Friday 21 November 2014

Basi linalotumia kinyesi lazinduliwa.......





















Basi la kwanza nchini Uingereza linalotumia kinyesi na uchafu unaotokana na chakula limeanza safari yake ya kwanza>>>>>INGIA HAPA<<<<<
Share:






wanawake wakiandamana huku wakiomboleza nchini Uganda
shughuli za mazishi ya mtoto wa miaka miwili zimefanyika nchini Uganda, mtoto ambaye kifo chake kimezua ghadhabu baada ya mtoto huyo kugongwa na gari la halmashauri ya jiji la Kampala ,baada ya mama yake kukamatwa akiuza matunda kinyume cha sheria.
Familia ya Ryan Ssemaganda na wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika mtoto huyo mpaka maofisa hao watakapo wajibika kwa kitendo hicho.Mwili wake ulichukuliwa wakati wakiandamana kuelekea bungeni siku ya alhamisi.
Raia wa Uganda wanaona kuwa halmashauri hiyo inatumia nguvu nyingi kupambana na wachuuzi wa mitaani.
Mama wa mtoto Ryan alikamatwa siku ya jumatatu baada ya kukutwa akiuza matunda huku akiwa hana leseni.
Siku iliyofuata, Bibi wa mtoto huyo alimpeleka katika Ofisi za Mamlaka ya mji wa Kampala ambako mama mtoto alikuwa akishiliwa , nia ilikua kumpa mama mtoto ili amnyonyeshe.
Maafisa wa Ofisi hiyo walikataa na wakati wakijadiliana kuhusu hilo, mtoto alichoropoka kutoka kwa mama yake na kugongwa na gari linalomilikiwa na Mamlaka hiyo.

Siku ya Alhamisi polisi ilizuia kupelekwa kwa mwili katika Bunge, wakisisitiza mwili huo uzikwe ili marehemu apumzike kwa amani, na kuwataka waepuka jambo hilo kushughulikiwa kisiasa.
Share:

Mkanyagano hatari wawaua 11 Zimbabwe.......

Watu 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufnayika katika uwanja wa soka.
Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga baadhi ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.

Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea vifo hivyo alihuzunika sana.
Share:

Shambulio laua tena Mombasa Kenya.....source BBC

Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya. Polisi walipambana na vijana walioingia katika Msikiti wa Swafaa eneo la Kisauni na mpaka sasa zaidi ya vijana 400 wanashikiliwa tangu kuanza kwa msako huo, mapema wiki hii.
Mwandishi wa BBC, Emmanuel Igunza anasema Msikiti huo ulifungwa jana baada ya polisi kuuvamia Jumatano, ambamo walipata magruneti, mabomu ya petroli na silaha nyingine. Hali ya wasi wasi bado imetanda katika mji huo wa pwani. Serikali imekwishafunga misikiti minne ambayo wanasema ina uhusiano wa watu wenye misimamo mikali ya imani ya kidini.
Pamoja na kukamata silaha mbalimbali, polisi pia walikamata bendera nyeusi, alama ya kuunga mkono kundi la kigaidi la Al-Shabab la nchini Somalia

Awali polisi mjini Mombasa pwani ya Kenya walisema wamepata silaha nyingine zaidi yakiwemo mabomu katika msikiti wa tatu ambao ulifanyiwa upekuzi                                               Msako huo katika msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni unakuja baada ya msako mwingine wa Jumatatu ambapo polisi pia walipata silaha ndani ya msikiti ambao wanasema hutumika kutoa mafunzo yenye itikadi kali.
Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihami kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha nyingine.
Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema kuwa msako huo ulifanywa katika misikiti ambayo hutumiwa na watu wanaoeneza itikadi kali za kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa wanajiunga na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.
Viongozi wa kiisilamu wamelaani misako hiyo katika Misikiti wakisema kuwa itachochea zaidi vijana kuendeleza itikadi kali za kidini.
Share:

