Thursday 26 February 2015

Nyong'o aibiwa vazi lake la bei Mbaya..


Nguo iliyobuniwa na kampuni ya Calvin Klein yenye thamani ya dola 150,000, na kuvaliwa na msanii maarufu wa kike Lupita Nyong'o katika tuzo za Oscar imeibiwa Hollywood .
Gauni hilo lililobuniwa kwa namna ya pekee na kupambwa kiasilia na konokono weupe zaidi ya 6,000 toka baharini, lilichukuliwa kwenye hoteliya London magharibi mwa Hollywood.
Lupita Nyong'o kutoka nchini Kenya aliibuka msanii bora wa kike mwaka jana baada ya miaka kumi na mbili ya utumwa, Lupita alikuwa mtangazaji wa sherehe za jumapili.
Baadhi ya magazeti yanamwita Lupita Nyong'o mrembo wa mwaka 2014.
Sheriff William Nash anasema nguo hiyo inaonekana kuibiwa siku ya jumatano jioni na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kupitia kamera maalum za CCTV.
Share:

Chinja chinja wa IS akamatwe:Ndugu..


Dragana Haines mke wa David Haines,mamlaka zinapaswa kumsaka na kumkamata akiwa hai mtu aliyemuua mume wake kwa kumchinja baada ya kutekwa na kundi la wapiganaji wa dola ya kiislam Islamic State wakati akifanya kazi na shirika la misaada la Uingereza.Mtu aliyemchinja David Haines na wengine tayari amefahamika kuwa ni Mohamed Emwazi.
Bi.Dragana amesema tangu alipojua kuwa mmewe David amechinjwa alijipa matumaini moyoni mwake kuwa ipo siku muuaji huyo atafahamika na hatimaye kukamatwa.Lakini baada ya kupatika kwa taarifa hizi za muuaji huyo anasema kuwa itakuwa faraja ya pekee kwa familia za kila aliyeuawa kinyama na wauaji hao, kwa sababu kama atakutwa amekufa anaona hicho kitakuwa ni kifo cha heshima kwa Mohamed Emwazi, lakini maombi yake ni kwamba kukamatwa akiwa hai na afe baadaye.
Kwa upande wake Barak Barfi ambaye ni msemaji wa familia ya Sotloff iliyopoteza ndugu yao pia, anasema kuwa hawana wasiwasi juu ya kukamatwa kwake muuaji huyo Mohamed Emwazi ama JIHAD JOHN.
"Tuna Imani kubwa sana na nchi ambayo vyombo vyake vya usalama na kiintelijensia vitawakamata watu hawa.Tungependa kwenda kumuangalia muuaji huyu ana kwa ana wakati wa mashtaka yake katika mahakama ya Marekani,na pia kuona akitumikia kifungo chake, katika gereza maalumu ambako ataishi huko pekee yake katika upweke.hiyo ndiyo sheria ya Marekani na hivyo ndivyo nchi yetu inavyoshughulikia matatizo kama haya"amesema Barak.
Share:

Kofi Annan atua Cuba kutatua migogoro,...


Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan amewasili nchini Cuba kuhamasisha mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Colombia na nchi zenye makundi ya waasi.
Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Havana ni mwendelezo wa hjjitihada za kusaka Amani katika nchi kwa zaidi ya miaka miwili hadi sasa.
Hata hivyo katika mazungumzo hayo ya Amani lengo ni kumaliza migogoro iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano.
Annan amesema atakutana na pande zote mbili za viongozi na kuwa na mazungumzo nao ya pamoja na kwamba atatumia uzoefu wake wa utatuzi wa migogoro katika nchi alizowahi kuwa msuluhishi.
Share:

UJUMBE WA RAIS JAKAYA KIKWETE KUTOKA KWA BI. CLARA PETER JUU YA MAUAJI YA WALEMAVU WA NGOZI...habari na matukio blog


Nilizaliwa kwenye familia ya watoto sita nikiwa mtoto pekee mwenye albinism. Mama alitupenda na anatupenda sawa bila kujali hali yangu na kunifanya nijione sawa na wenzangu. Tunapendana sana. (Pichani ni Bi. Clara Peter akiwa na mwanae).
Nilizaliwa kwenye familia ya watoto sita nikiwa mtoto pekee mwenye albinism. Mama alitupenda na anatupenda sawa bila kujali hali yangu na kunifanya nijione sawa na wenzangu. Tunapendana sana.

