa sasa nchi iliyoathirika zaid ni Sierra Leone ambapo karibu visa 500 vya ugonjwa wa Ebola huripotiwa kila wiki.

Amesema kuwa maziko ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha maambukizi bado hayafanywi kwa njia iliyo salama.
Share:

Polisi aliyemuua kijana mweusi ajiuzulu........BBC


Wakili wa Darren Wilson ambaye ni afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.
Afisa huyo amekuwa likizoni tangu mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya maandamano.
Gazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28 aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho kwamba ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.
Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali hata kidogo.

Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.