Mwandishi wa BBC, Emmanuel Igunza anasema Msikiti huo
ulifungwa jana baada ya polisi kuuvamia Jumatano, ambamo walipata
magruneti, mabomu ya petroli na silaha nyingine. Hali ya wasi wasi
bado imetanda katika mji huo wa pwani. Serikali imekwishafunga
misikiti minne ambayo wanasema ina uhusiano wa watu wenye misimamo
mikali ya imani ya kidini.
Pamoja na kukamata silaha
mbalimbali, polisi pia walikamata bendera nyeusi, alama ya kuunga
mkono kundi la kigaidi la Al-Shabab la nchini Somalia
Awali polisi mjini Mombasa pwani ya Kenya walisema
wamepata silaha nyingine zaidi yakiwemo mabomu katika msikiti wa tatu
ambao ulifanyiwa upekuzi Msako huo katika msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni
unakuja baada ya msako mwingine wa Jumatatu ambapo polisi pia
walipata silaha ndani ya msikiti ambao wanasema hutumika kutoa
mafunzo yenye itikadi kali.
Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihami
kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha
nyingine.
Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema
kuwa msako huo ulifanywa katika misikiti ambayo hutumiwa na watu
wanaoeneza itikadi kali za kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa
wanajiunga na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab nchini
Somalia.
Viongozi wa kiisilamu wamelaani misako hiyo katika
Misikiti wakisema kuwa itachochea zaidi vijana kuendeleza itikadi
kali za kidini.
0 comments:
Post a Comment