Hali hii ilinifanya nisijute na wala haitokaa itokee nijute kuzaliwa na hali (mwenye albinism). Mungu aliniumba kwa kusudi lake, kusudi maalum na wala si kwa bahati mbaya. Ila kusudi hili linaharibiwa na kukatishwa na baadhi ya wapumbavu (wauaji) wenye fikra mgando. Ila bado sijakata tamaa nitapambana mpaka dakika za mwisho za pumzi yangu.

Moyo wangu unavuja damu, damu na maji, japo bado nina tumaini la kuishi, moyo wangu huu umekunja ngumi ambayo sijui itatua kwa nani kwani adui yangu simjui. Je Ni familia, wazazi na ndugu zangu, majirani na marafiki au watu kuja nisowajua?

Hivi ni nani hasa anayedhamini mauaji haya ya kikatitili kwa watu waenye albinisim? Hakika hii ni system pana tena pana sana yenye kujitosheleza katika kila Nyanja. System inayolindwa kama nyara za serikali ama hata zaidi ya nyara hizo, kwani siamini kama serikali yetu hii ya maisha bora kwa kila mtanzania imeshindwa kuwakamata wahusika.

Muda mwingine najiuliza hivi mauaji haya yanasababishwa na imani za kishirikina tu au kuna mengine chini ya mwamvuli huu mpana wa imani za kishirikina? Mh! Mimi na wewe hatujui. Na je soko kuu la bidhaa hizi haramu lipo wapi na nani ana hisa nyingi? Pia mimi na wewe hatujui. Kuna connection gani kati ya hawa majasusi wauaji na watunza usalama? Mbona inakuwa ngumu kuwatia mikononi mwa sheria? ama kwa hakika kuna jambo zito ambalo limejificha chini ya kapeti ambalo mimi na wewe hatuljui.

Naamini kwa kutumia teknolojia ya sasa na hasa ya mawasiliano kuyakamata haya majitu mauji kuanzia jani, tawi, shina na hata mzizi wake, mwezi ni mrefu.

Mtukufu Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete watu wenye albinism tunakulilia baba tunaomba utuokoe sisi wana wa Israel tunapukukutika kwani tunaamini AMRI yako itasaidia kusitisha tatizo hili ikiwemo ya kunyongwa mpaka kufa kwa wote waliobainika kuhusika na uchafu huu.

Tunaomba haki itendeke kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na wahanga wote. Tunahitaji uhuru katika inchi yetu, amani na upendo. Mbona tunaishi kwa kuificha kama wahalifu katika nchi yetu? Hatuna hatia wala hatuna bahati yeyote badaala yake tumekosa vimelea vinavyosababisha rangi ya asili (melanini), MSITUUE hakuna tulichotofautiana.

                                                 WE NEED NO,  WE DEMAND JUSTICE
Share:

HATIMAYE KINYESI CHA MWALIMU CHATEKETEZWA...


 Kinyesi kikiwa kimehifadhiwa ndani ya chumba cha mwalimu


Maulid Liuguyo ambaye ni mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke kitengo cha usafi akishiriki katika zoezi hilo.


Mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke Kitengo cha Usafishaji, Ramadhani Athuman akiweka dawa katika vyombo alivyokuwa akitumia kuhifadhia kinyesi mwalimu Gaudensia Albert wa Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam, kabla vyombo hivyo havijaenda kutupwa dampo. (Picha na Francis Dande)



 Umati wa watu ukiwa nje ya nyumba wakati zoezi la kuteketeza kinyesi likiendelea.


 Mlango ukivunjwa ili maofisa wa afya waweze kuingia ndani ya chumba cha mwalimu.


Manispaa ya Temeke leo imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.

Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo walilipata juzi juzi jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa Kata hiyo wafanye utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani.

“Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika, ambapo tulischukua jukumu la kwenda kumhoji Mkuu wa washule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la, hata hivyo, Mkuu wa shule atueleza kuwa alikuwa na akili timamu,”alisema Tembo.

Alisema pamoja na kuutekeza mlundikano huo wa kinyesi pamoja mikojo na matapishi bado wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.