Rais Obama awatangazia neema wahamiaji.....source BBC


Rais Barack Obama amelihotubia taifa kueleza mageuzi makubwa katika mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Amesema atachukua hatua za kikatiba kutoa ruhusa ya muda kisheria kwa takriban wahamiaji haramu milioni tano. Obama amesema nchi hiyo ilijengwa kwa uhamiaji na ameshutumu wanachama wa Republican kwa kuzuia mageuzi hayo. Wanachama hao wametishia kuchukua hatua.
Amesema watakaohalalishwa watalazimika kulipa kodi na wasiwe na rekodi ya uhalifu. Hata hivyo amesema urejeshwaji makwao kwa watu wenye makosa utaharakishwa.
Bwana Obama ametangaza mpango wake, ambao anaupitisha bila baraza la Congress, katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni.
Kwa upande wao wajumbe wa Republican wamesema hatua ya Rais Obama inavuka mipaka yake na uhusiano na rais utaingia dosari
Kuna wahamiaji wasio halali wapatao milioni 11 nchini Marekani na mwaka huu watoto wanaovuka mpaka wamesababisha tatizo.
Rais Obama ameliambia taifa kuwa kile anachopendekeza sio msamaha
"Ninachokieleza ni uwajibikaji - akili ya kawaida, mtazamo wa kawaida," amesema.
"Kama unatimiza vigezo, unaweza kujitokeza na kuishi maisha ya kawaida ukiendana na sheria."
"Iwapo ni mhalifu utarejeshwa ulikotoka.Kama unapanga kuingia Marekani kinyume cha sheria, nafasi ya kukamatwa na kurejeshwa ulikotoka ni kubwa." anasema Rais Obama.
Rais Obama amesema mfumo mpya wa uhamiaji utawawezesha watu wanaoishi nchini Marekani kinyume cha sheria, kujulikana na kuchangia katika uchumi wa taifa kwa kuwa watakuwa huru kufanyakazi.
Kuamuru kufanyika kwa mageuzi hayo kumesababisha malalamiko ya hasira kwa wanachama wa Republicans ambao wanasema hatua hiyo ni kutolishirikisha baraza la Congress na kuendesha mambo kwa mfumo wa Kifalme. Baadhi wanasema hawatatoa ushirikiano katika maeneo mengine ya kisera, na wengine wamemtaka Bwana Obama ashitakiwe.

Rais Obama anasema anachukua hatua hiyo kwa sababu baraza la Congress mara kadha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu limeshindwa kurekebisha mfumo wa uhamiaji ambao umeharibika.
Share:

Msichana kutoka Syria ashitakiwa.....

Monique akiwa mbele ya TV akiomba binti yake kurejea nyumbani Uholanzi miezi miwili iliyopita
Msichana wa kiholanzi aliyerejea kutoka Syria ambako alikwenda huko kujiunga na wapiganaji wa jihadi lakini baadaye alirudishwa nyumbani na mamake anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kushukiwa kutishia usalama wa taifa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19, akijulikana kama Aicha, alikamatwa aliporejea nyumbani kwao katika mji wa Maastricht.
Aicha, aliyebadili dini hivi karibuni kuwa Mwislam, anaaminika kusafiri kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State (IS) katika ngome ya Raqqa nchini Syria kuoana na mpiganaji mmoja.
Mama yake Monique alisaidia kumrejesha nyumbani Uholanzi na si mtuhumiwa.
Aicha ni mmoja wa idadi ndogo ya wasichana na wanawake kutoka Ulaya ambao wamekwenda Syria na Iraq katika miezi ya karibuni.
Baadhi wanaaminika kusafiri kwenda hukokupata mafunzo ya kiitikadi, wakati wengine wanasemekana kuoana na wapiganaji, wakiwemo wanaopigana bega kwa bega na wapiganaji wa IS.
Mahakama nchini Uholanzi Ijumaa itasikiliza kesi hiyo bila wasikilizaji na itaamliwa Aicha anaweza kushikiliwa kwa muda gani.

Upande wa mashitaka unatarajiwa kumwomba jaji kuongeza muda wa kumshikilia Aicha wakati wakichunguza ushahidi.
Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.