Sunday 9 November 2014

TAZAMA TASWIRA YA SAMAKI MTU(NGUVA) ALIYEFIA UFUKWENI

INGIA HAPA KUJUA ZAIDI>>>>AMAZING THINGS<<<<<
Share:

SHULE za msingi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa zimeongoza matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2014 kwa kushika namba moja hadi saba kati ya shule 10 bora kitaifa.


Jiji la Mwanza

Aidha, watahiniwa wamefaulu zaidi somo la Kiswahili na kufeli zaidi somo la Hisabati.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (NACTE), wavulana wameongoza somo la Hisabati kwa kupata alama 50/50, ambapo 26 wamefaulu kwa kiwango hicho na wasichana wakiwa wanane.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alizitaja shule 10 bora kuwa ni Twibhoki ya Mara ambayo imeshika nafasi ya kwanza, Mugini iliyoshika nafasi ya pili, Peace land na Alliance zote za Mwanza, Kwema (Shinyanga), St. Severine (Kagera), Rocken Hill (Shinyanga), Tusiime (Dar es Salaam), Imani (Kilimanjaro) na Palikas (Shinyanga).
Kwa upande wa mikoa iliyofanya vizuri kitaifa na asilimia zake za ufaulu kwenye mabano ni Dar es Salaam (46,434), Kilimanjaro (26,192), Mwanza (37,017), Iringa (14,650), Arusha (23,250), Tanga (26,261), Njombe (11,389), Kagera (24,501), Geita (17,560) na Mtwara (15,608).
Wilaya zilizoongoza kitaifa ni Mpanda Mji (Katavi), Biharamulo (Kagera), Moshi (Kilimanjaro), Kibaha (Pwani), Arusha (Arusha), Kinondoni (Dar es Salaam), Korogwe Vijijini (Tanga), Ilala (Dar es Salaam), Iringa (Iringa) na Mji Makambako (Njombe),” alisema Dk. Msonde.
Akizungumzia ufaulu wa kimasomo, alisema katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 0.64 na 8.94 ikilinganishwa na mwaka jana.
Watahiniwa wamefaulu zaidi somo la Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 69.70 tofauti na asilimia 69.06 ya mwaka jana, na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Hisabati lenye ufaulu wa asilimia 37.56 ambapo mwaka jana ilikuwa ni asilimia 28.62.
Katika somo la Kiingereza watahiniwa waliofaulu kwa mwaka huu ni asilimia 38.84 ikilinganishwa na mwaka jana asilimia 35.52 na Sayansi kwa mwaka huu waliofaulu ni asilimia 54.89 na mwaka jana asilimia 47.49,” alisema.
Dk. Msonde alisema jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 waliofanya mtihani huo wamepata alama 100 au zaidi katika alama 250 ambapo idadi hiyo ni sawa na asilimia 56.99.
Alisema kati ya watahiniwa hao, wasichana ni 226,483 ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909 sawa na asilimia 60.87.
Miongoni mwa watahiniwa hao waliofaulu, Dk. Msonde alisema wamo wenye ulemavu 795 wakiwamo wasichana 355 ambao ni sawa na asilimia 44.65 na wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35.
Katika mtihani huo uliofanyika Septemba 10 na 11, mwaka huu jumla ya watahiniwa 808,085 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwamo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83.
Kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 691 walikuwa na uoni hafifu, 87 walikuwa na ulemavu wa macho (wasioona), wenye matatizo ya kusikia 374, wenye mtindio wa ubongo 252 na watahiniwa 27 walikuwa na ulemavu zaidi ya mmoja,” alisema Dk. Msonde.
Pamoja na mambo mengine, NECTA imemfutia matokeo mtahiniwa mmoja aliyebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo. Mwaka jana watahiniwa 13 walifutiwa matokeo yao kwa kufanya udanganyifu.

Hata hivyo, Baraza hilo limesita kutoa matokeo ya shule zilizofanya vibaya kwa madai ya kuendelea na uchambuzi wa kuzitambua zaidi.
Share:

MAKINDA KUONGOZA UJUMBE WA BUNGE LA SADC KUMZIKA RAIS SATA LUSAKA, ZAMBIA



Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda.