“Hili tukio halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana kuna tatizo lingine ingawa hatuwezi kuamini mambo ya ushirikina lakini haiwezekani mwalimu kama yule ajisaidie na kuhifadhi uchafu kama ule ndani,”alisema.

Aidha, alisema mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la tukio hali iliyofanya mlango wa chumba chake uvunjwe chini ya uwaangalizi wa polisi.

Tembo, alisema mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo la tukio kwa vile alipelekwa Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Haspitali ya Taifa muhimbili kwa ajili ya kupimwa afaya baada ya kupata mshituko ambao umesababishwa na taarifa hizo.

Afisa Afya wa Usafi wa Mazingira, Jumamne Muhogo, alisema uchafu walioubaini ulikuwa ni uchafu wa kinyesi, mikojo na matapishi inasemekana kuna kipindi alikuwa anatapika.

Pia alisema kipo kifungu cha sheria, walifika pale maofisa kutoka idara mbalimbali kupima uzito wa tukio, ambapo kama wangemkuta wangemkamata kwa hatua za kimfikisha mahakamani.

Mhogo, alisema hata kama alikuwa mtaalamu wa sayansi, alikuwa amehifadhi uchafu ule kwa ajili ya utafiti basi hayo yote angekwenda kuyaeleza mahakamani.

“Tukio hili kwa manispa ya Temeke ni la kwanza kutokea yani inaekekea huyu mtu hana akili ya kawaida kama angekuwa na akili za kawaida asingeweza kufanya na mna hii,”alisema.

Umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo walikusanyika kwa wingi tangu saa tatu asubuhi wakisubiri kazi hiyo hadi ilipofnyika saa tisa jioni na wataalamu wa manispaa hiyo.

Wataalamu hao walimwagia dawa uchafu huo kisha kuanza ubeba na kutumbukiza chooni kwa uangalifu mkubwa.

Walipomaliza walvisafisha vyombo hivyo kwa kutumia dawa ambazo zimeweza kusaidia kuondoa harufu mbaya iliyokuwa imezagaa hewani.

Awali, Sajenti wa Jeshi la Polisi  Ramadhan Kagolo, alisema aliwajibika kusimamia kuvujwa kufuli la chumba hicho kwa vile Kazi iliyokua ikifanyika ni kwa ajili ya kulinda afya ya jamii.
Share:

Mtandao wa 5G hadi mwaka wa 2020...



Wanasayansi wamefaulu kuzindua mtandao wa 5G......>>>>>INGIA HAPA<<<<<
Share:

BBC yawateua Vijana wabunifu Kenya..


Makundi mawili ya ubunifu wa kiteknoligia wameteuliwa kuisaidia shirika la utangazaji la BBC kuafikia ruwaza yake ya kupanua upeo wa usikilizaji wa vijana kupitia kwa mfumo mpya wa kidijitali.
Vijana hao wataalamu wa digitali kutoka muungano wa Go Sheng na Ongair walichaguliwa kutoka timu 13,zilizoshiriki mashindano hayo kutoka Afrika na Marekani.
Mashindano ya ubunifu "hackathon" ya BBC yalilofanyika mjini Nairobi Kenya mapema mwezi huu.
Watafadhiliwa kufanikisha majaribio ya miundo msingi waliozindua kwa kipindi cha miezi sita ijayo.
‘’Nimefurahia kwamba studio ya kwanza iliyoshikanishwa ya BBC Afrika inalengo la kuchochea vipaji vya ubunifu hapa hapa barani'' alisema
Dmitry Shishkin mhariri wa BBC wa maswala ya kiteknolojia ya dijitali.
Bwana Shishkin alikuwa miongini mwa wakaguzi katika mashindano hayo ya ubunifu.
Timu mbili zilizochaguliwa zilikuwa zimepeana natharia mahsusi ya jinsi ya kuwafikia vijana kupitia mfumo huu wa kidijitali.
Kundi la Go Sheng lilipendekeza kuwafikia wasilikizaji na watazamaji wa BBC kupitia lugha ya mtaani iitwayo ''Sheng''
Nahodha wa kundi hilo Euticus Mola alisema kuwa wanatazamia kuwafikia vijana kupitia kwa lugha ya sheng.
Aidha wapinzani wao Ongair nao walipendekeza kufungua njia za mawasiliano na vijana kwa nia ya kuwakutanisha vijana na kuelewa matakwa yao.
Kiongozi wa kundi hilo Trevor Kimenye 30 aliiambia BBC kuwa mbinu hiyo anahakika itawezesha vijana kujieleza.
Share:

Vikombe vya kahawa vinavyoliwa..


