Joseph Zablon, Kawe Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameahidi kumsaidiana kwa maombi na njia zingine, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili aweze kulipata eneo la Tanganyika Pakers analolitumia kwa mahubiri ili ajenge kanisa kwa ajili ya waumini wake. Kauli ya Lowassa imefuatia ombi la askofu huyo wakati wa uzinduzi wa helkopta ya kanisa hilo ambayo ameahidi kuitumia kwa ajili ya kusaidia majanga yanapotokea na pia kusambaza neno la Mungu ambako alidai kuwa amesikia kuwa eneo hilo lipo katika mchakato wa kupatiwa mwekezaji. “Nasikia hapa kuna mtu anataka kulinunua hili eneo hivyo naomba sana ikiwezekana liuziwe kanisa langu ili liweze kujenga kanisa kwa ajili ya waumini” alisema Gwajima wakati anamkaribisha waziri mkuu mstaafu kuzungumza katika hafla hiyo. Alisema Lowassa kuwa ombi na kilio hicho amekisia na anahidi kushirikiana nao kuhakikisha wanapata ardhi kwa ajili ya kanisa hilo “Nitashirikiana nayi kwa maombi na njia zingine kuhakikisha mnapata ardhi kwa ajili ya kanisa hili” alisema. Alibainisha kuwa Gwajima ni mmoja kati ya viongozi wenye maono ambao kimsingi ndio wanaohitajika kwa ajili ya ustawi wa jamii.Awali Askofu Gwajima alisema kuwa helkopta hiyo ni moja kati ya zingine mbili zinazotarajiwa mwakani kwa ajili ya huduma za kanisa na uokozi. Alisema kuwa ameshawishika kuinunua baada ya kuona abiria waliokuwa katika meli yam v Spice walivyopoteza maisha kutokana na kukosa msaada hali ambayo inawapata pia majeruhi wa ajali zingine ambao wengi hufariki dunia wakiwa njiani kukimbizwa hospitalini. waziri mkuu mstaafu, Mhe Edward lowassa akiwasili viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es salaam kwa ajili ya uzinduzi wa helkopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima jijini Dar es Salaam.
Mhe Edward lowassa akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
waumini wakishuhudia uzinduzi wa helkopta hiyo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa
akiikagua helkopta hiyo mara baada ya uzinduzi.
0 comments:
Post a Comment