Mwili wa Rais wa Zambia, Michael Sata umewasili Zambia tayari kwa mazishi ambayo yamepangwa kufanyika November 11,2014

Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda kesho tarehe 10 Novemba, 2014 ataongoza ujumbe wa Bunge la SADC kushiriki Misa Maalum ya kuombea mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Chilufya Sata katika misa maalum itakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mjini Lusaka, Zambia.
Katika ujumbe huo wa Bunge la SADC, Makinda ataongozana na viongozi wengine wa Bunge hilo ambao ni Spika wa Zimbabwe Mhe. Jaji Jacob Mudenda, Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete, Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Richard Msowoya Spika wa Bunge la Angola Mhe. Fernando da Piedade Dias dos Santos na Mwenyeji wao Spika wa Zambia Dkt. Patrick Matibini.
Kutoka secretariat ya makao makuu wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa Bunge Bunge la SADC Dkt. Essau Chiviya ataambatana na ujumbe huo kuwakilisha sekretariati ya Bunge hilo katika Misa hiyo Maalum Mjini Lusaka, Zambia.
Kwa mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Serikali ya Zambia, Misa hiyo Maalum ya kuombea mwili wa Rais Rata itanyika kesho tarehe 10 Novemba, 2014 na inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka kila kona ya dunia pamoja na viongozi mbalimbali wa Kimataifa watakaoziwakilisha nchi zao kabla ya kufanyika kwa mazishi yake ambayo yamepangwa kufanyika siku ya jumatatu tarehe 11 Novemba, 2014 mjini Lusaka.
Sata aliyekuwa na umri wa miaka 77 alifariki tarehe 29 Oktoba, 2014 jijini Londo Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo kifo chake kilitokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo, sherehe ambazo hakuweza kushiriki kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.
Sata ambaye alibatizwa jina la "King Cobra" na wafuasi wake wakati alipochaguliwa mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za Zambia na mtu ambaye alikuwa wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu kubwa na upinzania.

Makinda na ujumbe wake wanatarajia kurudi nchi siku ya jumatano baada kushiriki pia mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Novemba, 2014.
Share:

HOTUBA YA SHIGONGO YAWAKUNA WAHITIMU MLIMANI SCHOOL OF PROFESSIONAL STUDIES

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers  Eric Shigongo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo akiongoza maandamo maalumu yaliyoandaliwa na chuo hicho, kushoto ni Mkuu wa Chuo, Hassan Ngoma.
Shigongo akihojiwa na mwandishi wa chuo hicho cha Professional FM, Shikunzi Haonga ambaye ni mkuu wa kitengo idara ya habari mawasiliano kwa umma (hayupo pichani) ndani ya studio iliyopo chuoni hapo.
Shigongo akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa studio hiyo ya chuoni hapo.

Wahitimu wa Chuo cha Mlimani School Of Professional Studies walipata msisimko mkubwa  baada ya Mkurugenzi  Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo kutoa hotuba ambayo kila mmoja alijiona kuwa anaweza kujikwamua kimaisha kama wakijibidisha katika maisha yao ya kila siku.
Msisimko huo ulikua pale Shigongo alipotoa simulizi ya riwaya ya ombaomba mmoja aliyekuwa akiomba kila siku kwa  kutumia kopo,  kumbe kopo lile ni dhahabu yenye thamani ya mabilioni ya fedha kwenya mahafali ya pili katika chuo hicho.
Mmoja wa wahitumu ngazi ya diploma katika fani ya Habari na Mawasiliani ya Umma, Neema Kisimbo alimpongeza Shigongo kuwa ni kati ya Watanzania wachache waliopewa thawabu  na Mungu hata kama akifa leo atakuwa na la kusema kuhusu alivyoweza kuisaidi jamii.
“Baba huyu ana kipaji lakini mbali na kipaji chake pia kujituma kwake  kumefanya awe na mafanikio makubwa maana maisha ni malengo, si  kweli  kwamba ameenda kwa waganga,” alisema mhitimu huyo.
Katika mahafali hayo, Shigongo aliwatunuku vyetu wahitimu 119 katika Chuo cha Mlimani School of Profession Studies katika mahali yaliyofanyika katika chuo hicho hapo jana Mbezi Kwa Msugur jijini Dar es Salaam.
Wahitumu hao walifunzu katika kozi tofauti ndani ya chuo hicho ambapo kuna baadhi ya walipata ngazi ya cheti na wengine  katika ngazi ya diploma ambapo wote  hao walitunukiwa vyeti hivyo  na mkurugenzi  wa Global Publishars ambaye alikuwa  mgeni rasimi katika mahafali hayo.
Mkurugenzi huyo alitoa vyeti kwa  wahitimu 19 katika ngazi ya cheti kwa fani ya Manunuzi na Ugavi, Fani ya Habari na Mawasiliano ya Uma wahitimu ngazi ya cheti walikuwa 20,  Rasilimali Watu wahitimu 18, ngazi ya cheti wahitimu Uhasibu walikuwa 17 , Uongozi na Biashara ngazi ya cheti sita, Mauzo na Masoko ngazi ya cheti 3, Rasilimali Watu ngazi ya diploma sita , Uongozi wa Biashara diploma 10,  Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma ngazi ya diploma10.
Wengine ni wa Mauzo na Masoko ngazi ya diploma mmoja, Uhasibu ngazi ya diploma sita, Manunuzi na Ugavi ngazi ya diploma  wanne.
Mkuu wa chuo hicho, Hassan Ngoma alimtunuku Shigongo cheti cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ngazi ya Diploma kwa  mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari.
Share:

JK AFANYIWA UPASUAJI WA TEZI DUME

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. JakayaMrisho Kikwete akizungumza na Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya Johns Hopkins na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi(kulia) baada ya kuwasili katika Hospitali ya Johns Hopkins


iliyopo Baltimore, Maryland, Marekani kwa upasuaji Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.

Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Share:

MWAKIFWAMBA ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI MORO



RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba jana usiku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupata ajali na kupinduka eneo la Mkindu jirani na mizani mkoani Morogoro.
Mwakifwamba alipata ajali hiyo wakati akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki 'bodaboda' baada ya gari lake aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 176 CYM kupata pancha na kuanza kupoteza muelekeo. Katika gari hilo, Simon alikuwemo peke yake na alitoka salama salimini. Akiongea na tovoti hii kwa njia ya simu akiwa njiani kurudi Dar, Mwakifwamba alisema, "Ilikuwa majira ya saa 3 usiku wakati nikitokea mkoani…
Share:

Lowassa azindua helkopta ya kanisa la ufufuo na uzima, Askofu Gwajima ataka apewe eneo la Tanganyika Parkers

Joseph Zablon, Kawe Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameahidi kumsaidiana kwa maombi na njia zingine, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili aweze kulipata eneo la Tanganyika Pakers analolitumia kwa mahubiri ili ajenge kanisa kwa ajili ya waumini wake. Kauli ya Lowassa imefuatia ombi la askofu huyo wakati wa uzinduzi wa helkopta ya kanisa hilo ambayo ameahidi kuitumia kwa ajili ya kusaidia majanga yanapotokea na pia kusambaza neno la Mungu ambako alidai kuwa amesikia kuwa eneo hilo lipo katika mchakato wa kupatiwa mwekezaji. “Nasikia hapa kuna mtu anataka kulinunua hili eneo hivyo naomba sana ikiwezekana liuziwe kanisa langu ili liweze kujenga kanisa kwa ajili ya waumini” alisema Gwajima wakati anamkaribisha waziri mkuu mstaafu kuzungumza katika hafla hiyo. Alisema Lowassa kuwa ombi na kilio hicho amekisia na anahidi kushirikiana nao kuhakikisha wanapata ardhi kwa ajili ya kanisa hilo “Nitashirikiana nayi kwa maombi na njia zingine kuhakikisha mnapata ardhi kwa ajili ya kanisa hili” alisema. Alibainisha kuwa Gwajima ni mmoja kati ya viongozi wenye maono ambao kimsingi ndio wanaohitajika kwa ajili ya ustawi wa jamii.Awali  Askofu Gwajima alisema kuwa helkopta hiyo ni moja kati ya zingine mbili zinazotarajiwa mwakani kwa ajili ya huduma za kanisa na uokozi. Alisema kuwa ameshawishika kuinunua baada ya kuona abiria waliokuwa katika meli yam v Spice walivyopoteza maisha kutokana na kukosa msaada hali ambayo inawapata pia majeruhi wa ajali zingine ambao wengi hufariki dunia wakiwa njiani kukimbizwa hospitalini. waziri mkuu mstaafu, Mhe Edward lowassa akiwasili viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es salaam  kwa ajili ya uzinduzi wa helkopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima  jijini Dar es Salaam.

Mhe Edward lowassa akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
 waumini wakishuhudia uzinduzi wa helkopta hiyo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa 
akiikagua helkopta hiyo mara baada ya uzinduzi.





















Share:

Blog Owner

Blog Owner
FESTO MDEMU

Blog Archive

Flag


Total Pageviews

Translate

Powered by Blogger.