Maduka ya kuuza vyakula kote duniani KFC yamezindua kikombe cha kwanza duniani cha kahawa ambacho kinaliwa.
KFC imezindua kikombe hicho ambacho kimeundwa kutokana na Chokoleti iliyochanganywa na Biskuti.
Vikombe hivyo pia vimewekwa harufu ya kupendeza ya mnazi.
Vikombe hivyo vinavyoitwa ‘’Scoff-ee-cup’’ vinautamu uliyotengenezwa kutoka biskuti ya kipekee iliyofungwa na karatasi ya sukari safi ya chokleti ,inayoweka kahawa kuwa moto.
Lakini baada ya muda chokleti hiyo inaanza kuyeyuka kwa hivyo inakupasa ule ‘’kikombe ‘’chako kwa haraka.
Ikitengenezwa kwa ushirikiano wa wanasayansi maarafu wa vyakula ’’The Robbin Collective’’,vikombe hivyo vya kahawa ambavyo ni asilimia mia

mmoja vinaweza liwa zimetengenezwa na harufu nzuri inayoweza kusisimua .
Aidha upishi na viungo vya Robbin collective ‘’siyo tu kuwa vikombe hivyo bali pia vina ladha nzuri mbali na harufu ya kupendeza’’alisema Jocelyn
Bynoe ambaye ndiye meneja wa mauzo wa kampuni hiyo.
Vikombe hivyo vya kahawa vimebuniwa kuadhimisha kahawa nzuri ya ‘’Seattle’’iliyotengenezwa kutokana na kahawa aina ya Arabica .
'Scoff-ee Cups' haziko katika maduka yao kwani bado zinafanyiwa majaribio ya ubora wa bidhaa.
Share:

Upandikishaji wa kichwa sasa unawezekana..


Unaposikia habari hii utadhani ni maudhui ya filamu ya kutisha ,lakini wanasayansi wanaamini upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwengine huenda ukafanikiwa.
Madaktari watazindua mradi huo katika kongamano wakati wa msimu wa joto ,kwa lengo la kuanzisha utaratibu huo mnamo mwaka 2017.
Mtu atakayeongoza mpango huo ni daktari raia wa Italy Sergio Canavero kutoka kundi moja la wanasayansi mjini Turin.
Anaamini kwamba upandikishaji wa vichwa vya watu utawasaidia wanaosumbuliwa na magonjwa ya misuli na saratani.
Baada ya kutoa wazo hilo mnamo mwaka 2013,daktari Canavero anaamini vikwazo vikuu vya upasuaji huo vimekabiliwa ,kulingana na ripoti mpya ya wanasayansi.
Vikwazo hivyo ni pamoja na usimamizi wa uti wa mgongo kuingiliana na kichwa kipya pamoja na kuhakikisha kuwa kinga ya mwili haikikatai kiungo hicho kipya.
Daktari Canevaro alichapisha taarifa iliokuwa na nadharia kuhusu vile anavyoamini upasuaji huo unaweza kufanyika.
Share:

Wapiganaji wa IS wavunja sanamu Iraq...


Wapiganaji wa Islamic State wametoa kanda ya video inayowaonyesha wakivunja sanamu ndani ya makavazi katika mji wa Mosul nchini Iraq.
Video hiyo inaonyesha wanaume kadhaa wakiwa katika chumba kimoja cha makavazi ya kitaifa wakiangusha na kuharibu sanamu ziliko ndani,
Moja baada ya nyingine sanamu hizo zilizoundwa kwa njia maalum, zilirushwa na kutapakaa kila mahala.
Kisha wanaharibu sakafu na kisha sanamu za watu walioshika visu zikigongwa na kuharibiwa kabisa.
Miongoni mwa sanamu zilizoharibiwa ni pamoja na sanamu ya fahali iliyotengenezwa karne ya tisa kabla ya kuja kwa yesu kristu.
Mmoja wa wanamgambo hao anasikika akisema kuwa sanamu hizo ni miungu bandia na kusema kuwa mtume Mohammad, aliamuru kuwa vitu kama hivyo viharibiwe kabisa.
Share:

Bomu lazua taharuki uwanjani Dortmund.....


Bomu la vita vya pili vya dunia ambalo halijalipuka limepatikana katika uwanja wa Borussia Dotmund.
Bomu hilo lililoripotiwa na mwandishi wa DW nchini Ujerumani linadaiwa kuwa na chimbuko la Uingereza na sasa kuna mpango wa kulivunja makali.
Ugunduzi huo unajiri saa kadhaa kabla ya mkufunzi wa kilabu hiyo Jurgen Klopp kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya mechi ya siku ya jumamosi na kilabu ya Shalke.
Watu waliokuwa karibu na uwanja huo unaobeba takriban watu 80,720 waliondolewa.
Haijulikani ni kwa mda gani eneo hilo la uwanja litakuwa haliendeki walisema wamiliki wa kilabu hiyo waliofunga eneo la mashabiki pamoja na makavazi ya kilabu hiyo.
Share:

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC (Bensouda) awasili Uganda....


Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda amewasili nchini Uganda ili kutafuta ushahidi kuhusu kesi ya aliyekuwa kamanda mkuu wa wapiganaji wa LRA nchini Uganda .
Dominic Ongwen ambaye alisema alitekwanyara na LRA akiwa mtoto alifikishwa mbele ya mahakama ya ICC mjini Hague mnamo mwezi Januari akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Mwandishi wa BBC mjini Kamapala anasema kuwa Bensouda atazuru kazkazini mwa Uganda katika ziara ya siku tano ili kuzungumza na mashahidi mbali na kutembelea maeneo yaliotekelezewa uhalifu huo.
Pia anatarajiwa kukutana na rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mahakama hiyo ya ICC akiishtumu kwa kuwabagua viongozi wa Afrika.
Share:

Mchinjaji wa IS 'Jihadi John' atambuliwa..



Mwanaume ambaye amekuwa akitekeleza mauaji ya mateka wa kundi la wapiganaji wa Islamic State ajulikanaye kwa jina la utani "Jihadi John",ametambuliwa.
Bwana huyo ambaye taswira yake akiwachinja mateka kwa kisu bila huruma ndiyo nembo ya wapiganaji hao sasa ametambuliwa kuwa anatokea Uingereza.
Shirika la Habari la BBC limetambua kuwa jina lake kamili ni Mohammed Emwazi.
Emnuazi ameonekana kwenye video kadhaa ya mauwaji ya mateka wa mataifa wa magharibi, akiwemo Mmarekani James Foley, Raia wa Uingereza, Alan Henning na mwaandishi habari wa Japan, Kenji Goto.
Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London.
Yamkini Emnuazi aliyezaliwa Kuwaiti na mwenye umri wa kati ya miaka 20 -29 alikuwa amefahamika sana na vyombo vya usalama lakini kwa sababu za kiusalama haikuwezekana kumtambua.
Anaaminika amewahi kuishi Somalia mnamo mwaka 2006 na anauhusiano mkubwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabab nchini humo.
Polisi nchini Uingereza imeziomba vyombo vya habari kutosambaza habari ambazo hawajazithibitisha kumhusu jamaa huyo kwani uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo bado habari za kina kumhusu Jihadi John hazijatolewa.
Mwandishi wa maswala ya Usalama wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa vyombo vya usalama vya serikali za mataifa yanayokaribia Somalia sasa yana kila sababu ya kutahamaki.

Kwa sababu Kuhusika kwake na kundi la Al Shaabab kisha akajiunga na kundi la Islamic State ambalo kwa wakati mmoja lilikuwa linashindana na wanamgambo wa Al Qaeda kuhusu yupi kati yao anayeushawishi
mkubwa
Ishara kuwa Al Shabab inazingatia msimamo mkali wa kidni hata zaidi ya Al Qaeda.
Kwa sababu itakumbukwa kuwa Al Qaeda ilipinga hatua kali ya kuwachinja mateka nchini Iraq na Syria.
Emnuazi ambaye amekuwa akiwabeza mataifa ya Magharibi kabla ya kuwakata shingo naaminika kuwa mtaalamu wa maswala ya kompyuta alisomea chuo kikuu cha Westminster.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC bwana huyo anaaminika kuwa alikwenda Syria mwaka wa 2012, lakini kabla ya wakati huo majasusi wa Uingereza na Marekani walikuwa hawajajua tishio lake.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.